Header Ads

HONGERA MEMBE KUANZISHA 'BERNAD MEMBE SCHOLARSHIP FUND'







HONGERA  MEMBE  KUANZISHA 'BERNAD MEMBE SCHOLARSHIP FUND'

Na Happiness Katabazi
DISEMBA  7 Mwaka huu,Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) Chenye Makao yake makuu ya muda Mikocheni B,Dar Es Salaam ambacho kinaongozwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho ,Profesa Costa Ricky Mahalu kilifanya mahafali yake ya pili.

Mahafali hayo yalifanyika Katika Viwanja Vya Hoteli ya Kiromo ,Bagamoyo Mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Mamia ya watu wakiwemo  maofisa wa juu toka Taasisi za kiserikali, watu binafsi na wakazi wa kijijini Cha Kiromo ,Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Nikiwa na wadhifa wa Afisa Habari  wa UB kwaniaba  ya Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo, Mosi, namshukuru Mkuu wa Wanadiplomasia nchini, Membe kwa kuichagua UB ndiyo iwe msimamizi wa Bernad Membe Scholarship Fund.

Pili, nawashukuru wale  wote walioshirikiana na UB  katika kufanikisha mahafali yake ya pili ya UB ambapo jumla ya wanafunzi 90 walihitimu kozi za fani mbalimbali ikiwemo kozi ya Shetia , Elimu  na Sayansi. Mungu awabariki.

Itakumbukwa mahafali ya kwanza ya UB yalifanyika  Disemba 6 Mwaka 2013 Katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal.

Na Mahafali hayo ya pili ya UB ,mgeni rasmi alikiwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe ambaye pamoja na kuwa alikuwa ni mgeni rasmi, pia  alikasimiwa madaraka na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo, Askofu Elinaza Sendoro  kuwatunuku shahada wahitimu wote kwaniaba yake kwasababu Sendoro alishindwa kuhudhuria mahafali hayo kwasababu alikuwa na hudhuru.

Membe alitimiza  majukumu yake aliyotakiwa ayafanye siku hiyo na aliyafanya KWA   unyeyekevu na kwakufuata Itifaki zote zilizokuwa zimewekwa na UB.

Katika hotuba yake siku hiyo,Membe aliwaasa wahitimu waingie Katika kusaka Soko la ajira na kujiajiri kwasababu anaamini UB imewapatia  elimu bora na Mungu atawasaidia kufanikisha Malengo Yao.

Membe akisoma hotuba yake Katika mahafali hayo alisema Amefikia uamuzi wa kuanzisha mfuko wa kusaidia wanafunzi wa Makundi Maalum ambao wanaitaji kupata elimu ya juu lakini hawana uwezo wa kifedha wa kujilipia Ada kwasababu anafahamu Umuhimu wa binadamu kupata elimu.

Alisema mfuko huo unaojulikana kwa jina la Bernad Membe Scholarship Fund  ambao utakuwa  chini ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo .

Alisema mfuko huo ukijazwa Fedha ,Fedha hizo zitatumika kusaidia kuwalipia Ada Makundi maalumu ambapo watakuwa wamepangwa na TCU kusoma vyuo vikuu vya binafsi na serikali na siyo UB peke yake.

Binafsi Nampongeza Membe kwa uamuzi huu ambao unatija kubwa Kwa vijana wa taifa hili. Waliopata baada ya kupata elimu ya juu watakubaliana na mimi kuwa elimu ni bidhaa isiyooza na haina mfano wake.

Hakuna ubishi Kuwa serikali kupitia Bodi ya mikopo imekuwa na sera nzuri ya kutaka wananchi wake wapate elimu ya juu kwa kuwapatia mikopo na kweli baadhi ya wanafunzi wanaostahili kupata mikopo na waliotimiza vigezo wamekuwa wakipata mikopo ya kutoka Bodi ya Mikopo.

Licha kumekuwepo na malalamiko Kuwa pia mikopo hiyo haitosholezi na nikama sera ya Utoaji mikopo ni ya ubaguzi.Vyovyote isavyo minasema  malalamiko hayo ni Changamoto ,wahusika wafanyie  kazi wakiona kuna haja ya kufanya hivyo.

Faida ya kuanzishwa kwa Bernad Membe Scholarship Fund, ni kubwa, Hivyo uamuzi huo wa Membe Unatakiwa uungwe mkono kwanza na watu wenye akili timamu, watu wanaompenda Mungu kwasababu hata Biblia inawanataka Binadamu waikamate elimu, Wanaofahamu Umuhimu wa elimu na wanaopenda maendeleo ya vijana wa taifa hili.

Ila kwa wale wafuasi wa shetani tu ndiyo wanaweza kupinga makala hii Na kupinga uamuzi huo wa Membe Kwani siku zote kazi ya shetani na wafuasi wake ni kuvuruga mipango mizuri na matendo mazuri inayoanzishwa na watu wake kwaajili ya manufaa ya binadamu wenzao ambao wameombwa na Mungu. Nitawapuuza .

Binafsi Mimi ni Mwanafunzi wa Sheria UB pia ni mfanyakazi wa UB, nafahamu ugumu wa alipata wanafunzi ambao hawana huwezo wa kulipa Ada Kwa wakati na wengine hawana hata uhakika wa kulipa ada ila wameingia kusoma chuoni na hawajui watapata wapi Ada ada wengine walikuwa wakilipiwa  ada na wazazi ,Jamaa zao lakini ghafla wazazi wao au Jamaa zao wakaharibikiwa kiuchumi au kufariki Kabla vijana wao hawajamaliza chuo.

Nimeshuhudia na minaendelea kushuhudia kuna baadhi ya wanafunzi wanasoma kwa  tabu sana na wengine kulazimika kuahirisha Mwaka wa masomo kwasababu Hana Fedha za kulipia hosteli, mkopo hautoshi, wazazi wake hawana huwezo wa kumlipia sehemu ya Karo.

Kuna  mwanafunzi mmoja wa fani ya Sayansi ,Oktoba  Mwaka huu, alifika Makao makuu ya UB, akiwasilisha barua ya kuomba kuahirisha  Mwaka kwasababu Hana Fedha za kulipa ada,Chakula, hosteli, photocopy, na baba yake Mzazi Kasema Hana huwezo wa kumlipia Ada wala kutumia Fedha ya Chakula  hivyo kijana huy  Huyo akaandika barua ya kuairisha Mwaka.

Niliumia sana Moyoni  na nilimsii sana asikabidhi hiyo barua chuoni kwasababu bado Ana muda Mungu  anaweza kumuinulia mtu  akamsaidia kumlipia Ada.

Yule Kijana aliendelea kushikilia  msimamo wake na akaikabidhi  ile barua kwa uongozi wa chuo Kuwa anaiarisha Mwaka wa masomo na akanieleza Kuwa amepata kazi ya kuendesha Tax , hivyo ataifanya kazi hiyo kwa Mwaka mmoja ili aweze kupata Fedha ili Mwaka Ujao wa masomo aweze kutumia Fedha hizo chuoni.

Lakini Mungu ni mwema Novemba Mwaka huu, kijana Huyo alirudi Katika Makao makuu ya UB , na Kusema Kuwa anaomba ile nakala yake ya barua ya kuairisha Mwaka iondolewe kwenye Kumbukumbu za chuo Kwani Tayari amepata Shirika Moja linamlipia sehemu ya Ada hivyo ataendelea na masomo.

Nilifurahi alivyonieleza Hilo, Kwani nafahamu ni jinsi gani alivyokuwa Katika Lindi la mawazo ya kukosa Ada, Kwani hata mimi niliteswa sana na tatizo Hilo lakini Mungu aliniinulia watu wakanisaidia.

Siyo kijana Huyo peke  tu , kuna wanafunzi Watano pale UB, wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha walifika ofisini kwa Makamu Mkuu wa UB, Profesa Mahalu na kumlilia Shida ,Mahalu ameamua sehemu ya mshahara wake itolewe ili Iweze kuwalipia ada wanafunzi hao na ni kweli wanalipiwa na wengine wamehitimu kozi zao. Mungu ambariki Mahalu.

Ndiyo maana nilipoona Membe kawa  nawazo  hili la kuanzisha mfuko huo , nimeamua kuandika makala ya kumpongeza Kwani Dunia ya sasa bila elimu ni matatizo sana.

Na Mataifa mengi yaliyo endelea ,yaliweza kuwawezesha vijana wao wakapata elimu ya juu. 

Tanzania nayo ambayo ni miongoni mwa Mataifa yanayoendelea, Hatuna  budi kuakikisha kila mmoja wetu ikiwemo serikali kuakikisha inawekeza Katika elimu ili vijana ambao hawana huwezo wa kuwalipia ada ,wanalipata elimu kwa kulipiwa ada.

