Header Ads

MEMBE AZINDUA MFUKO WA ELIMU CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO(UB)

MEMBE AZINDUA MFUKO WA ELIMU UB
Na Happiness Katabazi,Pwani 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe amezindua mfuko wake wa elimu Katika Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), ' utakaojulikana kwa jina la ' Bernad Membe Scholarship 'Membe kwaajili ya kusaidia vijana wenye maitaji Maalum.

Membe aliyasema hayo Juzi Katika Viwanja Vya Hoteli ya Kiromo , iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika sherehe za Mahafali ya pili ya UB  na Kisha aliwatunuku jumla ya wahitimu 90 Shahada ya Uzamili,shahada ya kwanza, Diploma na Cheti wahitimu wote hao.

Membe ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amefikia uamuzi huo wa yeye binafsi kaunzisha  mfuko wake huo wa elimu ndani ya UB, kwasababu yeye anaamini kuwa elimu ni Taa na ufunguo wa maisha ya binadamu yoyote hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na kwamba kuna vijana wanaitaji kupata elimu ya juu lakini wazazi wao hawana huwezo wa kuwalipia Ada.

"Binafsi naamini ukimlipia kijana Ada ya chuo utakuwa umempatia kitu kikubwa sana kijana. ...hivyo mfuko wangu huu wa elimu niliyouanzisha hapa UB ,utasaidia Makundi hayo maalumu kulipiwa Ada ya chuo ...na nitayari nimeishaanza kufanya mazungumzo na baadhi ya watu wenye Fedha ili waweze kuingiza Fedha Katika mfuko huo  na ninawaomba matajiri ambao Mungu amewajilia kuwa na uwezo kiuchumi waanze kuchangia Fedha Katika elimu ili vijana wetu kote nchini ambao hawana uwezo wa kulipa Ada Fedha hizo zilizotolewa matajiri ziweze kuwasomesha "  alisema  Membe na kushangilia.

Kwa  upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Professa Costa Mahalu alisema anamshukuru Membe kwa uamuzi wake kimaendeleo kwa kuanzisha Mfuko huo , UB kwasababu hata sera ya bodi ya mikopo bado haitosholezi Mahitaji ya wahitaji wa mikopo ya kusoma elimu ya juu.

Profesa Mahalu alisema Taifa linaitaji kuongeza jitihada za Kuzalisha wahitimu bora wa elimu ya juu ili wasomi hao wawewe kuingia kwenye mapambano ya kuwatokomeza maadui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasiki na pia waweze kwenda kushindana katika soko la ajira katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Aidha Profesa Mahalu alisema kuanzia Januari mwakani, UB itaanza kujenga makazi yake ya kudumu katika kijiji cha Kiromo Bagamoyo  ambapo ujenzi ukikamilika kutakuwa NA uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5000.

Chanzo: Gazeti la Raia Tanzania, Desemba 9 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.