OFISA JKT KORTINI TENA KWA PEMBE ZA NDOVU
Na Happiness
Katabazi
OFISA
uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)
Suleiman Isanzu Chesana na anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya Tembo
yenye thamani ya Sh.bilioni nne, jana tena kwa mara nyingine amefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na kesi nyingine ya kukutwa na meno ya teambo Kg.781 yenye
thamani ya Sh.bilioni 9.3.
Mbele ya
Hakimu Sundi Fimbo, wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka alidai kosa la kwanza ni la
kujishughulisha na nyara hizo za
serikali bila kibali kinyume na sheria ya uhujumu uchumi na kwamba Mei 23 mwaka
huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara
hizo za serikali zenye thamani ya
Sh.bilioni 9.3 zikiwa zimefichwa katika
mifuko ya sementi wakidai wanasafirisha cementi na kwamba
upelelezi bado haujakamilika.
Hata hivyo
Hakimu Fimbo alimtaka mshitkiwa asijibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba ni Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka
ya kusikiliza na akaiarisha kesi hiyo hadi
Julai 20 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kuamuru
mshitakiwa arejeshwe gerezani.
Julai 9
mwaka huu, mshitakiwa huyo, alifikishwa mahakamani hapo kwa hakimu mkazi Nyigulile
Mwaseba akikabiliwa na kesi ya kukutwa
na meno ya tembo yenye thamani ya Sh.bilioni nne, ambapo pia hakimu Mwaseba siku hiyo
alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na akaamuru
apelekwe gerezani.
Wakati huo
huo , Ramadhan Shabani na Pendo Msaki waliokamatwa na askari wa kikosi cha
Kupambana na kuzuia dawa za kulevya katika Uwanja wa Mwalimu Julias Nyerere mwishoni mwa wiki, jana walifikishwa
mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa
ya kula njama na kusafirisha dawa za kuleya zenye uzito wa gramu
833.51 zenye thamani ya Sh 82,732,950 .
Katika kosa
la pili linalomkabili Pendo peke yake
ni la kusafirisha dawa za kulevya nakwamba Julai 6 mwaka huu, katika uwanja wa
mwalimu Nyerere alikamatwa gramu
500.08 aina ya Heroine zenye thamani ya
sh67,536,000. Upelelezi bado na hakimu akaamuru waende gerezani hadi Julai 24 mwaka huu, kwaajili ya kutajwa na
akasema mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Julai 12 mwaka 2013.
1 comment:
This is awesome!
Post a Comment