RAIS MAGUFULI UMEINGIA CHAKA
Na Happiness Katabazi
IBARA ya 72 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema ;
"Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa Serikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g) ataamua:-
(a) kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au wa nafasi nyingine yoyote chini ya Katiba hii;
(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa kinyume na masharti ya ajira,
mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea uongozi katika chama cha siasa.".
Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya nchi inasema ; " ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
Kanuni ya Utumishi wa Umma ( Gorvement Standing Order ya mwaka 2009 ya 20(2) (e) inakataza Wakili wa Serikali asijihusishe na siasa.
Nimelazimika kuanza na nukuu za Ibara hizo za Katiba na Kanuni hiyo ya Utumishi wa umma kwasababu makala yangu Leo itamjadili hasa masuala Kadhaa ikiwemo taarifa ya Msemaji wa serikali Assah Mwambene ambaye alisema Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Jana hiyo hiyo akasema amepokea uteuzi wa rais Magufuli Kuwa amemteua Dk.Ackson Kuwa Mbunge .
Sasa taarifa ya Msemaji wa serikali Mwambene Jana inasema Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali Dk.Ackson wakati Ibara ya 72 ya Katiba ya nchi inasema ; Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa Serikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g) ataamua:-
Ibara ya 72(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa kinyume na masharti ya ajira, mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea uongozi katika chama cha siasa.".
Kwa maana hiyo utumishi wa umma wa Dk.Ackson ulikoma Novemba 11 Mwaka huu alipoenda kuchukua fomu ya Kugombea Uspika.
Hivyo basi Rais Magufuli kwa mujibu wa Ibara ya Ibara 72(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977 ,hajatengua uteuzi huo ,kwasababu Ibara hiyo inasema wazi kabisa mtumishi wa umma mwenye aina ya Cheo kilichotajwa Katika Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya nchi akigombea Uongozi wa ngazi yoyote Katika Chama cha siasa kinyume na Masharti ya ajira kama alivyofanyiwa Dk.Ackson ,mtu Huyo atahesabiwa Kuwa utumishi wake umekoma tangu tarehe yake ya Kuwa mgombea uchaguzi au ya Kugombea Uongozi Katika Chama cha siasa.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 20(2)(e) ya Utumishi wa Umma Dk.Ackson alikuwa na cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ulikoma siku alipoenda kuchukua fomu ya kugombea uspika Novemba 11 mwaka huu na Novemba 14 mwaka huu, Kamati Kuu ya chama chake CCM kilipoteua jina lake, Job Ndugai na Dk.Mwinyi kugombea uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo hata hiyo jana Dk.Mwinyi,Dk.Ackson walitangaza kujitoa na kumuacha Ndugai peke yake kama mgombea spika kupitia CCM.
Hivyo, basi kitendo cha Rais Magufuli kumteua Dk.Ackson kuwa mbunge wa kuteuliwa na kutuambia kwamba ametengua uteuezi wake kama Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali si sahihi kwa sababu kwa mujibu wa sheria nilizo zinukuu hapo juu alishasita kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kabla ya Jana rais kutengua uteuzi wake.
Alichokifanya Rais Magufuli ni kuthibitisha tu labda kuwa Dk. Ackson hafai kuendelea kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivyo hata kumteua kuwa mbunge si jambo sahihi sana hasa katika ulimwengu huu wa demokrasia ya vyama vingi licha Rais anayo mamlaka ya Kumteua kuwa miongoni mwa wabunge 10 wanaoteuliwa na rais kama ilivyoanishwa Katika Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Nchi.
Itakumbukwa Kuwa Novemba 15 Mwaka huu, baada ya Kamati Kuu ya CCM kuteua majina matatu ya makada wake Kuwa miongoni mwa wagombea wa uspika ambapo Majina hayo yalipaswa yapelekwe Jana Katika Kikao cha wabunge wa CCM ili jana hiyo hiyo lipatikane jina Moja tu la mgombea wa CCM ambalo litaenda kushindana na wagombea Uspika wa vyama Vya upinzani.
