MKENYA KORTINI KWA KUIHUJUMU TCRA
Mkenya kizimbani kwa kuiujumu TCRA
Na Happiness Katabazi
RAIA wa Kenya, Nelson Rading Onyango Jana amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na na saba likiwamo kosa la kutoa huduma ya mawasiliano ya Kimataifa bila ya kuwa na leseni na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano nchini (tcra), zaidi ya Sh.ya zaidi ya Sh.bilioni 6.8 .
Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Devotha Kisoka alidai kuwa kati ya Julai 2010 na Novemba 2013 katika eneo la Kariakoo mshtakiwa huyo kwa nia ovu alifanya udanganyifu katika matumizi ya kimtandao kinyume cha sheria.
Wakili Kweka alidai kuwa Onyango kwa nia ovu na udanganyifu alikuwa akifanyisha huduma za mawasiliano ya Kimataifa huku akikwepa kutumia njia halali za maalipo ambazo zinatolewa na ( TCRA.
Shitaka la pili, Wakili Kweka alidai Kuwa mshitakiwa Huyo anadaiwa kutoa huduma ya mawasiliano bila ya kuwa na leseni inayomruhusu kufanya hivyo.
Kweka alidai kuwa katika kipindi hicho, mshtakiwa huyo bila ya kuwa na uhalali kisheria alitoa huduma ya simu za Kimataifa bila ya kuwa na leseni inayotolewa na TCRA.
Mshtakiwa huyo katika Shtaka la tatu anadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Novemba 2013 akiwa katika eneo hilo la Kariakoo alitumia kadi za simu ambazo hazijasajiliwa kama inavyotakiwa kisheria zenye namba 0778350683,0778498179,0774395401,0774552099,0774552122,0774552138 na 0777225.
Alizitaja namba nyingine kuwa ni 07748802243,0774802250,0774802255,0774802265,07748022278,0777848892,0779579620,0779579848,0779663386,0779716796,0779716800,0779716804,0779716811,0779716812,0779716822 na 077971.
Shtaka la nne, mshtakiwa huyo anadaiwa kuingiza nchi ni vifaa vya kielectroniki bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya hivyo.
Akiendelea kusoma mashtaka yanayomkabili Onyango , Wakili Kweka alidai kuwa siku isiyofahamika aliingiza mitambo ya mawasiliano ambayo ni SIM Boxi bila ya kuwa na kibali.
Wakili Kweka, shtaka la tano alidai kuwa licha ya kuingiza nchini mitambo hiyo bila ya kuwa na kibali mshtakiwa huyo, alisimika mitambo mine ya mawasiliano na kuiendesha ambayo ni SM Boxi zenye namba za siri TX 2SN5600C5/05, TX2SN48002/K21, TX2SN102335A na wa Cisco Router iliyotengenezwa Cisco AS5300 mfululizo yenye namba ya siri ASN 050-332-940 na AP12KGCAA.
Katika shtaka la sita, wakili huyo wa Serikali Mwandamizi alidai kuwa Onyango alitumia mitambo hiyo ya Kielectroniki ambayo ilikuwa haijathibitishwa na TCRA.
Aliongeza kudai kuwa Novemba 22, 2013 Kariakoo , akiwa na ufahamu kuwa mitambo hiyo haijathibitishwa na TCRA aliitumia.
Shtaka la saba, mshtakiwa huyo anadaiwa kusababisha hasara kwa mamlaka husika ya TCRA kati ya Julai 2010 na Novemba 2013 kwa kufanya huduma hizo za mawasiliano ya Kimataifa bila ya kuwa na leseni .
Ilidaiwa kuwa kati ya Julai 2010 na Novemba 2013 mshtakiwa huyo alichepusha mawasiliano ya simu za Kimataifa kwa kutumia namba hizo ambazo hazijasajiliwa na TCRA na kwamba kutokana na kitendo hicho aliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 6,842,880,000.00.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa aliyakana yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Devotha Kisoka alimwambia mshtakiwa huyo kuwa kulingana na makosa hayo yanayomkabili dhamana ipo wazi hivyo alimtaka kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh 3.4 bilioni na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika.
Akiendelea kutoa masharti hayo ya dhamana, hakimu Kisoka alisema mdhamini mmoja kati ya wadhamini hao wawili awe ni mtumishi wa serikali na mwingine atakayekubalika na mahakama na kwamba wadhamini wote hao watasaini bondi ya Sh milioni 50.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 27 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment