Header Ads

HAPPINESS KATABAZI NA DK.MVUNGI KATIKA PICHA ENZI ZA UHAI WAKE

Happiness Katabazi na marehemu Dk.Sengondo Mvungi, katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Oktoba 29 mwaka 2013.
PIcha zote hizi zilipigwa na mdogo wangu Michael Machali Oktoba 29 mwaka huu, saa moja asubuhi katika ofisini kwa marehemu Dk.Sengondo Mvungi ambapo mimi na mdogo wangu alitutaka tufike ofisini kwake muda huo kwaajili ya maongezi binafsi na Dk.Mvungi alinipatia vitabu mbalimbali vya kisheria ambavyo alisema vitanisaidia katika kozi yangu ya sheria. Kumbe ndiyo ilikuwa ni siku ya mwisho ya mimi kuonana na kuzungumza na Dk.Mvungi hapa duniani kwani usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu, ndipo alijeruhiwa na Novemba 12 mwaka huu, ndiyo karafiki hospitalini huko nchini Afrika Kusini.Nimeumizwa sana na kifo hiki cha mzee wangu na mwalimu wangu.Happiness Katabazi 'First Lady' na marehemu Dk.Mvungi siku ya uzinduzi wa kozi ya kuwanoa watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Afrika Mashariki(AKIBA UHAKI),.Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo eneo la Kawe Beach ,mimi na Dk.Mvungi ambaye ni mwasisi wa chuo hicho tuliudhulia Septemba mwaka huu kama mnavyotuona pichani.(Picha na Francis Dande).

No comments:

Powered by Blogger.