Header Ads

KORTI YAMRUHUSU MRAMBA,YONA KWENDA INDIA KUTIBIWA


Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, imemtuhusu waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Daniel Yona, WANAOKABILIWA na Kesi ya matumizi Mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali Hasara ya sh Bilioni 11.7, kwenda nchini India kutibiwa.

Ruhusa hiyo ilitolewa Jana na Jaji John Utamwa, MUDa mfupi baada ya Wakili wa serikali Shadrack Kimaro kuiambia Mahakama hiyo upande wa jamhuri Hakuna pingamizi na ombi Hilo liliwasilishwa na Wakili wa washitakiwa Juzi Peter Swai liloomba Mahakama iwapatie Ruhusu wateja wake warned nje ya nchi kutibiwa.

JAJI  Utamwa Alisema licha Amearuhusu washitakiwa waende kutibiwa India, pia Amekataa washitakiwa watakapo rejea nchini waakikishe wanatetewa hati zao za kusafiria mahakamani hapo na akaairisha Kesi hiyo hadi Aprili 21 hadi 25 kwaajili ya kuendelea kusikilizwa.

Wakati huo huo, Kesi ya Mauji nayomkabili Mfanyabashara Maarufu Papa MSOFFE imearishwa tena mahakamani hapo baada ya Wakili wa serikali Leonard  Chalo Kudai Kuwa jarada la Kesi hiyo bado lipo kwa MKURUGENZI wa Mashitaka na Hakimu Hellen Liwa akaiairisha hadi Machi 25 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutaka.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 12 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.