Hivyo basi kuanzia Disemba 7 Mwaka huu, siku Membe ulipotangaza kuanzisha mfuko huo,vijana wa Makundi Maalum yanayoitaji kupata elimu ya juu ila hayana huwezo wa kujilipia Ada, wanaona ahadi hiyo ni deni jipya kwa Membe.

Hivyo Membe ukae ukifahamu uamuzi wako wa kuanzisha mfuko huo wa elimu ni deni Kwa wapenda elimu na Makundi hayo Maalum. Na tangu ulipotangaza uamuzi huo wanafunzi mbalimbali wamekuwa wakiuliza mfuko huo unaanza kutoa ufadhili lini.

 Hivyo unapolala,kuamka,kufanyakazi,kutembea ukae ukifahamu una deni kwa Makundi hayo yanayoitaji ufadhili wa kulipiwa Ada kupitia mfuko wako huo.

Kama ulivyosema Membe Kuwa utaakikisha unawasialiana na baadhi ya Taasisi zichangie mfuko .Nakutakia kila la kheri na Taasisi hizo zikubali kuchangia mfuko huo. 

Membe ameonyesha njia , naomba na wafanyabiashara na wanasiasa wengine mumuunge mkono  Membe Katika hili la kuchangia Katika elimu Kwani siyo Siri huku Katika vyuo vikuu kuna vijana wanaishi na kusoma Katika mazingira magumu kwasababu hawana ufadhili wa kutosha wa kupata Fedha za kujikimu wakiwa masomo ni.

Baadhi  ya wanasiasa,wafanyabiashara aachane na tabia ya kutapanya  Fedha ili zikafanyie  matendo machafu Kama baadhi ya wafanyabiashara ,wanasiasa wenye Nguvu ya kiuchumi kutoa Fedha kwa Makundi Fulani ili fedha hizo ziweze kutumika kuwachafua mahasimu wao kupitia Ndani ya Bunge, kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao.

Maana  hata Katika kile kinachoelezwa ni Mashaka Katika Sakata la Escrow Kuwa kuna baadhi ya Mfanyabiashara na Mwanasiasa  (Majina nayaifadhi) wamekuwa wakidaiwa kuwahonga  baadhi ya wabunge waende kupiga makelele bungeni ya kuwapaka matope wenzao kuhusu Escrow 
Spika  wa Bunge, Anne Makinda zaidi ya Mara mbili sasa amekuwa akiwataka  baadhi ya wabunge waache kutumiwa na wafanyabiashara Kuja kuwasemea bungeni ajenda zao chafu.

Hizo Fedha mnazowahonga baadhi ya wabunge na baadhi ya waandishi wa habari wachafue wenzao ,ningewaona wamaana sana hizo fedha zenu mngezitumia kuwasaidia vijana  wajiendeleze kielimu  na Mungu angewalipia yaliyo mema na kuwaponya hizo dhiki na maradhi yanayowakesa kila siku Kwani Fedha,mali mnazo lakini kila kukicha mnasumbuliwa na Maradhi.

Kuna raha gani Mtu una madaraka,Fedha na mali halafu una Afya mbovu?Mrudieni Mungu wenu na mtende yaliyomema uone Kama hatawaondolea kila aina ya mateso yanayowakabili.

Lakini   sehemu za Fedha Zenu mnazotumia kuwazushia wenzenu uongo  ,kutikisa nchi kwa uzushi na kupandikiza Chuki kwa wananchi ili wananchi wamchukie kiongozi Fulani kwa kumpachika Majina Mabaya Mabaya Kama fisadi,jambazi sugu ,mhadilifu  wa Fedha za umma wakati mioyoni mwenye mnafahamu Fika ni fitna tu mmeamua kwazushia  wenzenu, Mkae mkijua mnamchukiza Mungu na ipo siku Mungu atalipa kisasi kwenu kwaniaba ya Hao mnao wazushia uongo na kuleta taharuki Katika Taifa kwaajili ya ulafi wenu wa madaraka,Chuki, visasi Vya kunyimwa Rasilimali Fulani za taifa wakati hata vigezo wakati mwingine hamna.

Katika hili Nampongeza Membe ,na wahitaji wote Tushikamane ,kila Mara tumkumbushe Membe atekeleze ahadi yake hiyo ya kuzitafuta Taasisi zitunishe mfuko huo ili vijana Watanzania wasio na uwezo wapate elimu .

Mungu Ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 10 Mwaka 2014.

















No comments:

Powered by Blogger.