Header Ads

BABU SEYA KUACHILIWA HURU LEO?

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Rufani nchini Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa uamuzi wake wa ama kulikubali au kulikataa ombi la marejeo liliowasilishwa mahakamani hapo na MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Papi Kocha Mtoto wa Mfalme,ambapo waliomba mahakama hiyo ifanyie marejeo hukumu yake iliyoitoa Februali 2010 ambayo iliyowahukumu kifungo cha maisha warufani hao kwasababu ina dosari za kisheria. Kwa mujibu wa hati ya wito wa kuitwa mahakamani iliyotolewa kwa mawakili wa pande zote mbili, mahakama imemtaka Nguza Vicking na Papii kocha na mawakili wa pande zote kufika leo mahakamani hapo bila kukosa ili waje wapokee uamuzi wa maombi hayo. Oktoba 30 mwaka huu, jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliokuwa wakiongozwa na jaji Nataria Kimaro, salum Massati ma Mbarouk Mbarouk walisikiliza ombi hilo la Kuomba mahakama hiyo ifanye majeo ya hukumu yake Februali 2010 .Ombi hilo la marejeo Na.5/2010 Ambapo waombaji wanatetewa na Wakili wa kutegemea Mabere Marando. Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake. Wakili Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 , ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi, litaja moja ya utelezi wa wazi wazi wa kisheria uliofanywa na mahakama hiyo, ni kwamba katika hukumu hiyo kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosoea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto waliokuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo na kwamba mahakama ya rufaa ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono ndiyo walioutumia kuwatia hatiani waomba rufaa kwa adhabu ya kifungo cha maisha “waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii; “Nafahamu ni kazi ngumu sana kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu’ alidai Marando. Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo,Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010. Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari. “Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”alidai wakili Jackson. Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Addy Lyamuya, aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo liliwatia hatiani waombaji na kuwafunga kifungo Cha Maisha lakini jopo hilo la majaji wa tatu linaloundwa na Jaji Kimaro ,Massati na Mbarouk liliwatia hatiani Nguza Vicking na Papii kocha na kuwaachiria huru wanae wawili kwa makosa ya kuwabaka watoto wadogo na likawahukumu kifungo cha maisha gerezani. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 21 Mwaka 2013

No comments:

Powered by Blogger.