Header Ads

HONGERA KIKWETE KUTEGUA KITENDAWILI CHA FEDHA ZA ESCROW


HONGERA KIKTWETE KUTEGUA KITENDAWILI CHA FEDHA ZA ESCROW

Na Happiness Katabazi

KWA  MIEZI  kadhaa Tanzania iliingia kwenye zogo na kujiuliza maswali ambayo walishindwa kupata majibu kuhusu je fedha za Escrow ni za umma au la?

Kitendawili hicho ambacho kilimshinda  Mwenyekiti wa Kamati ya  Mashirika ya Umma( PAC), inayoongozwa na Zitto  Kabwe na wenzake 24 ambao taifa linawategemea Kwani Kamati yake iliuaminisha umma na baadhi ya Wanasheria uchwara waliopo ndani na nje ya Bunge Kuwa Fedha za Akaunti ya Escrow ni za umma Kumbe ni za IPTL.

Msimamo wangu tangu mwanzo nilisema tusubiri mamlaka husika zifanye uchunguzi wake Kisha zitupatie  Jibu kuhusu watu waliotajwa Katika Escrwo kweli wamefanya makosa waliyotuhumiwa nayo? 

Fedha za Escrow ni mali ya Umma? Je Fedha za Escrow zilibwa kweli na maofisa wa serikali ?Je utaratibu wa kutolewa Fedha hizo Katika Akaunti hiyo hazikufuata Taratibu? Je kuna harufu ya Rushwa.

Profesa Kikwete amesema baadhi ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Rushwa, Maadili zinaendelea ila akategua kitendawili Kuwa Fedha za Escrow siyo mali ya umma huku akatumia vielelezo Kuwa Fedha za escrow siyo za umma ni mali ya IPTL.

Sasa kwa hotuba ya Rais  Kikwete ni wazi zile hisia za baadhi ya watu zilizosababishwa na Kamati ya PAC na wanasiasa uchwara ambao sasa tumewabaini ni uchwara  Kuwa kuna mchezo mchafu  Katika Fedha zile ambazo zilihusisha Majaji,watumishi wa serikali Kuwa Fedha za escrow zilibwa,Rushwa,na kwamba Fedha za escrow ni Fedha chafu.

Hivyo hisia hizo zimekufa  rasmi Leo Kwani kupitia hotuba ya Rais Kikwete makosa ya wizi yamekufa kifo Cha Mende.Maana Fedha hizo ni mali ya IPTL siyo serikali, na IPTL hawalalamika Kuwa Fedha zimeibwa.

Pole Habinder Singh  mmiliki wa PAP ambaye amenunua hisa zote za IPTL kwa kutaka kudhurimiwa  pato lake  halali na Kamati ya BUnge ya PAP inayoongozwa na Zitto ambayo Kamati hiyo ilituaminisha Kuwa  Fedha hizo ni za umma wakati si kweli.

Singh Ondoa kinyongo  ,ushauri wangu fanya Kama aliyofanya Lugemalila alivyopata Fedha zake alilipa kodi yetu, na ninakupongeza kwa  kitendo Chako Cha uungwana Cha kukubali ombi la TRA la kulipa kodi yetu baada ya hapo fanya Kama Mtanzania mpenda maendeleo Lugemalila maana Rais Kikwete ametuambia amelipa kodi, wapatie zawadi ya Christmas na mwaka mpya wajumbe wa Kamati ya PAC.

PAC ya Zitto na mhasisi wa hoja ya Escrow David Kafulila ilituaminisha kwamba Fedha za Escrow siyo za Sighn.

Kuwa Sigh ni mwizi mkubwa na jambazi kwamba ulishaitikisa  serikali ya Kenya lakini Leo  Profesa   Kikwete ambaye ndiye Mkuu wa nchii hii na ndiye Mkuu wa Mashirika ya umma ambayo yanakaguliwa  na PAC ya Zitto na ndiye Mtendaji Mkuu wa serikali  Kuwa wewe siyo mwizi wa hizo Fedha na Fedha zilizokuwa zikiifadhiwa Katika Akaunti ya Escrow ni mali ya IPTL.

Napongeza hotuba ya Kikwete Kwani pia ameweza Kutupatia kiasi sahihi Cha Fedha zilizokuwa zimeifadhiwa Katika Akaunti ya ESCROW.

Kamati ya Zitto iliuaminisha umma Kuwa Katika Akaunti ya Escrow kulikuwa na sh .Bilionioni 306.7  Kumbe Kiukweli kiasi hicho ni uongo mkubwa na uzushi na kwamba kiasi halisi kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye Akaunti hiyo ni Bilioni 202.9. 

