HEKO SERIKALI KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI
Na Happiness Katabazi
WAHENGA waliwahi kusema ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni”
Januari 10 mwaka huu, gazeti hili lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Ugumu wa maisha utatuangamiza”.
Ndani ya makala hiyo nililamikia sana ugumu wa maisha na upandaji wa bei za vyakula.
Leo nimeamua kutumia msemo huo ambao naamini utasaidia kuunga mkono hoja yangu nitakayoijadili leo na makala yangu iliyochapishwa Januari 10 mwaka huu.
Leo nitajadili kuhusu upunguzwaji wa bei ya bidhaa ya vyakula hapa nchini katikia masoko mbali hivi sasa ukilinganisha na kipindi cha mwanzoni mwa mwaka huu.
Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu bei ya bidhaa za vyakula masokononi na madukani zilipanda kwa kasi hali iliyosababisha sisi waandishi wa habari kuandika makala za kukerwa na upandwaji huo wa bei na pia baadhi ya wananchi nao walipaza sauti kuonyesha kuumizwa na hali hiyo.
Lakini kwa sisi wanawake ambao hasa ndiyo mashuhuda wa kuu wa upandaji na ushukaji wa bei hizo ambao ndiyo tunaoenda masokoni na madukani kununua bidhaa hizo hivi sasa mimi binafsi nadiriki kusema hali nitofauti kwani bei za nafaka kama Mchele,Unga,Maharage na Sukari zimeshuka.
Bei za nafaka hizo zilipanda kwa kiasi kikubwa kilomoja ya mchele ilikuwa ni shilingi 2300-2500,Maharage Kg.sh 2,000,Unga Kg 1,000,sukari kg 2000-2500.Na itakumbukwa Sukari licha ya kupanda bei pia iliadimika sana na ikawa inasafirishwa nje ya nchi kwa magendo.
Kwa wiki moja sasa nikiwa nipo likizo ya kujiandaa na mitihani nimepata fursa ya kutembelea soko la Kawe,Buguruni na Tandale na kuona bei za bidhaa hizo zikiwa zimeshuka hali iliyosababisha nishikwe na butwaa na kulazimika wauzaji ni kitu gani kimesababisha washushe bei.
Ila muuzaji alitoa sababu yake wengine walisema serikali ililazimika kutumia mamlaka yake kimya kimya bila kufafanua kwa kuwataka wauzaji wakubwa wa bidhaa hizo washushe bei na wasafirishwe kwa wingi bidhaa hizo ili zipatikane kwa wahitaji tena kwa wakati na wengine.
Kwanza kabisa napongeza hatua zote za wazi na za siri zilizochukuliwa ama na serikali,wauzaji wa kubwa wa bidhaa hizo hadi leo hii bei za nafaka hizo zimeshuka.
Leo nii mchele kilo moja unauzwa kuanzia Sh 1,400-1,500,1,600 hadi 1,800.Sembe Sh 900,800 na maharage sh 1,500,Sukari sh 2,000.
Hakika ili ni jambo jema sana kama bei ya bidhaa inapanda kwa ghafla na kisha wafanyabiashara hao hao wanakubali kushusha bei ya bidhaa hizo hizo.
Hakuna haja ya kufichana ilifika mahala kupika wali katika baadhi ya familia ilikuwa ikionekana ni anasana na familia hiyo ilihesabika kuwa ina uwezo wa kifedha.
Kwa uhalisia huo hapo juu leo nataka kuwaasa wanahabari wenzangu,wananchi na wale wanasiasa ambao kila kukicha wamekuwa wakipigia kelele kuhusu gharama za vyakula kupanda na kushutumu serikali,wabadilike na wawe na tabia ya kukosoa mambo fulani wanayoyaona ni vikwazo kwa taifa na pindi mambo hayo yatakapopatiwa ufumbuzi iwe na serikali au taasisi yoyote ya kirahia pia wawe wanajitokeza kupongeza.
Bei za vyakula zimeshuka sisi tuliokuwa mstari wa kwanza kupigia kelele bei zishuke na leo kweli bei hizo zimeshuke, basi tusiogope tena kurudi uwanjani na kuwapongeza wale wote waliosababisha bei hizo zikashuka na huo ndiyo utakuwa uzalendo wa kweli na kuwatia moyo wale wote waliosababisha bei zishuke ili sikunyingine taifa likijakukumbwa na kadhia hiyo waweze kulitatua haraka jambo hilo.
Ndiyo maana leo nimeanza makala yangu kwa kunukuu maneno yale ya wahenga yasemayo ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni’.
Hivyo ni kweli wananchi tuna haki na tulikuwa na haki ya kuibana serikali kuhusu upandwaji wa bei za bidhaa na leo hii bidhaa hizo zimeshuka bei,hivyo hatuna budi kuipongeza serikali na wafanyabishara wote walioshusha bei nafaka hizo hadi leo hii tunaenda masokoni kifua mbele tena bila woga.
Maana zile bei za awali zilikuwa zikitutisha na kutusikitisha mno na kutukatisha tamaa ya maisha.
Kwani itakumbukwa kuwa kipindi kile cha uhaba wa sukari na bei ya sukari na kwa kuwa Shida ni mwalimu sisi maskini tulilazimika kuwa tunakwenda kununua tena kwa kuviziwa sukari katika maduka ya Shoprite ,maana katika maduka hayo sukari ilikuwa ikuuzwa bei rahisi na maduka hayo yaliweka kiwango cha ununuaji wa sukari ,kwani walimtaka kila mnunuaji anununue sukari sichini ya Kilo tatu ambapo kilo moja ilikuwa ikiizwa kwa shilingi 1,900.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika
0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Agosti 21 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment