MMILIKI JENGO LILILOANGUKA DAR ABADILISHIWA SHITAKA
MMILIKI JENGO LILILOANGUKA DAR ABADILISHIWA SHITAKA
Na Happiness Katabazi
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi Amemfutia Kesi ya KUUA bila kukusudia mmiliki wa jengo liloanguka Katika MTaawa INdra gandi mwenye asili ya kiasia, Raza Hussein Raza na Wenzie 11 akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na kisha kuwafungulia Kesi mpya ya Mauaji ya watu 27.
Wakili Kiongozi wa Serikali Bernad Kongora akisaidiwa na Joseph Mahugo,Inspekta Jackson Chidunda,Peter Njike, Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoki , alianza KWA Kudai Kuwa awali washitakiwa 11 walikuwa wakikabiliwa na Kesi KUUA bila kukusudia ambayo il ifunguliwa Mwaka Jana mahakamani hapo na walikuwa nje KWA DHAMANA, isipokuwa Fuime ambaye alifunguliwa Kesi ya Mauaji hivi karibuni mahakamani na Kuwa akiishi gerezani.
Wakili Kongora alidai Kuwa upande wa jamhuri unaomba kutumia Kifungu cha 234(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , kubadilisha hati ya Mashitaka ya Kesi Kuua bila kukusudia kwasababu wanamuunganisha mshitakiwa mpya (Fuime) Katika Kesi mpya ya Mauji ya kukusudia ya watu 27 kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, ombi AMBAlo lilikubaliwa na Hakimu Huyo.
Akisoma hati hiyo , Kongola aliyetaja Majina ya washitakiwa Kuwa ni RAZA ambaye ni mmiliki wa Jengo lililoanguka Mtaa wa Indra Gandi na KUUA watu 27, Goodluck Silvester,Wilbroad Mugya, Ibrahim Mohamed ,Charles Salum Ogare ,Zonazea Anange,Oushao Udada,Vedasto Frednand Ruhele,Michael Leth,Albert Mnuo ,Joseph Ringo na Gabriel Fuime wanaotetewa na Wakili John Mhozya.
Kongora alidai makosa hayo 27 ya Mauaji ya watu 27 waliyatenda Machi 29 Mwaka 2013 Katika Mtaa wa INDRAGANDI na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.
KWA upande Wake Hakimu Kisoki ambaye ndiye hakimu ALIYEKUWA akiisikili za Kesi ya awali ya KUUA bila kukusudia iliyokuwa ikiwakabili washitakiwa Hao, ambayo Jana ilifutwa na kufunguliwa Kesi mpya ya Mauji ambayo pia amepangwa kusikiliza yeye.
Hakimu Huyo Alisema KWAKUWA upande wa jamhuri umebadilisha hati ya Mashitaka na kuwafungulia washitakiwa Kesi mpya ya Mauji ha watu 27 , kesi ya zamani ya KUUA bila kukusudia na dhamana zinakuwa zimetutwa na hivyo HIvi sasa washitakiwa watakuwa wanaokabiliwa na Kesi mmoja ya Mauji ambayo haina dhamana na Mahakama hii hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza Kwani ni Mahakama Kuu ndiyo Ina mamlaka ya kuisikiliza , hivyo akaamuru washitakiwa wapelekwe Rumande hadi Machi 26 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Baada ya Hakimu Kisoki Kutoa Amri hiyo ndugu na Jamaa wa washitakiwa Hao akisemo Mtawa (sister ) wa Kanisa Katoriki, aalijikuta wakiingia Bilioni Katika Viwanja Vya Mahakama hiyo wakiwa hawaamini Kama ndugu zao HIvi sasa washitakiwa kwa Kesi ya Mauji ambayo haina dhamana na kwamba HIvi sasa watakuwa wakiishi gerezani.
hata hivyo washitakiwa Hao ambao walikuwa wakilindwa chini ya Ulinzi MKALI wa kaka hero wa JESHI la POLISI, mshitakiwa wa kwanza Raza ambae ana asili ya Kiasia Kabla ya Hakimu kuingia mahakamani mwandishi wa Habari hizi alimshuhudua Akiwa amesimama wakati washitakiwa wenzie wamekaa Kwenye mabenchi wakisubiri Hakimu aingie akiwa ameshika (tasibiri) mkononi anaibesabu na mara Hakimu Alipoingia walk panda kizimbani na wakati wakisomewa Mashitaka alikuwa amesimama akiende lea kuiesababu na Muda mchache aalijikuta alishindwa kuendelea kusimama na akaomba ape we Kiri akae ambao ambapo alikaa Kwenye Kiti kilichoketi nyuma ya washitakiwa.
Machi Mwaka Mwaka Jana washitakiwa Hao 11 ,walifikishwa mahakamani hapo KWA Kesi na KUUA bila kukusudia na Hakimu Huyo aliwapatia DHAMANA, lakini Jana DPP aliwafutia Kesi hiyo na kuwafungulia Kesi mpya ya Mauji ambayo kisheria haina dhamana.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 13 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment