Header Ads

LOWASSA UWENDA URAIS UKAUSIKIA REDIO TBC1

LOWASSA UEWENDA URAIS UKAUSIKIA REDIO TBC1 
Na Happiness Katabazi. 

KWA  zaidi ya siku tano sasa zimesambaa taarifa zinazozilituhumu genge la 'Askari 'watiifu wa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye yupo mapumziko ya Zanzibar kuwa wanatapanya fedha kwa baadhi wa jumbe wa NEC ili waweze kumpigia kura za ndiyo Lowassa siku atakapogombea nafasi ya urais ndani ya CCM.

Tujikumbushe  taarifa ya  Kamati ya Maadili ya CCM  iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye Februali 18 Mwaka 2014  kwa vyombo Vya Habari.

Taarifa hiyo ni hii hapa :  Kati ya tarehe 13/02/2014 na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama. Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2014.

Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:- 1. Ndugu  Frederick Sumaye 2. Ndugu Edward Lowasa 3. Ndugu Bernard Membe 4. Ndugu Stephen Wassira 5. Ndugu January Makamba 6. Ndugu William Ngeleja Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika. Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-

 1. Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i). 2. Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo. 

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi. Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:- “Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.” 

Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama. Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu. Mwisho.

Nimelazimika kunukuu taarifa hiyo ili watakaosoma makala hii wakumbuke Chanzo cha Lowassa na Wafungwa wenzake yaani wakina Membe, Ngeleja, Sumaye na wengine Kutiwa hatiani, Chanzo Chake kilikuwa ni malalamiko na tuhuma Kama hizi mpya zinazoelekezwa kwa Lowassa na genge lake huko Zanzibar na hatimaye tuhuma zile zilifanya Kamati mbalimbali za CCM ngazi ya Taifa kuwahoji watuhumiwa na hatimaye kuwakuta na hatia Katika tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

Kwanza kabisa naomba Ieleweke wazi Kuwa sina ugomvi na Mzee Lowassa wala mtu yoyote anayetaka kugombea urais wa nchi hii.Mzee Lowassa hadi leo hii sijawahi kumshuhudia hadhari akisema atagombea urais , isipokuwa kumekuwepo nataarifa kuwa Lowassa na hao wenzake  waliokuwa na hatia  wanania hiyo na ndiyo maana vikao Vya juu Vya CCM vile wakuta na hatia katika makosa mbalimbali likiwemo kosa la kuanza kampeni Kabla ya wakati.

Ni haki Yao ya Kikatiba Kugombea urais mtu yoyote ambaye Ametimiza vigezo Kugombea na wakati anagombea anakikishe anafuata Taratibu zote za Chama Chake, na Sheria za nchi.

Kwa Kuwa Chanzo vile vikao Vya CCM kukeketa na kuwapatia Adhabu Lowassa na wenzake zilikuwa ni tuhuma na baada ya uchunguzi tuhuma zinathibitika Kuwa ni kweli.

Hivyo Katika makala yangu ya Leo nia jadili tuhuma mpya zilizoibuka muda mfupi baada Mzee Lowassa Kwenda Zanzibar kupumzika Kuwa ' Askari wake   Watiifu' wanashiriki kutoa Rushwa za wazi wazi kwa baadhi ya wajumbe wa NEC ili waipigie kura za ndiyo Lowassa Katika Kikao Cha kupitisha jina Moja la mgombea atakayepeperusha Bendera ya CCM Katika nafasi ya urais Mwaka 2015.

Tuhuma hizi ziwe  za kweli au uongo, hazipendezi kusikilizwa Katika masikio ya wapenda haki na wapenda maendeleo. CCM Kama Chama Moja ya sera zake ni kupinga  Rushwa licha baadhi ya wanachama wake wamekuwa wasishiriki kufanya vitendo hivyo.

Wakati tuhuma hizo za genge la Lowassa kumwaga Fedha Zanzibar zikiendelee kushika kasi, bado Mzee Lowassa ajajitokeza hadharani kukanusha tuhuma hizo licha Makamu Mwenyekiti wa CCM ,Philip Mangula amenukuliwa na Gazeti la Raia Mwema  bila kutaja majina ya watu CCM ina vikao vyake na ikithibitika wanafanya hivyo watachukuliwa hatua.

Kama Mtu una akili timamu ukilisoma tamko Hilo hapo juu la Nape, ni wazi Hilo tamko ni kitanzi kikubwa kwa Lowassa na wenzake na wengine ambao Wataanza kampeni mapema.Ila   naona wakosoaji hao  uwenda hawakulielewa Hilo tamko Kuwa ni kitanzi Cha wazi Kwao.

Wangekuwa wameelewa  kitanzi hicho ,Wafungwa Hao  Mara nyingi upenda kuwatumikia wapambe wao kuwanadi kiaina Wafungwa Hao,wangetulia na wangesubiri muda wa rasmi wa kuanza kampeni utangazwe na Chama chao uanze ndiyo nawao waanze kujipitisha.

Au Kama Hilo limewashinda basi wangekuwa wakifanya kampeni zao kimya kimya kuliko mbinu hizi za kifedhuli wanazozifanya wazi wazi ambazo zinaonyesha wazi kabisa wanajimaliza wenyewe.

Kwa uelewa wangu, hicho kitanzi Cha CCM  kwa Lowassa na wenzake naona ni Kama Tayari  kimeishawaondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais baadhi ya Wafungwa ndani ya CCM.

Maana tamko Hilo la Nape limesema wazi kabisa licha ya Lowassa na wenzake kupewa Adhabu zile ,bado wataendelea Kuwa chini ya uchunguzi wao na wapambe wao. 

Na Hakuna Siri ni kweli Baadhi ya wafuasi wa Makundi ya watu wanaotajwa Kugombea Urais ambao wamepewa Adhabu wanaendelea na Kampeni za wazi wazi kupitia maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba za Ibada na kwingineko.

Na akili zao zilivyo mbovu wanazani  hawaoenekani,wamejificha kwenye Giza Kumbe wamejificha kwenye mawingu watu tunawaona.

Mzee wangu Lowassa minakuomba ujitokeze utolee ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo ambazo kwenye mitandao zinataja majina ya baadhi ya mawaziri na wakuu wa mikoa ndiyo eti wamepewa jukumu na wewe la kuwahonga fedha watu muhimu katika mchakato wa kuteua jina la mgombea urais.Tuhuma hizi zimeanza kukuchafua tena.

Narudia tena kukushauri Mzee wangu Lowassa Kama kweli unania ya Kugombea urais mi nasema ni haki yako, naomba sana kaa chini itazame upya hiyo kambi yako na safu yako ya ushindi.

Misioni Kama hiyo safu yako  Kama inakusaidia sana   maana kama ungekuwa na wapanga mikakati wazuri  wasingekuwa wanakushauri uanze vurugu hizo mapema kabla ya muda rasmi wa CCM ambao itakuwa imeupanga. 

Kumbuka tayari CCM imeshakukuta na hatia ya kuanza kampeni kabla ya wakati, na baadhi ya wafuasi wako ni wapuuzi kwani hawana siri, wanabwabwaaja mitaani siri za kambi yako hali inayosababisha maadui wako wa kisiasa kusambaratisha kiraini kambi yako bila kujua,wajuzi wa mambo wanaamua kukutazama na kusema wanakuacha kwanza hao wapambe wako wakulie fedha zako weee huku wengine unaowaona ni wema kwako wa akusanya taarifa za kambi yako Kisha wanapeleka taarifa hizo Katika kambi nyingine.

Lowassa ni Kada Mwandamizi wa CCM na ameishawachukilia  Kuwa Waziri Mkuu, CCM kukuta na  hatia kwa  makosa ya utovu wa Maadili ndani ya CCM na Katika Jamii ni Makosa Mabaya ambayo yameshusha heshima yako Mbele ya Jamii.

Hata ikitokea Leo hii wewe na Hao Wafungwa wenzako kati yenu akafanikiwa kuchaguliwa Kuwa mgombea urais na Akawa rais wa nchi hii, hivi mnaweza Kuwa na ujasiri wa kukemea wanachama wenu wanaovunja Maadili ndani ya CCM wakati Tayari Nyie mlishapatikana na makosa ya utovu wa Maadili?Jibu ni Jepesi,hamtaweza..

Lowassa Kumbuka wakati unachaguliwa Kuwa Waziri Mkuu Bunge na bunge ,ulishangiliwa sana, lakini balaa la Richmond lilipokukumba wanasiasa na baadhi ya wanachi ambao waliokuwa wakikushangilia ndiyo walikuwa  wa kwanza kuvishutumu na Kukupaka matope  maneno Mabaya Kuwa wewe ni Fisadi Mkuu na mengine yalikuwa ni ya kizushi.

Ghafla watu hao kuanzia Mwaka Juzi hadi sasa baadhi Yao wamejitokeza hadharani Kusema Lowassa ni mtu Msafi sana,mwadilifu, siyo fisadi, ni Chuki tu za Rais Jakaya Kikwete, unafaa Kuwa rais wa Tanzania Kwa Sababu unafahamu kuchukua maamuzi magumu na wengine wote hawafahai isipokuwa ni wewe.

Mimi Binafsi namfahamu Lowassa Kuwa ni mtu ambaye kweli anachukua  maamuzi Katika jambo Fulani licha kuna baadhi ya maamuzi aliyowahi kuyachukua  yaliiletea Shida serikali mfano alipoamuru maghorofa mawili yaliyokuwa yamejengwa eneo la Masaki Dar es Salaam, ya vunjwe,kweli yakavunjwa na mwisho wa siku mmliki wa maghorofa akafungua  Kesi Mahakama Kuu Kitengo Cha Ardhi na serikali ikatakiwa imlipe fidia mmiliki Huyo wa majengo.

Lowassa ni kiongozi ambaye akitaka jambo lake lifanyike basi ataakikisha Hilo jambo kinafanyika ikibidi hata kumwajibisha Mtu atamwajibisha.Licha tabia yake ya Kuwafokea hadharani baadhi ya maofisa wa serikali Katika ziara zake aliyokuwa akijifanya wakati akiwa Waziri Mkuu zilikuwa zikiwakera watu wastaarabu na waumini wa Sheria Kwani Kiongozi bora hawezi kukemea kwa kuwadhalilisha maofisa wake adharani  kwa Kigezo tu awakate kueleza jambo Fulani analolitaka kwa wakati.

Pamoja na mazuri  hayo ya Lowassa, minaona hii tuhuma zinazomwanda Kuwa ameandaa Fedha nyingi za kuakikisha jina lake linapitishwa Kuwa mgombea urais,   genge lake limekuwa likigawa Fedha kwa Lengo na kuamini Kuwa Fedha ndiyo njia kufanikiwa jina lake lipitishwe Kugombea urais ,utamwangusha siku za usoni.

Maana Imefikia mahali sasa tuna hoji Fedha hizo Hilo genge lake inazipata wapi? Kwanini basi genge linaona Fedha ndiyo silaha Kuu ya ushindi?Kumbe Ina maana basi hawa wajumbe wa NEC ni wachafu hawa pigi kura kwa Hiari Yao ila Rushwa?CCM inajenga Chama gani na viongozi wa aina gani?

Kama Lowassa kweli unakubarika na watu Wengi kwanini uanze kampeni mapema?Manaa tamko hilo limesema wewe na wenzako mlikutwa na hati ya kuanza kampeni mapema?Kama kweli unakubarika  kwanini genge Lako lituhumiwe kutoa Rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa NEC ili wakuchague huko Zanzibar?

Kama kweli Lowassa unakubarika hofu ya nini hadi uanze kampeni mapema?.Kama wewe na Wafungwa wenzako mmeshindwa kuheshimu Kanuni za Chama chenu mnazivunja kwa makusudi hadi mmetiwa hatiani na Chama chenu, ni vipi sisi wananchi tusipate Mashaka ya kuvitaka vikao Vya CCM vinavyopitisha Majina wagombea urais visipitishe Majina yenu kwasababu hamfahi Kuwa Marais kwasababu endapo mkiwa Marais mtakuwa wa kwanza kuvunja Sheria za nchi?

Kama kweli Mzee wangu Lowassa unakubarika na wafuasi wako, Kwani Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotangaza Kuwa atagombea urais kimya kimya, Mbona baadhi ya waliokuwa wafuasi wako waliama kambi yako na kwenda Kambi ya Pinda?

Mimi ni Mtu Mdogo sana Katika taifa hili kimadaraka, ila Mzee wangu Lowassa kwa mtindo huu na tuhuma hizi ukae ukijua zinazidi kukuweka  kwenye nafasi Mbaya Katika harakati zako za kutaka urais.

Sikuombei Mabaya wala sikutabirii Mabaya ila minaona hivi  ndivyo itakavyokuwa, tuombeane Uhai.Hii ni Moja ya sifa Mbaya sana licha Leo hii unaweza kuipuuza.

