Header Ads

KILA LA KHERI JAJI WEREMA




KILA LA KHERI JAJI  WEREMA
Na Happiness Katabazi
LEO Disemba 16 mwaka 2014, Rais Jakaya Kikwete amekubali  ombi la kujiuzulu  kazi lilowasilishwa mbele yake na aliyekuwa  Mwanasherika Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Fredrick Werema .

Jaji Werema Katika barua yake hiyo ,amesema amefikia uamuzi huo kwasababu alipokuwa na wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa serikali alitoa ushauri wake wa kisheria Katika ESCROW, ushauri ambao Amedai umechafua  hali ya hewa.

Binafsi namfahamu Jaji Werema Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali Enzi hizo akiwa Jaji wa Mahakama Kuu na Ofisi zake zilikuwa ndani ya Jengo la Mahakama Kuu Kitengo Cha Biashara.

Kabla ya kuteuliwa Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Werema aliwahi Kuwa Wakili wa serikali hadi kufikia Cheo Cha Kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Haki za Binadamu.

 Nilipokuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka 15 nilipata fursa ya kupigana nae vikumbo na Werema kwenye korido za Mahakama na hadi  alipoteuliwa Kuwa Jaji nilikuwa naingia kusikiliza na kuripoti Kesi ambazo alikuwa akizisikiliza na kuziamua.

Aidha Jaji Werema alipoteuliwa Kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali pia nilikuwa nikiandika hotuba mbalimbali aliyokuwa akizitoa na kufanya naye mahojiano mbalimbali.

Namfahamu Werema Kama ni miongoni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa na hulka ya Kupenda kufanya mambo yake kwa uwazi, kujiamini hulka ambayo ilikuwa ikiwakera baadhi ya watu ambao hawataki kuambiwa ukweli kuhusu mambo Fulani.

Tuliomfahamu hulka hiyo ya Jaji Werema wala halikuwa hatupi Shida ,na tulimpenda  Kwani yeye alikuwa akipenda kutoa ushauri mapema wa jambo Fulani la kisheria Kabla hata watu hawajaamua kunifikisha mahakamani.

Ushahidi mmoja wa Jaji Werema Kuwa na hulka hiyo ya uwazi, na ukweli ni Kipindi kile wanasiasa uchwara walivyoshikilia  Bango  kuishinikiza serikali ikafungue Kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kulipa fidia ya Tuzo ilishinda kampuni ya Dowans dhidi ya Tanesco Katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara ICC.

Jaji Werema kwa zaidi ya Mara mbili ndani ya Bunge nje ya Bunge alijilipua na Kusema kwa mujibu wa Sheria ,serikali hata ikienda Mahakamani kupinga Dowans Isilipwe haitaweza kushinda kwa Sababu Katika Mkataba baina ya Tanesco na Dowans ,pande hizo mbili zilikuwa liana endapo wakikoroishana watakushinda kushitakiana Katika Mahakama Moja tu ya ICC.

Lakini wanasiasa uchwara waliipuuza ushauri wa AG- Werema na Kuishia kumtolea maneno ya kebehi .Wanaharakati , Tanesco wakafungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam,kupinga Dowans Isilipwe, Kesi Yao ikatupwa.

Hawakurudhika ,wakakimbilia Mahakama ya Rufaa huko nako Mahakama ya Rufaa Mahakama ikatupilia Mbali rufaa Yao. Dowans ikalipwa Fedha zao,na wasiasa Hao HIvi sasa wapo kimya.

Nakutakia kila la Kheri Mtani wangu Jaji Werema huko uendako unakoenda kuanza Maisha mapya. Mungu ndiye aliyeruhusu upate Cheo Cha Uanasheria Mkuu wa serikali na katika uamuzi wako wa Leo wa kujiuzulu  Cheo hicho pia naamini Kuwa ni Mungu pia ameruhusu uchukue uamuzi huo.

Hivyo ni Mungu Huyo pia aliyekuruhusu uachie madaraka hayo ,pia ni Mungu Huyo Huyo atatumia njia zake Kukupatia nafasi   nyingine ambayo uenda ikawa ni nafasi nzuri kuliko hiyo ya Uanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania ambayo  hata watu wasiyo na taaluma ya Sheria nao wamejigeuza Wanasheria.

Tungali tukikumbuka yaliyomkuta Werema Katika Escrow ,pia yanafanana na yaliyomkuta aliyekuwa Mtangulizi wa Werema, Johnson Mwanyika.Mwanyika alikuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali naye jina lake lilichafuliwa sana na wanasiasa na wananchi Katika Sakata la Richmond.

Lakini Mwanyika kujiuzulu  aliweka Pamba masikio hadi muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Sheria Ilipofika alistaafu. Kila lakheri Jaji Fredrick Mwita Werema na Mungu akutangulie katika Maisha mapya.

Mungu Ibariki Tanzania.

Chanzo: Facebook.Happy Katabazi
Disemba 16 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.