Sasa cha kushangaza Jana asubuhi ilitolewa taarifa ya kwa umma Kuwa Rais ametengua uteuzi wa Dk.Ackson na wakati huo huo Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila akatangazia umma kuwa amepokea taarifa za uteuzi kuwa Rais Magufuli amemteua Dk.Ackson Kuwa Mbunge wa kuteuliwa .
Na saa Chache baadae Jana hiyo hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa Habari Kuwa aliyekuwa mgombea Uspika Dk.Ackson na Dk.Mwinyi wamejitoa Katika kinyang'anyiro hicho cha uspika hivyo wameacha Ndugai Kuwa mgombea pekee ambaye amepita bila kupingwa na saa Chache baadaye Jana hiyo eti Dk.Ackson ameenda kuchukua fomu za Kugombea nafasi ya unaibu Spika kupitia CCM.Mmhhhh.
Watu tunaofikiri sawa sawa tumeona matukio hayo manne yaliyotokea ndani ya saa zisizo zaidi nane kwa siku Moja tu yaani Jana yanayomhusisha Dk.Nackson ya rais kutengua uteuzi wake, rais Kumteua Ubunge, yeye Dk.Nackson Kujitoa dakika za mwisho Katika kinyang'anyiro Uspika na Dk.Ackson kwenda kuchukua fomu ya Naibu Spika ,siyo ya kawaida na ya nachezwa na watu wazito hasa ambayo mwisho wa siku yameanza kumchafulia sifa Magufuli ambaye Mara zote Katika kampeni zake alikuwa alidai atalinda Sheria za nchi .
Hivi kwanini Magufuli umeamua kujiingiza Katika mtego huu mchafu mapema kiasi hiki? Rais Magufuli sikufichi umeanza kujitia madoa na baadhi ya watu Taratibu Tumeanza kukutilia Shaka ?
Huyu Dk.Ackson kavunja wazi wazi Sheria hiyo ya Utumishi wa umma lakini wewe Rais Magufuli ambaye wakati ulipolishwa kiapo na Jaji Mkuu, Othman Chande ,Novemba 5 Mwaka huu pale Uwanja wa Taifa uliapa Kuwa utailinda na kuifadhi Katiba , sasa huku Kumteua Dk.Ackson ambaye amevunja Sheria ya utumishi wa umma wazi wazi na kuiletea sifa mbaya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujiingiza Katika siasa wakati akijua hatakiwi kuvunja Sheria.
Najua kuna watu hamtaelewa kwa nini nasema Dk.Ackson amekiuka sheria kugombea uspika wakati yeye ni mwanasheria wa serikali katika cheo cha Naibu mwanasheria Mkuu.
Ni hivi, makatazo ya kisheria juu ya watumishi wa umma kujihusisha na siasa yamegawanyika katika sehemu mbili, ambayo yanafanya watumishi wa umma wagawanyike katika makundi mawili.
Kundi la kwanza la watumishi wa umma kwa mujibu wa kanuni ya 20 ya kanuni za utumishi wa umma, hawa ni marufuku kabisa kujihusisha na siasa. Kwa maana nyingine hata kama walipoteuliwa walikuwa wanachama wa vyama vya siasa, mara baada ya uteuzi wanapaswa kurudisha kadi zao au kusitisha uanachama wao. Katika kundi hili wapo askari wapo majaj, mahakimu, wanasheria wa serikali, watumishi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi.
Kundi la pili, ni watumishi wa kawaida ambao sio askari wala hao niliowataja hapo juu.
Hawa wanaruhusiwa kujihusisha katika mambo ya siasa, yaani kuwa wanachama na kushiriki shughuli zote za kisiasa isipokuwa tu, hawaruhusiwi kugombea uongozi kwenye vyama vyao vya siasa, nahata pale watakapogombea kwenye nafasi za kisiasa utumishi wao unakoma baada ya kuteuliwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na rais kuwa wabunge. Dk.Ackson hayupo kwenye kundi hili. Yeye yupo kwenye kundi la kwanza.