Tuiulize wajumbe wote wa PAC walishindwa kutoa takwimu halisi za Fedha hizo?Maana haiingii akilini wajumbe zaidi ya 20 wa PAC washindwe kupata takwimu sahihi ya fedha hizo na wadanganye umma  Kiwango hicho Cha Fedha Na kuaminisha umma Kuwa Fedha za Escrow ni za umma?

Maana mapungufu ya ripoti ya PAC yalisababisha umma kuingia katika zogo?Je walikuwa wajipumbe wa PAC walikuwa wana lao jambo?

Itakumbukwa Kuwa Ijumaa,  iliyopita niliandika makala ya kumpongeza aliyekuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi ,Profesa Anna Tibaijuka ambaye Leo rais Kikwete ametengua  uteuzi wake kwa kosa la kimaadili Kuwa niliungana mkono msimamo wa mwana mama huo wa kukataa kujiudhuru hadi apewe nafasi ya kusikilizwa na Leo Rais Kikwete ametuambia walimuita ,wakamhoji  wakawaambia awapishe na amekubali.

Napongeza Hatua hiyo ya Rais Kikwete ya kutoa nafasi hiyo ya kumsikiliza kwanza Profesa Tibaijuka na kisha rais akachukua uamuzi wa kumtaka ampishe katika baraza lake mawaziri kwa makosa ya Maadili kwani mashaka na maswali kwanini fedha zile hazikuingizwa kwenye akaunti ya shule hadi ziingizwe kwenye akaunti yake binafsi na Lugemalila. 

Kwa mujibu wa Kikwete , Tibaijuka ameachia ngazi Katika nafasi ya unazidi siyo baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya Rushwa,wizi Kama alivyokuwa akituhumiwa na baadhi ya wananchi.

Hivyo kwa Kuwa Fedha zile alizopewa Tibaijuka na Lugemala na kuingizwa kwenye akaunti yake kama mchango wa shule. Kwa maana hiyo fedha alizopewa Tibaijuka siyo za Escrow, fedha za Escrow alipewa Lugemalila na wakala ambaye ni Benki Kuu na kwamba Tibaijuka alipewa fedha za Lugemalila.Hiyo ndiyo dhana ya uwajibikaji.

Mwisho narudia kusisitiza Kuwa wananchi PAC imejifunjia heshima mbele ya watu wenye akili timamu kwasababu imetoa taarifa ambayo ina dosari za wazi ambazo zimeanishwa na Rais Kikwete leo, ambazo dosari hizo zimeleta madhara ya kushushiwa heshima kwa baadhi ya watu waliotajwa kwenye ripoti ya PAC kumbe baadhi ya data walizozikusanya hazikuwa na ukweli wowote.

Wale wazushi,waongo na ambao mlijiingiza kwenye mkumbo wa kuwahukumu maofisa wa serikali kuwa ni wezi wa fedha za umma za Escrow kumbe ukweli ni kwamba fedha za Escrow  si fedha za umma, mmemuhukumu mfanyabishara Sighn baadhi ya wanasiasa walituaminisha tumuone ni mtu hatari, mwizi kumbe siyo kweli. 

Kamati ya Zitto kwa upande mmoja imejiimarisha na HIvi sasa ikitoa ripoti yake wananchi tunaanza kuitilia Mashaka ,Kwani Kafulila alitoa inaisha Kuwa   Sigh ni mtu  hatari, jambazi na mwizi wa Fedha za Escrow na serikali isipokuwa makini ataiangusha Kama Sighn alivyoingusha serikali ya Kenya.

Kwa hotuba hiyo ya Kikwete, ni dhahiri hata Kafulila hivi sasa tutaanza kuitilia Mashaka baadhi ya hoja na Kauli zake anazozitoa Kwani Leo Kikwete amethibitishiwa Kuwa Fedha za  Escrow siyo za umma hivyo wale wanaodai ni za umma wanakosea na ni wazushi.

Hivyo wale vizabinazabina waliokuwa wakizusha uongo ,kupotosha umma kuwa Fedha zile za escrow ni za umma Leo wameumbuka.Mwenye nchi yake Kikwete amesema Fedha siyo za umma. 

Hongera Rais Kikwete kwa kutoa hotuba nzuri ambayo imetegua kitendawili Kuwa fedha za Escrow siyo mali ya umma ni mali ya IPTL na imetufundisha mengi Kuwa Kumbe hata Watunga Sheria wetu yaani baadhi ya wabunge wanaweza kufanya uchunguzi na Kuja maazimio yenye uongo na uzushi mkubwa ndani yake.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 22 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.