KESI YA CHE MUNDUGWAO YAZIDI KUSOMBA WASHITKIWA
Na Happiness Katabazi
WAKAZI wawili wa Dar es Salaam,jana
walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili
ya hapo baadae kuja kuunganishwa katika kesi ya wizi wa Paspoti 26
inayomkabili Msainii wa Muziki wa asili, Chingwele Che Mundugwao na wenzake
wanne.
Wakili wa serikali Aidah Kisumo mbele Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa hao walifikishwa jana kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa yanayofanana ambayo yanamkabili Chemundugwao na wenzake ni Rajab Momba na Haji Mshamu.
Akiwasomea mashitaka Momba na Mshamu, Wakili Kisumo alidai kuwa tarehe isiyofahamika washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa. Aidha tarehe tofauti Dar es Salaam, Momba aliiba hati ya kusafiria yenye namba AB 651926 mali ya serikali.
Alidai Momba, Mshamu na Iqbal wanadaiwa tarehe isiyofahamika Dar es Salaam, walighushi hati ya kusafiria yenye namba hiyo, kuonesha ni halali na imetolewa na Idara ya Uhamiaji ya Tanzania jambo ambalo si kweli.
Mbali na Che mundugwao washitakiwa
hao wataunganishwa na Raia wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa
Ugavi wa Idara ya Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na mfanyabiashara Ally Jabir.
Hata hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka na kurudishwa rumande
kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana
washitakiwa hao wawili kama alivyofanya kwa kina Chemunduwao na wenzake na
kwamba upelelezi bado haujakamilika na
kesi itatajwa tena Julai 22, mwaka huu, ili waunganishwe na Chemundugwao ambapo
kesi yao nayo imepangwa kuja kutajwa Julai 22 mwaka huu.
Juni 3 mwaka huu, Chemundugwao na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26, ambapo hata hivyo DPP aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo hadi sasa wapo gerezani.
Juni 3 mwaka huu, Chemundugwao na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26, ambapo hata hivyo DPP aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo hadi sasa wapo gerezani.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Julai 19 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment