10 KIZIMBANI KWA KUMUUA DK.SENGONDO MVUNGI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE watu Kumi wanaodaiwa kumuua Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Sengondo Mvungi Jana walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam, wakikabiliwa na kosa Moja tu la kumuua Dk.Mvungi kwa kukusudia.
Wakili wa serikali Aida Lusumo Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni chibago Magoze (32),John Kanjunju(29),John Mayunja,Longishu Losingo(29),''Masunga Makunza,Paulo Dondondo(30),mkanda Mlewa(40),zakaria msese(33),msungwa Matonya(30) na Ahmed kilebu(30).
Wakili Lusumo alidai wanashitakiwa kwa kosa la Kua kwa kukusudia kinyume na kifungo Cha 196 Cha Sheria ya kanuni a adhabu ya Mwaka 2002 , Kuwa Novemba 11 Mwaka 2013 huko eneo la msakuzi kino done Dar es salaam, wote kwa pamoja walimuua Dk.Mvungi ambaye alikuwa ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es salaam na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Fimbo aliwataka washitakiwa Hao wasiyonaidai chochote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo hivyo akaamuru washitakiwa wapelekwe gerezani.
Washitakiwa walifikishwa chini ya Ulinzi MKALI wa wanausalama AMBAPO walipandishwa Kwenye Gari aina ya Landcruser yenye namba za usajili Kx 06EFD na walisikikiza na Gari aina ya NOah yenye namba za usajili T 539 CCB AMBAlo LILikikuwa likiongoza msafara huo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi ,Novemba 23 Mwaka 2013
No comments:
Post a Comment