Mbaya zaidi baadhi ya waliodai kupatiwa Fedha kutoka kwa baadhi ya wafuasi wako huko Zanzibar wamesema ' Wewe ni Kama babu jinga kaa chini ufikiri mali yako inaliwa.

Na wengine wanasema  ' wajinga ndiyo walio wao'. Wanamaanisha wewe ni Mjinga  hivyo Fedha zako watazidi kuzitafuta  lakini kura ya ndiyo watampa   mgombea ambaye aandamwi  na skendo za kumwaga Fedha na kuvunja Taratibu na Kanuni  za CCM ambapo wewe  Lowassa  na wenzako Februali Mwaka 2014 CCM iliwatia   hatiani kwa  makosa hayo na kwamba bado kuna taarifa zinadai Ujakoma ,unaendelea kujihusisha na vitendo Vya utovu Maadili na kuvunja Kanuni za CCM.

Lowassa Mzee wangu nakukumbusha Kuwa Ufahamu Kuwa Watanzania wengi Hasa ndani ya CCM ni wanafki na wazandiki, Leo hii wanakushabikia na wanajifanya wema kwako kwasababu wapo kwenye kambi yako na kuna manufaa wanayapata  na wengine ni Bendera Fuata upepo.

Lowassa   Mungu amekujalia kitu Kimoja kikubwa sana una moyo wa kusaidia watu,huu moyo unao sana. Sikuombei Mabaya itokee usishinde ,ndiyo utawajua vizuri wale wote waliokuwa wakijifanya ni Askari watiifu kwako, watakuama na maneno ya shombo juu watakupakaza. Tusubiri na yatatimia wakati ukifika.

Lakini uchafu wote huu na tabia chafu ya kuzushia watu uongo hadi inaenea kwa Kipindi kirefu halafu ukweli unakuja kujulikana baadae sana naweza Kusema unasababishwa pia na Rais Kikwete kwa tabia yake ya kuacha uzushi uenee, watu wanaovunja Sheria ,Kanuni watambe na madhara ya Kisha tokeo ndiyo anaibuka na kutoa tamko wakati Tayari watu wameishaathirika na kupata madhara kutokana na matendo hayo Mabaya na wakati mwingine ni uzushi na uonevu. 

Binafsi tabia hii ya rais siipendi hata kidogo na akikasirika akasarike ila ukweli nimesema. Maana tabia hiyo hiyo ndiyo pia imesababisha nchii hii hivi sasa kuwa na wazushi ,wanaotajwa kugombea ndani ya CCM kufanya wanavyotaka.

Na ndiyo maana  Katika Utawala wake Leo hii kila mtu anafanya analoweza mwenye kutaka kumwagia kinyesi ,ukoko,kinyesi,Kuzushia wenzio uongo anazusha kwa kisingizio Kuwa Hakuna wa kuwachukulia Hatua na hata Kama akijakuchukuliwa Hatua basi hatua hiyo atachukulia baadae sana  ila tayari Lengo lake linakuwa limeshafanikiwa.Tabia chafu sana.

Nafasi ya Kiti Cha Urais ni nafasi nyeti na haitaji majaribio. CCM tunaomba itupatie mgombea kwanza mwenye afya njema  ambaye anaweza kuhimili miki miki ya Kampeni za Mwaka 2015 na Ikulu. Kwa kifupi Tanzania hatumuitaji  Michael Sata mwingine.

Tunaitaji rais msomi hasa na ambaye ana heshimika ndani na nje ya nchi ,anayejiheshimu na ambaye anaweza Kuinyosha CCM na serikali kwa ujumla maana siyo Siri kuna Ujinga Ujinga ambao unafanywa na baadhi ya watumishi wa umma na wana CCM ,wafuasi wa vyama vya upinzani na wananchi wa kawaida ambao hauna tija kwa Taifa hili na bado unaendelea kuchekewa.

Asiye  na jazba ,kuandamwa na tuhuma za genge lake kugawa Rushwa , visasi ,ambaye hajawahi kutuhumiwa kuendelea kuvunja kanuni za CCM ,akili zake ambazo zimetulia na yupo Tayari kuitumikia Tanzania kwa moyo wake wowote na siyo kuwatumikia kwanza Mabwana  zao waliowapatia Fedha za kuwahonga baadhi ya wajumbe wa NEC wapitishe Majina Yao na kufanya kampeni kabla ya wakati.