Alichofanya Dk.Ackson ni sawa na leo hii ajitokeze jaji wa Mahakama Kuu akiwa jaji hivyo hivyo aende kuchukua fomu ya kugombea uspika kwa tiketi ya CHADEMA au CCM kisha apitishwe kabisa na chama chake.
Baada ya hapo Rais ndio aseme nimefuta uteuzi wa mamlaka yako kama jaji, ila nakuteua kuwa mbunge, kwa mujibu wa katiba. Hii si sahihi hata kidogo.
Je hivi ndiyo rais Magufuli anatuonyesha jinsi anavyotekeleza matakwa ya kiapo cha kulinda Sheria za nchi alizoapa kuzilinda kwa kumtunuku fasta fasta Ubunge wa kuteuliwa Dk.Ackson ikiwa ni saa Chache tangu utengue uteuzi wake ambao hata hivyo pia umma haujaelezwa Sababu za rais kutengeua uteuzi wa Dk.Ackson ambaye aliteuliwa Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9 Mwaka huu na Novemba 11 akajiingiza Kwenye siasa kwenda kuchukua fomu ya kugombea uspika wakati akiwa mtumishi wa umma na Hukutangaza kujihudhuru?
Hivi rais Magufuli kwanini ukuona ni busara Kuwa ulipotangaza kutengua uteuzi wake ,ungetulia watu wasahau alichokitenda basi ipite hata miaka kadhaa au miezi fulani ndiyo umpe madaraka mengine watu wasingehoji na kuanza kukutilia mashaka .
Lakini rais wetu Magufuli unafahamu kabisa bado kuna mijadala ya wananchi kuhusu kilichotendwa na Dk.Ackson za kujihusisha na siasa wakati haruhusiwi kufanya hivyo,wewe sijui huku lions hilo au sijui umeliona ila kwasababu unazozijua umeamua kupuuza ukaamua kusema eti umetengua uteuzi wake na ghafla umemteua mbunge na muda huo huo Dk.Ackson kajitoa kwenye kugombea uspika badala yake kaenda kugombea unaibu Spika.
Hivi serikali na CCM mnafikiri Watanzania wote hatuna akili hadi tushindwe hata kung'amua usanii 'Perliament Drammer' unaoendelea hapo ambao sikufichi rais wangu Magufuli umekutia doa kabisa tena mapema.
Sawa Rais Magufuli unaweza Kusema wewe siyo Mpiga kura wa kumchagua Spika na Naibu Spika hivyo Katika hili hausiki.
Lakini Kwa mazingira ya matukio hayo manne yaliyofanyika siku Moja ya Jana yanayomhusisha Moja kwa Moja Dk.Ackson ni Ngumu sana watu kuamini Kuwa Ufahamu Sinema yote inayochezeka na huyo Dk.Ackson ambayo wajuzi wa mambo tumeng'amua muda mrefu na ndiyo maana nakutadharisha rais Magufuli Kuwa Katika hili watu wameanza kupata Mashaka na wewe Kuwa na wewe ndiyo wale wale na CCM ni ile ile.
Tunajiuliza ni lazima awe yeye tu? huku ameteuliwa akachukue fomu ya kugombea uspika, hapo hapo anateuliwa Kuwa Mbunge , halafu tena tunasikia amejitoa kugombea uspika
saa chache baadaye ameenda kuchukua fomu ya kugombea unaibu spika tena ndani ya siku Moja ya Jana?
Hivi, haiwezekani Dk.Ackson akatosha kuwa mbunge tu asubiri kwa imani aliyopewa na Rais labda atateuliwa kuwa waziri au aendelee kutumikia kama mbunge? iwaje tena kugombea unaibu spika? Hapa ndipo zinapokuja hisia za watanzania wengine kwamba huenda huyu anatumwa lakini si yeye kwa utashi wake. Na hili linaweza kumtia doa rais Magufuli.
