Header Ads

MASKINI SHEIKH PONDA



Na Happiness Katabazi
JITIHADA za Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu,, Sheikh Ponda Issa Ponda za kuiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaaam, ikubali ombi lake lililokuwa Linaomba Mahakama hiyo Ifanyie mapitio uamuzi wa awali wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro , umegonga Mwamba baada ya Mahakama, hiyo kutupilia Mbali ombi lake.

KORTI Kuu yamliza sheikh Ponda
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia  Mbali ombi la kuomba Mahakama hiyo Ifanyie Marejeo uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Oktoba Mosi Mwaka Jana, ambalo liliwasilishwa Mbele yake na Sheikh Ponda Issa Ponda.
Uamuzi huo ilitolewa Jana asubuhi na Jaji Agustino Mwarija ambaye alisema Mahakama yake imesikiliza hoja za pande zote mbili  na Imefikia uamuzi wa kukubaliana na pingamizi la awali liliwasilishwa mahakamani na mjibu  Maombi ambaye ni MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk.Elizer Feleshi,   Februali Mwaka huu mahakamani hapo AMBAlo liliomba ombi la Ponda litupwe kwasababu linakiuka matakwa ya Kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ambacho kinakataza amri za MUDa ,awali zinazotokana na Mahakama za chini zisikatiwe RUFAA katika Mahakama za juu Kama Ponda aliyofanya kukata rufaa amri hiyo ya MUDa ambayo uamuzi wa Oktoba Mosi Mwaka Jana haumalizi Kesi ya Msingi inayomkabili Ponda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Jaji Mwarija Alisema anashangazwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassor kushindwa kuelewa kuwa Kifungu hicho cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , kinakataza amri za MUDa, awali ambazo hazimalizi Kesi za Msingi na ambazo zinatolewa na Mahakama za chini, hazitakiwi Kupatiwa rufaa Mahakama za juu.

Jaji Mwarija Alisema ombi Hilo la Ponda Na.14/2013 liloletwa Mbele yake lilitokana  na amri  ya awali iliyotolewa na Mahakama ya Ya Hakimu Mkazi Morogoro ,Oktoba Mosi Mwaka Jana, AMBAPO Mahakama hiyo Iliikataa hoja ya Wakili wa Ponda , Nassor iliyokuwa ikidai Mahakama ya morogoro haina mamlaka ya  kusikiliza kosa la kwanza Katika Kesi ya Msingi Na. 128/2013  AMBAPO kosa la kwanza linalomkabili Ponda ni kutotii amri  halali ya JESHI la POLISI  kinyume na Kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , na kwamba alitenda kosa Hilo  AGOSTI  10 Mwaka Jana, Katika eneo la Kiwanja cha Ndege Wilayani Morogoro Kitendo ambacho ni kukiuka amri ya Hukumu ya Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotolewa Mei 9 mwaka jana, ambayo ilimtaka asitende makosa na awe mtunza amani.

Kwamba  uamuzi huo wa Oktoba Mosi Mwaka Jana iliusiana na kosa Hilo Moja tu licha Anakabiliwa na jumla ya makosa matatu na makosa hayo matatu hayahusiaji na Maombi hayo yaliyotolewa uamuzi Jana.

" KWA Kuwa Ponda Anakabiliwa na Mashitaka matatu Katika Kesi ya awali kule Morogoro na uamuzi wa wa Oktoba Mosi Mwaka Jana, sio uamuzi wa kumaliza Kesi ile ya jinai ni uamuzi wa MUDa tu,....Mahakama hii inakubaliana na pingamizi la awali la Wakili wa serikali Kongola Kuwa ombi Hilo la Ponda limevunja matakwa ya Kifungu hicho na kwasababu hiyo inalitupilia Mbali ombi Hilo la Ponda lililokuwa Linaomba Mahakama yangu Ifanyie Marejeo uamuzi wa awali wa Mahakama ya awali ya Morogoro" Alisema Jaji MwAarija.

Nje ya Mahakama wafuasi  wake na ndugu zake walikuwa wakisikika wakisema huku wakimpungia mkono " Takibiri' na Kisha kuondolewa eneo la Mahakama Chini ya Ulinzi Mkali wa jeshi la Polisi na Magereza. 

Ilipofika saa Sita mchana Wakili wa Ponda, Nassor aliwasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya kusimamisha usikilizwaji wa Kesi Na.124/2013 inayomkabili Ponda mjini  Morogoro hadi Rufaa Na.89/2013 iliyokuwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam , Kapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyotolewa MEI 9 Mwaka Jana, Ambayo ilimfungankifungo cha Nje Ponda itakaposikilizwa na kuamriwa.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 19 Mwaka 2014












No comments:

Powered by Blogger.