UPELELEZI KESI YA MADABIDA WAKAMILIKA
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa jamhuri Katika Kesi ya kusambaza dawa za kupunguza MAKALI ya ugonjwa wa ARVs inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.
Wakili wa serikali Jacline Nyantori adai Mbele yaHakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba,
Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na wa naomba wapangiwe tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.
Hakimu Nyigulila aliarisha kesi hiyo hadi Aprili 23 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.
Mbali na Madabida washitakiwa wengine ni Seif Salum Shamte ,Simon Msoffe, Fatma Shango ,Sadiki Materu na Evance Mwemezi na kwamba hati ya mashitaka ina jumla ya mashitaka matano.
Februali 10 Mwaka huu, washitakiwa Hao walifikishwa wa Mara ya kwanza Mahakamani hapo wakikabiliwa makosa matano yakiwemo makosa ya la kusambaza dawa za ARVs zilizokwisha muda wa matumizi kinyume na kifungu cha 76(1) cha Sheria ya Taifa ya Vyakula, Madawa na Vipodozi ya mwaka 2003 na kuisababishia Bohari yaMadawa Hasara ya sh 148,350,156.48
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 19 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment