PAPA MSOFFE KORTINI KWA KESI YA MAUJI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya mauji.
Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa m
oja la mauji ambalo ni kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Wakili Kweka alidai kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika.
Kwa upande wake hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauji na mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote.
“Kwa sababu hiyo naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe gerezani”alisema Hakimu Mchome.
Msofe ambaye alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao.
Msofe ambaye jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji.
Itakumbukwa hivi karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu.
Aidha itakumbukwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Papa Msofe kufikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mbalimbali ya jinai.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Agosti 11 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment