Header Ads

DK.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI UB






Dk.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI UB

Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais  ,Dk.Mohammed Gharib Bilal Kesho anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu  Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa Habari  ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam  Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema  sherehe hizo zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema  Januari Mwaka 2015.

Katabazi  alisema Dk.Bilal  ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa  mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa.

" Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu   katika mji huo, binadamu wote watakuwa  huru kwasababu tutapata elimu" alisema Katabazi.

Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni ,Dar es Salaam  na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu.

Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011 

Chanzo: Gazeti la Tanzania Diama, Jumatatu, Desemba Mosi Mwaka 2014


No comments:

Powered by Blogger.