Tunataka rais atakayekomesha  tabia hii ya uzushi, umbea ,kupakaziana ambao tabia hii imeonekana kushamili sana katika utawala huu wa serikali awamu ya nne. Tunataka rais mwenye maono na atakayeivusha taifa la Tanzania Kuwa miongoni mwa Mataifa yenye Nguvu ya kiuchumi, na kuleta mshikamo miongoni mwa wananchi maana mshikamano miongoni mwetu umelegalega. 

Nashauri vyombo husika Vya CCM vifanye kazi tuhuma hizi za Uvunjifu wa Kanuni zinazofanywa na baadhi ya watu wanaotajwa Kugombea urais na ikiwakuta na hatia kuwachukulie Hatua wote bila kumuogopa mtu.

Maana hivi sasa dhana iliyo jengeka ni kwamba Kama huna Fedha 'maburungutu' huwezi kupata madaraka.Na wakati mwingine minaona wanaofikiri hivi ni kweli mAana tumeshuhudia chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa Disemba 14 Mwaka huu, tumeshuhudia siyo tu wagombea wa CCM, Chadema na baadhi ya vyama vingine wametumia  mbinu chafu ikiwemo kutoa Rushwa Katika vikao husika na kwa baadhi ya wananchi ili wa wapigie kura.

Lowasss nakuomba urejee makala yangu ya Machi 25 Mwaka  2012 iliyochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima iliyokuwa na kichwa Cha Habari kisemacho ' LOWASSA UMEANZA MAPAMBANO NA SERIKALI'. 

  Katika Paragraphu ya  makala hiyo 35,36 ,35  nilikuasa  uache kutumia nyumba za ibada kujisafisha hukunisikia  Matokeo yake Makachero  wa CCM  walikuchunguza na kuona nikweli kule kwenye nyumba za ibada ulikokuwa unakwenda kusali na kushiriki harambee ulikuwa ukifanya kampeni za urais kiaina na Matokeo yake ukakutwa na hatia ya kuanza kampeni mapema na Kifungo juu na upo chini ya uchunguzi.

Na CCM ikatoa amri ya Kuzuia Mwanachama yoyote kutoa zawadi kwenye nyumba za ibada, kwenye harambee bila Kibali cha Chama.

Binafsi namfananisha Rais Kikwete ni Kama ' Askari Adui'. Yaani unaweza ukafikiri yupo pamoja na wewe anakulinda Kumbe ukimpa Kisogo a nakupigia risasi ya mgongo. 

Anakuchekea ila anakuacha ushughulikwe na mamlaka husika au anakutimua kazi huku anacheka na kujionyesha hakuwa haki fahamu chochote Kabla hujasurubiwa.

Na ndicho kilichokukuta wewe Lowassa Februali 2008 ,Bungeni siku ile ulipo shambuliwa  na wabunge wenzio Kuwa umeleta kampuni ya 'mfukoni 'ya Richmond na kwamba haina huwezo wowote. 

Tuliotazama Bunge Tuliona ulivyoshughulikiwa na maneno mazito na miongoni mwa watu waliokusurubu ni Askari wako watiifu wa sasa Beatrice Shelukindo ambaye yupo nchini India kwa matibabu , Christopher Ole Sendeka tena huyu Sendeka yeye na waliokuwa wanamgambo wenzake wa ufisadi walituaminisha Hakuna kampuni inayoitwa Richmond ni Stationary  tu na ipo pale Kariokoo wala haipo Marekani na kwamba ingekuwa China, Lowassa ungekuwa umeishanyongwa.

Lakini  kwa Kuwa siku zote minaamini penye ukweli uongo ujitenga, jina la Richmond lilibadilika na Kuwa Dowans na mwisho wa siku jina la Dowans lilibadilika na Kuwa Symbiom Power na Rais wa Marekani ,Michael Obama alipokuwa hapa nchini kwa shughuli zake za kikazi pia aliongozana na Kikwete kwenda Kufungua Mitambo ya Symbion Power ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Richmond na Mchora Katuni wa Gazeti la Tanzania Daima, Said Michael ' WAKUDATA' wakati Sakata la Richmond limepamba Moto alichodai Katuni    
aliyoipa jina la RICHMONDULI .

Tuliokuwepo kwenye vyumba Vya Habari Mwaka 2005 Kabla ya jina la rais Kikwete alijapitishwa Kuwa mgombea pekee wa Kiti Cha urais, nilikushuhudia wewe Mzee Lowassa , Marehemu Mzee wangu Ditopile Mzuzuri na baadhi ya watu wengine Mlivyokuwa mstari wa Mbele kuakikisha Kikwete anashida na kweli alishinda.

Lakini Katika awamu ya kwanza ya Utawala wake Ditopile alikumbwa matatizo ya Kesi ya Mauaji  lakini siku Chache baadae alibadilishiwa shitaka la Mauji na kushitakiwa kwa kosa la Kuua bila kukusudia na alipata dhamana .

Mzee Ditopile alipokuwa gerezani Keko nilikuwa nazungumza  naye kwa simu, na nilikuwa na kwenda kumuona na hata alizopata dhamana Mara nyingine alikuwa akiniita sehemu zetu tulizokuwa tutakutana ananipa umbea wa nchi hii unavyokwenda na njia walizozitumia kumuingiza Kikwete Ikulu.

Nilijifunza mengi sana toka kwa Mzee wangu Ditopile lakini yote  aliyokuwa akinieleza sikuyatoa adharani . Kikwete alikuwa na mamlaka ya Kuzuia Ditopile asishtakiwe  na Lowassa asijihudhuru  lakini aliamua kuacha Sheria ichukue mkondo wake.

Kwa Mifano hiyo tu michache licha ninayo mingine mingi tu ya ambayo baadhi ya wafanyabiashara, wana CCM ambao walikuwa kwenye Timu ya Kikwete wakati akisaka urais lakini ,vyombo vyake dola baadae vikabaini watu hao wanatuhumiwa kufanya makosa ya jinai serikalini yake iliwafikisha  mahakamani ,walioshinda Kesi walishinda walioshindwa walishindwa  Kesi na wanaondelea na Kesi zao mahakamani bado wanaendelea nazo na Mfano mwingine ni Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Dar es Salaam, Madabida anakesi ya jinai pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuingiza nchini dawa za RVs feki. 

Sasa Mzee wangu Lowassa muogope Kama kirusi cha ugonjwa wa Ebola Mtu mmoja anaitwa Rais Jakaya Kikwete.Ni mtu asiye tabirika na wala  Haoni Hasara kuona Mtu aliyeshiriki naye kwenye misheni Fulani anasurubiwa na vyombo vyake kaamuacha asulubiwe. 

Na ile Kauli ya Mangula aliyoitoa kwenye Gazeti la Raia Tanzania la Disemba 29 mwaka 2014 ambapo amenukuliwa akisema:  " Sisi tunaendelea kuhubiri wasitoe  Rushwa ,Rushwa ni adui wa haki ,Rushwa ni dhambi.Kwani Ulishaona padre au sheikh ameacha  kuhubiri  kwa Kuwa watu wanaendelea na dhambi?

" Lakini hukumu yake si ipo kwa wanaendelea na dhambi hizo? Na Katika siasa pia ni hivyo hivyo. Waache waendelee, lakini hukumu Yao ipo , ikithibitika watakula hukumu Yao.

" Uzuri Chama chetu kina Kamati za Maadili kuanzia ngazi ya Kata hadi Taifa. zote hizi kweli zitamuogopa Mwanachama mmoja? Hakuna  Mwanachama  aliyejuu ya Kamati  za Chama . Chama ni vikao , hakuna  Kikao kinaweza kumuogopa Mwanachama wake," alisema Mangula.

Mtu mwenye akili timamu atayatafakari kwa mapana maneno hayo ya Mzee Mangula.Hayo Maneno Mangula anamaanisha anachokisema.Hivyo kwa wale mlionza kampeni mapema mumeambiwa muendelee ila mfahamu Kuwa CCM Ina vikao vyake havimuogopi Mwanachama wake.Haya ni Maneno Mazito.

Lowassa narudia tena kukuasa Mzee wangu muogope sana Kikwete Manaa kwanza Anaujua uhuni wote wa ndani na nje ya Chama, Hana papara Katika maamuzi yake na wala hatumiagi  Nguvu kuongea Kama viongozi wa vyama Vya upinzani wanavyotumiaga Nguvu kuongea majukwaani ila ujumbe unawafikia walengwa.

Na Kama una unafikiri Sawasawa unapaswa ujipe  muda ujiulize ni kwanini chini ya Utawala wa Mwenyekiti wa CCM Kikwete, iliamua kuanzisha Kanuni za Uongozi na Maadili  za CCM  Toleo la Februali 2010?

Pia Unatakiwa ujiulize Kuwa wewe na Kikwete ni marafiki na hamjakutana barabarani lakini ni Kwani Kikwete Mara Kadhaa anakuacha ' upigwe ngumi za uso na vyombo vyake' yaani aliruhusu ujiudhuru nafasi ya Uwaziri Mkuu, aliruhusu Kamati za CCM zikukute na hatia na uwe chini ya uchunguzi? 

Inaitaji akili kubwa sana kutafakari haya na kukukubaliana na Msemo mmoja wa Rais Kikwete aliyowahi kuusema adharani  Kuwa ' Urais wake auna Ubia'.

Kwa uelewa wangu Mdogo, uanzishwaji wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februali 2010 , ni Kisu Kikali sana kitakachotumiwa Mwenyekiti wa CCM na Kamati zake kuwa chinja huku wakiwajaza wagombea wote ambao watapatikana na hatia za kuvunja hizo Kanuni . 

Minaamini Fedha siyo Msingi wa kila kitu, maana Kama Fedha ingekuwa ni Msingi wa kila kitu basi hata hao waliopo madarakani wasingekuwa basi wanapata hata Maradhi.

Lowassa jitokeze utolee ufafanuzi tuhuma hizi zinazosema wewe huko Zanzibar licha umedai umeenda kupumzika lakini kuna genge Lako linafanya vitendo Vya kugawa Rushwa.

Tuhuma hizo siyo nzuri hata kidogo na kwa Kuwa Makundi ya Kugombea urais ni mengi kuna uwezekano pia wakawa wamekuzushia maana uzushi ndiyo imekuwa ngazi ya kujipatia Umaarufu kwa baadhi  ya wanawasiasa wetu uchwara hapa nchini.

Kumbuka Wafungwa wote Sita waliohukumiwa na vikao Vya CCM hawajakata  rufaa hadi Leo kupinga uamuzi huo.Na Kwa Sababu hiyo 'Wafungwa' wote wamekubaliana na adhabu ile.

Lowassa nakushauri Tazama upya safu yako,maana haiingii akilini Kama safu yako ipo imara   ni kwanini kila siku inashambuliwa wazi wazi na kuelekezewa tuhuma chafu na hatimaye ukatiwa hatiani na vikao Vya CCM mapema?

 Isije Kuwa safu yako ipo hapo kwaajili ya kuzidi kukuingiza mtaroni maana tayari safu yako ya ushindi Februali mwaka huu , ilikuingiza Mtaroni na CCM ikakukuta  na hatia.

 Lowassa Wanasiasa , Watanzania hatuaminiki  Wengi ni ' Chaja ya Kobe' Maana chaja ya Kobe ina chaji aina mbalimbali za chaji iwe chaji ya simu ya Nokia, Samsung, Hiawei nk. 

Yaani mtu anajifanya ni mfuasi wako na unamuamini kabisa na kwenye vikao vya kamati za ushindi unamshirikisha kumbe ni chaja ya kobe, mchana yupo kwako usiku yupo kambi nyingine na akienda kwenye kambi nyingine anazipeleka Siri za mikakati yako ya ushindi na ndivyo wanavyokufanyia.

Kwa mwelekeo huu wa tuhuma mpya za kutoa Rushwa  zinazoelekezwa kila kukicha na tamko la CCM lilotolewa  na Nape ,Februali 18 Mwaka huu, ,mtazamo wangu naona Lowassa Uwenda urais ukausikia Redio TBC1.  Watoto mjini tunasema ' Lowassa sasa kazi ni kwako.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 30 Mwaka 2014.
1 comment:

Anonymous said...

Happy nashukuru sana kwa makala yako nzuri ambayo inatoa mwanga kwetu sisi wapiga kura ili kujua kinachoendelea dhidi ya watamani urais. Mimi najiuliza, hivi hizi pesa zinatoka wapi na zitarudishwaje? Hivi huu si utakuja kuwa mzigo kwangu hata kwa vitukuu vyangu? Kwani Ikulu kuna nini hasa hadi watu wawe kimwaga kwa pesa zote hizi? Nina mashaka makubwa na mbinu hizi. Pesa ikiwekwa mbele, watu wakanunua madaraka ni mwanzo wa nchi kupoteza dira, uchumi kushuka kutokana na pesa nyingi kuzagaa mitaani na matoke yake ni kupanda kwa bei za vitu. Tuwaangalie sana watu hawa.

Powered by Blogger.