Header Ads

MBUNGE HIGHNESS KIWIA NI MWENDAWAZIMU?
MBUNGE HIGHNESS KIWIA NI MWENDAWAZIMU?

Na Happiness Katabazi
MWENDAWAZIMU ni neno ambayo Utumiwa kumtambulisha  Katika Jamii  binadamu ambaye Ana matatizo ya akili(Insanity) .

Mwendawazimu anakuwa Hana akili  za binadamu wa kawaida na anafanya matendo ambayo binadamu mwenye akili timamu hawezi kuyafanya.

Nimelazimika kutumia neno Hilo la Mwendawazimu  Katika makala yangu Kwasababu Jana nilishuhudia kupitia taarifa ya Habari kwenye Televisheni Mbunge wa Jimbo la Ilemela(CHADEMA), Highness Samson  Kiwia akifanya vitendo Vya kiuwenda wazimu ambavyo vinavunja Sheria za nchi na kuatarisha Usalama Katika eneo la kupigia kura la Mtaa wa Ibungilo B, Wilayani Ilemela.

Tulimshuhudia Kiwia akipokonya madaraka ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Ilemela,Justus Lukaza ya kutangaza Matokeo.

Kiwia ambaye ni mtunga  Sheria akajipa madaraka hayo  sijui kwa kutumia Sheria gani akamtangaza aliyekuwa Mgombea Kiti Cha Uenyekiti kupitia Chadema ,Mtaa wa Ibungilo B,  Ramadhani Said Kuwa ndiyo Mwenyekiti wa Mtaa huo kwa Madai kwamba ndiye chaguo la wakazi wa Mtaa huo  na kwamba hawawezi kuchaguliwa kiongozi wasiyo mtaka.

Kitendo kilichowafanya   Polisi kuingilia kati kuwatawanya wafuasi hao kwa kupiga mabomu ya machozi.

Kwa upande wake Msimamizi   wa uchaguzi huo Wilaya ya Ilemela ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wilaya hiyo,  Justin Lukaza,  alisema  kwamba matokeo yalimtangaza Mgombe kiti cha Mwenyekiti (CCM)  ni sahihi, kwani uchaguzi wa Disemba 14 walishindwa kutangaza matokeo kutokana na tofauti zilizotokea, hivyo leo wameamua kuyatoa na kwamba Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa Misingi ya Sheria.

Hivi wewe Kiwia kwa kitendo hiki ulichokifanya Jana Cha si tu  Cha kuvunja Sheria za nchi,pia Cha kukuvua nguo  wewe Mwenyewe Kuwa licha ya wewe ni Mbunge ambaye ni mtunga Sheria lakini umekuwa wa kwanza kuvunja Sheria za nchi,una akili timamu au ulikumbwa na kichaa Cha muda 'Temporary Insanity'?

Ni ule umati wa wananchi uliokuwa ukikushangilia ndiyo uliosababisha Utendaji ule uwendawazimu wa kuvunja Sheria za nchi na kuuthibitishia umma Kuwa wewe ni miongoni mwa wabunge wahuni?

Kiongozi  tena wa ngazi ya Mbunge Kama wewe Kiwia mwenye akili timamu anayefahamu Kuwa Moja ya sifa ya Kuwa kiongozi nikuonyesha njia watu anaowaongoza, hawezi kufanya uhuni alioufanya Kiwia.

Hivi baadhi ya viongozi wa Chadema ,vurugu zinawapa manufaa gani?Maana kila kukicha  ni kuamasisha maandamano haramu, uzushi,huyu naye Kiwia ambaye alinusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga naye jana kaibuka na kufanya uhuni wa kufunga mwaka wakati hana mamlaka ya kumtangaza mshindi.

Mbunge mwenye hadhi ya Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,unafanya ushenzi wa aina hii ili upate nini?Wale wananchi waliopata Kadhia ya kutawanywa na Polisi kwaajili ya uhuni wako,utawafidia vipi?

Hata Kama Msimamizi wa Uchaguzi aliufanya  makosa,kwanini na wewe usikemee na kufuata Taratibu za kupinga Matokeo hayo kwa Amani  lakini wewe mbunge mzima ndiyo ukashiriki Kutenda kosa hilo la kupora  madaraka ya Msimamizi wa uchaguzi?

Tumuulize Kiwia Huyo aliyetangaza Kuwa ndiye  mshindi , ameishamtafutia Ofisi ya kufanyia kazi? Na Yule aliyetangazwa Kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ibungilo B ,na Kiwia naye anakashangilia na Kubebwa juu juu Hivi Ana akili timamu?

Tumuulize Huyo  Said ,HIvi  Kiwia Ana madaraka ya kutangaza mshindi wa Kiti Mwenyekiti Serikali za Mitaa? Jibu ni Jepesi Hana madaraka hayo.

Hivi wewe Said ulivyoshiriki kinyang'anyiro chote cha Kugombea  nafasi hiyo  ulikuwa hufahamu nani mwenye madaraka ya kumtangaza mshindi?

 Tueleze basi Said ,Ofisi yako ipo Mtaa gani utakapokuwa ukiitumia baada ya Jana kutangazwa mshindi na mtu  asiye na madaraka ya kutangaza ushindi?

Kiwia Hufahai Kuitwa kiongozi bora, na samahani Kama nitakuwa mimekukera ila kwa tabia hii chafu ya baadhi ya viongozi wa Chadema kushiriki Kutenda matendo ya kijinai kuhatarisha Amani ya baadhi ya maeneo ndiyo inakighalimu Chadema sasa.

Maana hata baadhi ya wasomi waliokuwa wakikiunga mkono Chadema HIvi sasa wameacha Kwani wamesema wamebaini Chama hicho kimekuwa ni Chama Kinachoamasisha wanachama wake wafanye vurugu,uzushi na kufanya vitendo Vya kihuni Moja kwa Moja na hakitaki kukosolewa.

Kitendo kilichofanywa na Kiwia Jana kinafanywa na Mwendawazimu. Najiuliza Mbunge wa Jimbo la Ilemela , Highness Samson Kiwia ni Mwendawazimu?

Uenda Kiwia ni Mwendawazimu kwasababu hata kura alizopata Said ambazo zilisababisha Kiwia amtangaze Kuwa ni  mshindi Kiwia ajatutajia Kuwa Said alishinda kwa kura ngapi.  Naomba kutoa hoja.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog.www.katabazihappy.blogspot.com
Disemba 22 Mwaka 2014.

 

No comments:

Powered by Blogger.