Hivi sini rais Magufuli huyu huyu Kwenye mikutano yake ya kampeni alikuwa akisema katika serikali yake hatomvumilia mtu anayevurunda na kuvunja Sheria na kwamba hata muamishia eneo Moja au kumpeleka sehemu nyingine na wala hatosubiri mchakoto na kwamba mtu huyo aliyovurunda mchakato huo ataukuta kwao.
Sasa Dk.Ackson ambaye alikuwa mtumishi wa Mwandamizi wa serikali yake amevunja Sheria ya utumishi kwa kujiingiza wazi wazi Kwenye siasa Mbona hatujaona akifanya alichokisema Kwenye kampeni Matokeo yake Anadai ametengua uteuzi wake na saa hiyo hiyo anamteua Kuwa Mbunge?
Mbona Rais alipoenda kutembelea Hospitali ya Muhimbili hivi Karibuni alibaini uzembe wa kutisha ikiwa ni pamoja mashine hazifanyakazi ,sasa Mbona hatukuona akimtimua Kazi Yule Mkurugenzi badala yake aliagiza Mkurugenzi Huyo aamishiwe Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili apangiwe Kazi nyingine?
Aidha siku hiyo aliyoenda Hospitali ya Muhimbili ,taarifa ya Ikulu ilieleza pia alibaini eti Bodi ya wa kurugenzi ilikuwa imemaliza muda wake wa kisheria Miezi miwili iliyopita na kwamba eti akatangaza kuivunja ile Bodi ya wakurugenzi ya Muhimbili.
Sasa sijui ni Mwandishi wa Habari wa Rais ndiyo aliandika taarifa hiyo kimakosa Kuwa rais ameivunja Bodi ya Muhimbili na umma ukaamini hivyo? Ila najiuliza hivi inawezekana je rais avunje Bodi ambayo ilikuwa Tayari imeishamaliza muda wake kisheria?
Bodi ambayo bado haijamaliza muda wa Uhai wake kisheria ndiyo inaweza kuvunjwa . Sasa taarifa ya Ikulu Kusema rais alivunja Bodi ya Muhimbili ambayo Ikulu hiyo hiyo imesema Tayari Bodi ilikuwa imeishamaliza muda wake minaona siyo sahihi na mnafanya Rais Magufuli aonekane ni Kituko Mbele za watu .
Dk.Ackson licha ni msomi ameandika historia hii ambayo kwa kiasi fulani siyo nzuri kwa sasa kuwa ni Mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu serikali na msomi mwenye shahada tatu za sheria ambaye ameshika wadhifa huo kwa kipindi kifupi sana ukilinganisha na watangulizi wake .
Septemba 9 Mwaka huu aliteuliwa kushika wadhifa huo na Novemba 11 mwaka huu akiwa na wadhifa huo na huku akijua hapaswi kuwa mwanasiasa alienda kuchukua fomu za uspika hali iliyosababisha kuzuka kwa mjadala na Novemba 16 Rais katengua uteuzi wake, na yeye akajitoa kwenye kinyanganyiro cha uspika halafu saa chache baadaye akachukua fomu za kugombea nafasi ya unaibu spika.
Na kitendo cha Dk.Ackson Kujitoa Katika mbio za Spika dakika za mwisho kwa kiasi Fulani zinaweza kuhalalisha zile taarifa zisizo rasmi kuwa aliingia au kuingizwa Kugombea Uspika kwaajili ya kuwawekea kauzibe baadhi ya wagombea ambao walikuwa na ushawishi mkubwa kwa wabunge na wananchi wengi walitamani waingizwe hata tatu bora kama wanasiasa aina ya Samuel Sitta na wengine ambao majina Yao yalifyekwa na Kamati Kuu Katika hatua za awali na kurudisha jina la Dk.Ackson, Ndugai,Mwinyi ambapo hata hivyo dakika za Mwisho Dk.Ackson ,Mwinyi walitangaza Kujitoa.Kweli siasa siyo chafu ila wachezaji ndiyo wachafu.
Hivi kabisa Msomi mzima wa aina yake anaweza kuamua kujilipua kwenda kuchukua fomu za Uspika na Kamati Kuu ikapitisha jina lake Kisha dakika za mwisho anajitoa licha ni Haki yake halafu saa Chache huyu huyu Ackson ambaye tunamuuita msomi anaamua kwenda kuchukua fomu ya Kugombea unaibu Uspika? Kweli?
Anapaswa aseme ni kwanini aliamua kuanza kuchukua fomu ya Uspika vikao vikampitisha na dakika za mwisho Kujitoa halafu dakika za mwisho eti anaenda kuchukua fomu ya unaibu Uspika?
Dk.Ackson anapaswa aeleze umma ni lini alijiunga na CCM?Na Je Oktoba Mwaka huu alipokuwa akiendesha Kesi ya mita 200 Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam iliyofunguliwa na Kada wa Chadema, Kibatara Tayari alikuwa ni ni Mwana CCM au alikuwa bado?
Lakini pia CCM inatakiwa ieleze umma Dk.Ackson alijiunga na CCM lini?Na Je Kanuni na Katiba ya CCM inataja sifa zipi kwa mwanachama anayeruhusiwa kugombea uspika au madaraka yoyote katika CCM awe na ni mwanachama kwa muda gani?
Je mwanachama ambaye amejiunga leo hii na CCM anaruhusiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya CCM? Maana Dk.Nackson alichukua fomu ya Uspika Novemba 11 mwaka huu akagombea na Novemba 14 mwaka huu, Kamati Kuu ya CCM ikamteua yeye na wenzie watatu kugombea nafasi ya uspika.
Sawa tufanye basi wakati siku hiyo Dk.Ackson ambaye alikuwa bado rais Magufuli ajatengua uteuzi wake alikuwa basi alishajiudhuru wadhifa huo, Tuelezwe alijiudhuru lini?Na kama alijiudhuru Mbona taarifa ya serikali ya Jana imesema rais Magufuli ametengua uteuzi wa Dk.Ackson?Kitendo cha rais Kusema ametengua inamaana Dk.Ackson hakuwa amejihudhuru.
Maana aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alipo andika barua ya kujihudhuru ,Rais Jakaya Kikwete alitoa taarifa ya Kusema amekubali ombi la Jaji Werema la kujihudhuru wadhifa huo.
inamruhusu Mwanachama ambaye amechukua fomu ya Uspika Novemba 11 Mwaka huu, Kugombea
Hivi kwa watu tunaofikiri sawa sawa Dk.Ackson kwa kitendo Chake hicho kilichonyesha wazi Kuwa hakuwa amedhamiria Kugombea nafasi ya Uspika bali aligombea kwa ajenda mahususi ambayo amefanikiwa na anajiona ni Shujaa ila atambue Mashujaa wote wakishakufa vitani na anaamua Kugombea unaibu Spika.
Hivi hata CCM Mbona hamkomi na kujifunza?uchaguzi Mkuu uliomalizika Jasho limewatoka kwasababu baadhi ya wananchi waliichukia CCM kutokana na mambo kama haya haya ya kisanii Sani na Ujinga Ujinga .
Hivi huko CCM kote Hakuna watu wa Kugombea unaibu Spika, au kupitisha Majina matatu wagombea Uspika ambao angalau hawaandamwi na tuhuma mpya kama Dk.Ackson hadi mng'ang'ane na Dk.Ackson kama gundi?
Nafahamu Dola la CCM likiamua Dk.Ackson awe Naibu Spika wa Bunge kwa Vyovyote vile Atakuwa .
Itakumbukwa Kuwa Enzi Rais Jakaya Kikwete alipokuwa rais alikuwa akifanya kila jitihada za kumbeba kwa mbeleko Zakhia Meghji lakini umma ulipaza sauti kila alipokuwa ataka kufanya jaribio la Kumrudisha Kwenye uwaziri umma ulipaza sauti Kuwa awamtaki na hatimaye mwisho wa siku aliishia Kumteua Kwenye vyeo Vya CCM.
Pia Enzi za Kikwete tulishuhudia aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ,Eliachim Maswi,David Jairo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa Nyakati tofauti waliandamwa na tuhuma za Escrow na Jairo akituhumiwa kuhonga wabunge na kelele zilivyo zaidi Katibu Mkuu Kiongozi alisimamisha Kazi Jairo,Maswi ili kupisha uchunguzi na Muhongo alijiudhuru kupisha uchunguzi.
Katibu Kiongozi aliunda Kamati yake kuchunguza tuhuma hizo kwa watumishi hao wa umma na uchunguzi ulipokamilika ulitoa ripoti ambayo ilionyesha watendaji wote Hao hawana hatia na Maswi akarejeshwa Kazi na amateuliwa Kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Muhongo amegombea Ubunge ameshinda.
Novemba 14 Mwaka huu ndiyo nilianza kumjadili kupitia makala yangu iliyokuwa na kichwa cha ( DK.TULIA ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI).
Kwasababu yeye ni mwanasheria kutuhumiwa kujiingiza Kwenye siasa wakati ni mtumishi wa umma CCM na serikali yake hata kama itaziba Pamba masikioni Kuwa tutakuwa Naibu Spika ambaye kwanza baadhi ya wabunge watakuwa hawamuheshimu kwasababu Tayari alipokuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali alivunja Sheria za utumishi wa umma hivyo sidhani kama Atakuwa akiwataka wabunge wakorofi watii Sheria na Kanuni za Bunge watamtii ipasavyo zaidi zaidi ataambulia kurushiwa vijembe tena a jiandae na Hilo.
Ifike mahali tukubaliane Hilo ni doa analo Mgombea Naibu Spika wa CCM Dk.Ackson na litasumbua yeye binafsi , Bunge,CCM ,rais Magufuli ,sasa na mbele ya safari.
Dk.Ackson nataka utambue hata Kipindi kile Anne Makinda naye alikuwa na kundi la watu wazito nyuma walimsaidia Akawa Spika kwa kigezo eti ni zamu ya wanawake lakini Leo hii lile kundi la watu lilokuwa likimuunga mkono Makinda limempa Kisogo na yeye kwa kuwa ni mtu mzima na mwanasiasa Mkongwe alisoma alama za Nyakati Akaamua mapema kabisa ili kulinda heshima akatangaza kung'atuka siasa.
Sasa na wewe ambaye Katika vita hii ya Uspika ya Mwaka 2015 umeonekana Mwamba sana kwasababu una genge la watu lina kuunga mkono na ndiyo maana unatamba utakavyo unaharibu huku unateuliwa huku ,unaachia nafasi ya uspika dakika za mwisho unaenda kugombea nafasi ya unaibu ni haki yako ila nakuomba utambue jambo moja hao wanaokuwezesha uwe na nguvu hizo hipo siku watakuachia udondoke mwenyewe na hawatakuokota.
Usione ufahari leo hii kupata hivyo vyeo vya chapchap .Kuwa makini na watu hao sana na ujiulize ni kwanini wakupe Nguvu wewe ghafla ghafla katika CCM,serikali ilihali wewe ni kijana mdogo mdogo na Si mtu mwingine? Bahati nzuri wanasiasa Wengi siyo watu wakuaminika sana.
Sina chuki na Dk.Ackson ,nampenda, ana elimu nzuri,na siwezi kusema leo hii hafai kuwa Naibu Spika wakati bado hajashika wadhifa ila shida yangu ni moja tu ni hilo doa la kujihusisha kwenye siasa akiwa ni mtendaji wa umma litakutafuna.Minamtakia mafanikio katika kinyang'anyiro hicho ,Mungu amsaidie .Dk.Ackson akikisha ukipata nafasi hiyo unafanyakazi Kazi vizuri ili watu wanadhani huwezi wakose la Kusema.Naomba kutoa hoja.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
17/11/2015.
No comments:
Post a Comment