Header Ads

WASHITAKIWA 'KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI' WASHINDA RUFAA





WASHITAKIWA 'KESI YA SAMAKI  WA MAGUFULI 'WASHINDA RUFAA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Rufaa Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na faini ya jumla ya sh.bilioni 22 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Februali 23 Mwaka 2012 dhidi ya Raia wa Taiwan na China , Nahodha wa meli Hsu Chin Tai na  wakala wa meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing baada ya kubaini Sheria zilikiukwa wakati wa uendeshwaji wa Kesi hiyo Katika Mahakama za chini.

Hukumu hiyo ilitolewa Jana na jopo la Majaji wa Tatu Salum Masati, Semistocles Kaijage ambao walisema dosari ya kwanza ambayo Mahakama ya Rufaa imebaini ni kwamba Kesi hiyo il ifunguliwa Katika Mahakama ya bila ya kuwepo Kibali Cha Mkurugenzi Mashitaka (DPP).

Hukumu hiyo inafuatiwana Rufaa iliyokatwa na waomba RUFAA Hao kupitia  Mawakili wao Ibrahim Bendera na John Mapinduzi  hawa kurudishwa na hukumu ya Mahakama Kuu na hivyo Februali Mwaka 2012 walikutwa RUFAA Mahakama ya RUfaa ambapo Jana Mahakama hiyo ya rufaa imekubaliana na hoja za rufaa za raia hao wa kigeni kuwa hukumu ya mahakama kuu iliyowahukumu kifungo cha jumla ya miaka 30 gerezani ilikuwA na makosa kisheria.

Hata  hivyo Mahakama Rufaa  umempatia Ruhusa ya kuwafungulia Kesi upya warufaniwa Hao na wale waliochiliwa na Mahakama Kuu, Kama ataona Ana  ya kufanya hivyo.

Kwa upande  wake Wakili wa waomba Rufaa hao , John Mapinduzi Alisema wamefurahishwa na hukumu hiyo na kwamba HIvi sasa wa najiandaa kupunguza Kesi ya Madai dhidi ya serikali wakuombwa walipwe Melissa Yao ya Tawaliq 1 ambayo imenyofolewa vifaa Vingi na sat wasiyojulikana, na pia serikali iwalipe Fedha ambazo zinathamani ya Samaki Waliokuwa wamekamatwa na serikali Katika Meli hiyo ambayo washitakiwa walk,KWA wakiiendesha.

Hata hivyo mwandishi wa Gazeti Hili aliwashuhudia raia Hao wa KIGENI saa tano Sita mchana Jana wakirejeshwa gerezani kwaajili ya Taratibu zaidi za JESHI la Magereza ili waweze kuachiliwa  Huru na mwandishi wa Habari hizi alipata fursa ya kuzungumzia na maofisa madhara wa Balozi wanazozitoa

FEbruali 23 mwaka 2012 , Jaji Agustine Mwarija alisema   washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu:Kosa la kwanza ni la kuvua samaki bila leseni kinyume na kifungu cha 18(1) cha Sheria Uvuvi katika kina kirefu cha bahari.Kosa la pili ni kuchafua bahari na kuathiri viumbe vilivyomo ndani ya bahari kinyume na kifungu cha 67 cha Sheria hiyo na kosa la tatu ni kusaidia kutenda kosa.

Jaji Mwarija alisema kwa mujibu wa maelezo ya onyo yaliyotolewa na Hsu Chin Tai (Nahodha) na Zhao Hanguin ambaye ni wakala wa meli hiyo nahodha wa meli hiyo alikiri kuwa ni kweli meli hiyo ilikuwa ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda huo na kwamba ni kweli meli hiyo ilivyokamatwa Machi 8 mwaka 2009 na boti ya askari wa doria wa nchi za Tanzania,Afrika Kusini,Botswana na leseni yake ilikuwa ikimaliza muda wake Desemba mosi mwaka 2008 na kwa upande wake wakala huyo wa meli alikiri kuwa kampuni yake ndiyo iliyoshughulika meli hiyo kutoka Bandari ya Mombasa kuja Tanzania.

. Nahodha na wakala nimewatia hatiani katika kosa la kwanza la kufanya uvuvi bila leseni ambapo kila mmoja atalipa faini ya Shilingi Bilioni moja au kwenda jela miaka 20 kila mmoja:

“Katika kosa la pili nimetia hatiani mshtakiwa mmoja tu ambaye ni Nahodha wa meli ambapo atapaswa alipe faini ya Shilingi bilioni 20 au kwenda jela miaka 10, na katika kosa la tatu mahakama hii inawaachiria huru washtakiwa wote kwasababu jamhuri imeshindwa kuthibitisha kosa hilo la kusaidia kutendeka kwa kosa hilo na kwamba adhabu zote hizo zinakwenda pamoja”alisema Jaji Mwarija.

Jaji Mwarija alisema kuhusu ombi la Wakili Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga liloomba meli ya Tawariq 1 ambayo ilikuwa ni kielelezo cha kwanza, itaifishwe, mahakama hiyo imekubali ombi hilo kwa sababu kifungu cha 18(1) cha Sheria ya Uvuvi katika kina kirefu cha bahari ,kinaeleza mahakama ina mamlaka ya kutaifisha chombo kilichotumika kutendea kosa na kwamba katika kesi hiyo meli hiyo ilitumika kufanya uvuvi haramu.

“Nimeangalia mazingira ya kesi hii, meli hiyo imekuwa na maji mengi tofauti na hali hiyo imenifanya niamini meli hiyo ilikuwa ikifanya uhalifu huo katika eneo la Tanzania kwa mbinu za aina yake na meli hiyo imeonyesha ilikuwa haitambuliwi na mamlaka husika: 

“….Na hili kukomesha uhalifu wa aina hii mahakama hii itatoa amri ya kuitafisha meli hiyo kuanzia sasa ili iwe fundisho kwa meli nyingine zinazokuja kufanya uhalifu katika Ukanda wa Tanzania na pia sitatoa amri yoyote kuhusu wale samaki waliokamatwa kwenye meli hiyo na kisha wakagaiwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali na washtakiwa kama hawajalidhika wana haki ya kukata rufaa ”alisema Jaji Mwarija.

Kwa upande wake wakili wa utetezi John Mapinduzi alisema anakusudia kukata rufaa katika mahakama ya rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hawajaridhishwa na hukumu hiyo.

Novemba 21 mwaka 2011, washtakiwa hao walimaliza kujitetea , ikiwa siku chache baada ya mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hao watano wanakesi ya kujibu na kuwaachilia huru washtakiwa 31 kwasababu mahakama iliona hawana kesi ya kujibu.Kesi hiyo imekuwa ikiwahusisha wakalimani wa ligha zaidi ya nne tangu ilipofunguliwa katika mahakama hiyo ya chini hadi mahakama Kuu. 

Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusaidia kutendeka kwa kosa hilo.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi ,Machi 29 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.