Header Ads

CHADEMA ,WATANZANIA HATUDANGANYIKI NG'O


CHADEMA,WATANZANIA HATUDANGANYIKI NG'O
Na Happiness Katabazi

WASWAHILI WANASEMA ' Aliye jamba  atakunya tu. Ndivyo ambavyo  ambavyo Leo tume kusikia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,kwenye vyombo vya Habari kikisema eti kimenasa mawasiliano ya Ikulu ,Kuwa Rais  Profesa Jakaya Kikwete Kesho Katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, atatumia kuwasafisha watuhumiwa wa Zogo la Akaunti ya Escrow.

Watoto wa mjini tunajiuliza hivi Profesa Kikwete lini amegeuka tambala la deki, fagio  au sabuni ya kusafisha mahali au watu waliyochafuka?

Tuiuleze  Chadema hayo mawasiliano waliyoyanasa ni mawasiliano ya aina gani maana mawasiliano yanafanyika kwa njia gani?

Watuonyeshe basi hicho kielelezo cha mawasiliano  Tumaini Kuwa ni kweli? Kwa hiyo ndiyo mnataka naye Ndugu yangu Mkurugenzi  wa Mawasiliano Ikulu, atimuliwe kazi?Maana mawasiliano ya Ikulu yapo chini yake  ,mnataka wahusika wamchukilie ?

Kwanza nawaualiza Chadema wasiwasi wanini Kama mnaoga barazani? Rais Kikwete alituacha tubwatuke weee na tu kibwatuka, sasa ni zamu yake nayeye Kusema ya moyoni.

Sasa Chadema kina wawasha kitu gani hadi mfukunyue, muitishe mkutano na waandishi wa Habari mseme hayo yote mliyoyasema Leo?Mbona hotuba nyingine za rais Kabla hajautubia Mbona uwa hamna yao jitihada za kwenda kunasa mawasiliano yake Kabla ya hotuba?

Kwanini mnahaha kunasa mawasiliano ya hotuba ya Kesho ya Rais Kikwete? Wenye akili timamu Tumeamua kukubaliana na Msemo huo wa waswahili usemao ' Aliyejamba atakunya tu'. 

Na Tayari wazushi,wanafki,Mabush Lawyer wa Escrow wameishaanza  kujisaidia haja kubwa kabla hata Profesa Kikwete atafika hata ukumbini kwenda kuongea na wazee wa mujini Dar ws Salaam. 

Kwa maana  kwamba wazushi, wanafki, waliopika majungu kuhusu Akaunti ya Escrow na kusababisha mtifuano ndani ya serikali na nje ya serikali na kuacha majeraha Katika mihili mitatu ya dola wameanza kujirudhiirisha wenyewe hadharani kupitia manendo Yao.

Msimamo wangu Katika zogo la Escrow ulikuwa wazi kuwa tusiwahukumu washukiwa hadi mamlaka husika zitoe taarifa ambazo zitatueleza Kuwa walihusika Kutenda Uhalifu au la.Wapo walionuna mkono na wapo walinipinga na kutukana,sikuwa jali.

Ni saa Chache zimebaki kufika Kesho jioni tumeshuhudie Profesa Kikwete, akihutubia umma.Naomba Mungu anipe uzima .Chadema Propoganda uchwara haisaidii ,acheni muda uamue tuwajue wazandiki ,wanafki na wapotoshaji ni wakinanani.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 21 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.