Header Ads

FM ACADEMIA "NGWASUMA" TUMEFIWA NA MARTIN KASIANJU






Na Happiness Katabazi

MKURUGENZI wa Bendi ya FM Academia ( Wazee wa Ngasuma) , Martin Kasianju   amefariki Dunia jioni hii Katika Hospitali ya Aghakhan Dar Es Salaam ,alipokuwa akipata matibabu.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi ,Mhasibu wa bendi Calvin Mkinga na Rais wa bendi hiyo Nyoshi El Sadat hivi Punde amethibitisha taarifa  za kifo cha Kasyanju  ambaye ni mmiliki wa bendi hiyo yenye umri wa Miaka 18 .

Mkinga alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa bendi hiyo na Kusema Kuwa Kasianju alitoa mchango mkubwa nchini wa kukuza muziki wa dansi nchini Kwakutoa ajira ya muziki kwa wanamuziki Wengi.

Aidha Nyoshi ambaye alikuwa akiongea kwa uzuni alisema ameshtusha na kifo hicho na kwamba anawaomba Watanzania na mashabiki wa bendi hiyo Waungane pamoja Katika Kipindi hiki kigumu na akawaomba radhi wapenzi wa bendi hiyo ambao Leo walikuwa wamefika Katika Viwanja Vya Msasani kwaajili ya kupata burudani ya bendi hiyo iliyokuwa ukitarajiwa kutolewa jioni ya Leo Kuwa onyesho Hilo limevunjwa kwasababu ya kifo hicho ambacho kimetukuka hivi Punde na kwamba msiba utakuwepo Oysterbay Mtaa wa Mahenge nyumbani kwa marehemu na Kuwa taarifa zaidi ya Ratiba wa msiba huo zitatolewa.

Mimi Happiness Katabazi ni shabiki namba Moja wa Bendi hii  na pia ni mkuu wa group la Whtasup la Familia ya Fm Academia , nimesikitishwa na kifo hiki.Kazi ya Mungu haina makosa.

Mungu aiweke roho ya marehemu Kasyanju mahali panapostahili.

Facebook: Happy Katabazi
1/11/2015.






No comments:

Powered by Blogger.