Header Ads

KESI YA MRAMBA BADO HAKIELEWEKI

Na Happiness Katabazi


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imesema kuwa mwendo wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na wenzake bado haujakamilika.


Jaji John Utamwa anayesaidiwa na Hakimu Mkazi Sam Rumanyika na Saul Kinemela alisema kesi hiyo ilikuja jana kwaajili ya kutajwa na kuangalia kama mwenendo wa kesi hiyo umekamilika lakini amebaini mwenendo wa kesi hiyo ambao ulishachapwa una makosa.
Jaji Utamwa alisema kwa sababu hiyo anaagiza mwenendo huo ukafanyiwe marekebisho na wahusika na endapo utakamalika basi mahakama hiyo itazipatia pande hizo mbili na akaiarisha kesi hiyo hadi Januari 13 mwakani ambapo kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa.
Mbali na Mramba washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegema Peter Swai, Hurbet Nyange na Elisa Msuya.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima, Desemba 15 mwaka 2011.

No comments:

Powered by Blogger.