Header Ads

WABUNGE WA UKAWA NI WENDAWAZIMU?


WABUNGE WA UKAWA NI WENDAWAZIMU? 

Na Happiness Katabazi 
NOVEMBA 16 Mwaka huu,  Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia ( CHADEMA) Tundu Lissu alinukuliwa akisema leo UKAWA wataakikisha wanafanya vurugu kwa kusimama ndani ya bunge na kuakikisha Rais Dk.John Magufuli hatoweza kuhutubia Bunge kwasababu Rais Magufuli siyo Rais na wao hawamtambui.

Kweli Leo saa Kumi jioni tumeshuhudia wabunge wanaounda umoja wa UKAWA wakifanya Fujo ndani ya Bunge tangu alipoingia Rais Magufuli, Rais wa Zanzibar, Dk.Mohammed Shein, Makamu wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, Makamu wa Rais Tanzania Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassa , Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Jaji Mkuu wa Zanzinzibar .

Wabunge wa UKAWA wakiwa wamesima wakati wakifanya Fujo hizo ambazo zimewashushia heshima Mbele za watu wenye akili timamu ,wazalendo wa kweli walikiwa wakisikika wakisema " Maalim Seif ,Maalim Seif". 

Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na ambaye alikuwa ni mgombea urais Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 Mwaka huu, ambapo Tume ya Uchaguzi Zanzibar ( ZEC) ,ilibaini dosari Katika kura zilizopigiwa Zanzibar hivyo ikatangaza Kuufuta uchaguzi ule hadi tarehe nyingine serikali ya Zanzibar itakapotoa taarifa .

Tangu ZEC ifute Matokeo ya kura za Zanzibar tumeshuhudia Maalim Seif ,aliyekuwa mgombea urais Tanzania, Edward Lowassa ,Tundu Lissu na wana UKAWA wengine Mara Kadhaa wamejitokeza hadharani wakipinga uamuzi huo wa ZEC na kusema Hawatashiriki uchaguzi wa marudio.

Tukiachana na historia hiyo Turejee Katika mada yetu ya Msingi.Kwanza napenda Kusema kilichofanywa na Wabunge wa UKAWA Leo ni uhuni, na pia ni Ishara Mbaya kwa Wapiga kura waliowapigia kura wa aina hiyo kura zao zimepotea bure Kwani wameteua watu ambao ni wahuni maana mhuni anafanya vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria, mila na desturi na ndicho kilichofanywa na wabunge wa UKAWA Leo.

Kitendo cha UKAWA kufanya Fujo  wakati rais Magufuli anakuja kuzindua Bunge ni kumuonea na pia ni kutojielewa.

 Maana Ibara ya 38(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema " Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata Masharti ya Katiba hii".

Sasa Magufuli ni rais aliye chaguliwa na wanachi waliowengi kwa mujibu wa Katiba .Sasa ni ajabu kikundi kidogo cha Wabunge wa UKAWA kinaibuka kinaanza kudharau maamuzi ya wananchi waliowengi waliomchagua Magufuli na Dk.Shein kuwa marais wetu.

Inashangaza sana hawa wabunge wa UKAWA ambao ni watunga wa Sheria ndiyo wamekuwa mstari wa Mbele kuvunja hizo Sheria ambazo zinasema Matokeo ya rais hayapingiwi nje ya Mahakama na ndani ya Mahakama.

Ibara ya 28 (2) (a)ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 inayozungumzia muda wa kuendelea na urais  inasema ; "  Kuongezwa kwa kipindi cha miaka mitano. 

(2) Kufuatana na maelezo ya kijifungu (1) cha kifungu hiki, Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano kuanzia tarehe, ambapo:
(a) kama yeye ni mtu ambaye ndiye mara ya kwanza amechaguliwa kuwaRaischiniyaKatibahiialipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais; n.

Hivyo matakwa ya Ibara hiyo  Kuwa  kama uchaguzi Mkuu utafanyika na mshindi  wa kiti cha  Urais atatangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.

Sasa Zanzibar ,ZEC ilifuta Matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 , na Rais aliyekuwa akimaliza muda wake ni Dk.Shein lakini kwakuwa ZEC ilifuta Matokeo ya uchaguzi hivyo Ibara ya 28(2)(a) ya Katiba ya Zanzibar ina mpa muda wa kisheria Dk.Shein kuendelea kushika wadhifa huo.


Ili  Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, ZEC  inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.

Kitendo cha UKAWA kufanya Fujo  wakati rais Magufuli na Rais Shein anaingia kuzindua  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumuonea na pia kumethibitisha wabunge wa UKAWA hawajielewi. 

Hivi Nyie wabunge wa UKAWA mnawazimu kichwani ?Mnaposema hamtambui Dk.Shein Kuwa ni Rais wa Zanzibar huyo Maalim Seif ananukuliwa akisema AMEOIOMBEA kufanya mazungumza na Rais Shein.

Sana Huyo Maalim Seif mnayemuita ni rais Tuonyesheni lini ZEC imemtangaza Maalim Seif ni rais wa Zanzibar ? Huo uhalali wa Nyie kumuita Maalim Seif ni rais mmepata wapi na kwa mujibu wa Katiba na Sheria hipi?

Ndiyo maana Minajiuliza kwamba hivi wabunge wa UKAWA uwenda ni wendawazimu.Kama Maalim Dk.Shein siyo rais wa Zanzibar basi Maalim Seif naye siyo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar maana hadi sasa Maalim Seif ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

UKAWA mlijiapiza Kuwa Leo mtaakikisha Rais hatoweza kuhutubia kutoka na Fujo mtakazo fanyia, sasa kwanini mmeshindwa kusimamia msimamo wenu huo wa kihuni na kuingia woga nakuamua kuingia woga baada ya kumuona Spika wa Bunge Job Ndugai kuwageuzia kibao?

Mashujaa gani Waoga? Nijuavyo Mimi Jemedari uwa haogopi wala hatishiki kwa maneno?Sasa Nyie mlijifanya majemedali  kuwa mtaakikisha Rais Magufuli autubii sasa mbona mmeshindwa kumzuia?

Kama mlijua nyie ni waoga wa mkono wa sheria hamtofanikiwa kumzuia Rais Magufuli  asihutubie Bunge Leo kwanini mliingia bungeni na kufanya Fujo kidogo  tu na mkashindwa kufanikiwa kudhibiti rais asihutubie?

Ombi langu kwa Uongozi mpya wa Bunge jipya ,kutokana na vitendo hivi Vya kihuni ambavyo vilishamiri na kukumbatiwa sana Enzi za Bunge la serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Leo Katika Hili Bunge jipya la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.Magufuli  vione Haja sasa ya kutunga Kanuni Kali za kuwabana wabunge wanaofanya vitendo Vya kihuni ndani ya Bunge kama uhuni uliofanywa na wabunge wa UKAWA Leo .

Aiwezekani mbunge aliyechaguliwa na wananchi anafika bungeni anashindwa kujiheshimu ,kuwawakilisha wananchi wanaamua Kujitoa fahamu nakuanza kufanya matendo ya kihuni na ya kiuwenda wazimu halafu eti hamna Kanuni za kuwabana wabunge wahuni wa aina hiyo Spika anaishia Kusema tu ' eti wabunge wanaofanya Fujo toka nje'.

Hii haitoshi,kuna haja ya Kufungwa Kanuni ambazo zitasema mbunge atakayefanya Fujo bungeni afungiwe kuingia bungeni na akafunguliwe Kesi Katika Mahakama za kiraia.Upuuzi huu unaofanywa Mara kwa Mara na wabunge hasa wa Chadema, CUF unawadhalilisha viongozi wetu, Bunge letu na pia kuwashushia hadhi wabunge walioufanya uhuni huo.

Hotuba iliyotolewa Leo na Rais Magufuli Leo ambayo ili nzuri na imetoa mwelekeo wa serikali yake na kwa mujibu wa Spika Ndugai amesema hotuba hiyo ikajadiliwa Katika kikao kijacho.

Swali langu Je hawa wabunge wa UKAWA ambao wameshindwa kusikiliza hotuba ya Rais Magufuli bungeni Leo, sasa Je ukifika wakati wa hotuba yake kujadiliwa bungeni Je nao wanachangia maoni Yao Kwenye hiyo hotuba ambayo Imebadili mambo mengi kuhusu wananchi wa taifa hili wakiwemo Wapiga kura wao?

Wabunge wa UKAWA mnatakiwa kukomaa kisiasa  Kwani mlichaguliwa na wananchi ili mkawatumikie ndani ya Bunge lakini Leo mmejishushia hadhi  kwa kufanya fujo ndani ya Bunge .

Mnaitaji Kuwa na mikakati ya maana si kwa faida yenu tu baki kwa faida ya wananchi na Ustawi wa taifa kwa ujumla.Jifunzeni kumpinga mtu kwa kufuata staha,Sheria na Kanuni.

Bunge ni Chombo Kilichoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .

Aidha Ibara  64(1)ya Katiba hiyo inasema: "  Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuw mikononi mwa Bunge".

Mtu  mwenye stahaa ,anayejitambua Kuwa yeye ni kiongozi yaani mbunge ambaye ni myunga sheria, anayejiheshimu  hawezi kuamua kufanya uhayawani kama uliofanywa leo na wabunge wa UKAWA ndani ya bunge letu tukufu.

UKAWA eleweni uchaguzi umekwisha aliyeshinda kashinda,aliyeshindwa kashindwa.Yaliyopita yamepita ,rejesheni mshikamano wenu wabunge wote bila kujali itikadi za vyama kwa lengo la kuletea taifa maendeleo.

Maana kama Mnasema hamtambui  Rais Magufuli kwanini nyie wabunge wa UKAWA jana mlikubali kushiriki uchaguzi wa Waziri Mkuu ndani ya Bunge?Maana jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lililetwa Bungeni ili mlithibitishe na Rais Magufuli ambaye mmedai hamtambui.

WABUNGE wa UKAWA ebu acheni wazimu ,fanyenikazi kwa maslahi ya wananchi waliowatuma bungeni.Na Nyie wabunge wa CCM baadhi yenu acheni tabia ya kurusha vijembe kwa wabunge wa upinzani Kwani Bunge Hilo siyo la vyama ni Bunge la wananchi. 
UKAWA ni wendawazimu maana mwendawazimu ufanya matendo tofauti na ya kushangaza mbele ya jamii ya watu wenye akili timamu.Na wabunge wa UKAWA leo wamefanya kitendo cha sawa na wendawazimu.Naomba kutoa hoja.


Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
20/11/2015.

No comments:

Powered by Blogger.