Header Ads

PAPA MSOFE AWEKWA KIPORO

Na Happiness Katabazi UPANDE wa jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabashara maarufu jijini Dar es Salaam, Abubakar Marijan [50] ‘Papaa Msoffe chuma cha Reli akishiki Kutu, mutu ya Pakee’ na Makongoro Joseph Nyerere, Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umedai Kuwa jarada la Kesi hiyo Tayari limeshatoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ,Dk.Eliezer Feleshi Lipo kwa Mkurugenzi wa wa makosa ya jinai. Mwendesha Mashitaka Inspekta wa polisi ,hamisi said aliikumbusha Mahakama Kuwa Kuwa Jana Kesi hiyo ilikuwa kwaajili ya kutajwa na kuangalia maendeleo ya Kesi hiyo. Inspekta hamis alieleza kuwa jarada la Kesi hiyo ambayo lilienda kwa DPP ,na DPP aligundua Lina mapungufu akamwelekeza DCI alifanyie marekebisho na kwamba Tayari DCI ameishalifanyia Kazi na kwamba MUDa wowote litarejeshwa mahakamani hapo kwaajili ya Hatua zaidi. Kwa upande wake Hakimu Hellen liwa aliarisha Kesi hiyo hadi Novemba 27 Mwaka juu, itakokuja kwaajili ya kutajwa na kuamuru washitakiwa wapelekwe gerezani. Novemba 31 Mwaka huu, wa serikali Charles Anindo aliambia aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mahakama kutoa uamuzi wake wa ama kuwafutia kesi washitakiwa au la , ila upande wa jamhuri umepelekea jarada la kesi hiyo kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kwaajili ya Mwanasheria wa Serikali kutoa maamuzi ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo hivyo akaomba kesi hiyo iarishwe. Ombi hilo lilisababisha Hakimu Mkazi Hellen Liwa kusema mahakama yake jana ilikuwa ipo tayari kwaajili ya kutoa uamuzi wake lakini kwakuwa upande wa jamhuri umewasilisha ombi hilo ambalo limeonyesha ni dalili nzuri za maendeleo ya kesi hiyo kwani kila mara kesi hiyo inapotajwa upande wa jamhuri umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika, hivyo anaiarisha kesi hiyo hadi Novemba 14 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa kwani siku hiyo inawezekana yakapatikana maendeleo mazuri ya kesi hiyo kutoka kwa upande wa jamhuri. Septemba 12 mwaka huu, wakili Kweka aliwasilisha pingamizi lililokuwa linaomba mahakama hiyo ilikatae ombi la wakili wa washitakiwa Malima lilokuwa likiomba mahakama hiyo iwafutie kesi hiyo kwani ni kesi ya muda mrefu na hadi sasa upelelezi bado haujakamilika na ombi hilo liliwasilishwa na wakili wa washitakiwa Daudi Malima. Wakili Kweka alidai kuwa kwanza mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauji ndiyo maana washitakiwa waliposomewa shitaka lao hawakutakiwa kujibu chochote na kwamba ni Mahakama Kuu peke ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauji na kwamba kesi hiyo inayomkabili Msoffe bado hipo katika hatua za awali kabisa na kwamba hata upelelezi bado haujakamilika. Februali 13 mwaka 2013, wakili wa serikali Charles Anindo aliiomba mahakama kuumunganisha Nyerere katika kesi hiyo ambayo awali ilikuwa ikimkabili Msoffe peke yake ambaye alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 10 mwaka 2012 ambapo aliwasomea shitaka ambapo aidai kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kumua kwa makusudi Onesphory Kituli, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyorekebishwa mwaka 2002 na kwamba kosa hilo walilitenda Oktoba 11 mwaka 2011, nyumbani kwa marehemu huko Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Katika Hatua nyingine Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo ,Aloyce Katemana alitupia Mbali Mbali ombi la vigogo wa SUMA JKT wanaokabiliwa na kesi ya matumizi mabaya aya madaraka lilotaka Mahakama hiyo ikatae kupokea maelezo ya onyo waliyochukuliwa wakati wakihojiwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Kabla hawajafunguliwa Kesi mahakamani hapo kwa maelezo Kuwa PCCB hawakufunja Sheria wakati wakiwavhukia maelezo ya onyo na akaairisha Kesi hiyo hadi Desemba 12 Mwaka huu, AMBAPO mashahidi wa upande wa jamhuri wataendelea kutoa ushahidi wao. Chanzo :Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 15 Mwaka 2013

No comments:

Powered by Blogger.