Header Ads

DK.SENGONDO MVUNGI AFARIKI DUNIANI



Na Happiness Katabazi
MWASISI wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), Dk.Adrian Sengondo Mvungi amefariki dunia jana katika Hospitali ya nchini Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwaajili ya matibabu zaidi.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, mtoto mkubwa wa marehemu ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria wa (UB), Dk.Natujwa Mvungi alisema alifarki saa 9:30 Alasiri  katika hospitali hiyo ambako aliamishiwa Novemba 8 mwaka huu, akitkea katika wodi ya wagonjwa mahututi ya Taasisi ya Mifupa Moi  Dar es Salaam ambako alilazwa tangu Novemba 3 mwaka huu na kwamba msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Kibamba.

Itakumbukwa kuwa usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu,watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivamia nyumbani kwa Dk.Mvungi huko Kibamba Kata ya Mpiji Magohe ambaye kabla kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo  na kumjeruhi vibaya kwa mapanga usoni na kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Tumbi usiku huo wa saa saba na kisha kuamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dk.Mvungi ameacha mke aitwaye Anna na watoto wa tano.Alizaliwa Novemba Mosi mwaka 1952.Mwaka 1994 alitunukiwa Shahda yake ya Udaktari katika fani ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Hambury ,Ujerumani.Mwaka 1987 aliipata shahada ya sheria  ya pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 1981 alipata shahada yake ya kwanza  UDSM.

DK.Mvungi hadi umauti unamkuta alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Kituo ya Kutetea Haki za Binadamu(LHRC), mwaka 1995-2008 alikuwa ndiye mtetezi na mtafiti mkuu  wa Sheria na Haki za Binadamu  katika mradi  wa kituo cha kutetea haki za wafugaji .Aliwai kuwa wakili toka LHRC katika kesi ya Kikatiba ya kutetea wananchi wa kijiji cha Nyamuma.Mwaka 2000/2003 alikuwa Mkaguzi wa kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na mwaka 2003 alishika wadhika na kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria UDSM.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 13 Mwaka 2013

No comments:

Powered by Blogger.