WANNNE WAONGEZWA KESI YA CHE MUNDUGWAO
Na Happiness
Katabazi
HATIMAYE
Wahudumu wa wawili wa Idara ya Uhamiaji jana walifikishwa kalifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, nakuunganishwa katika kesi ya
wizi wa Paspoti 26 inayomkabili Mwanamuziki wa muziki wa Asili nchini, Chingwele
Che Mundugwao na wenzake ambapo hadi
kufikia jana kesi hiyo imefanya kuwa na jumla ya washitakiwa tisa akiwemo raia
mmoja wa Uingereza.
Wakili
wa Serikali Lasdsalaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo
alidai
kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kujatwa lakini,pia upande wa jamhuri
imekusudia kufanya mabadiliko ya hati ya mashitaka ambapo jana imeweza
kuwaunganisha washitakiwa wawili wapya ambao ni wahudumu wa Idara ya uhamiaji
Adam Athuman na Abdallah Salehe na washitakiwa
wengine wawili ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 18
mwaka huu ambao ni Rajab Momba na Haji
Mshamu katika kesi hiyo ya Che Mundugwao ambao inawashitakiwa watano na hivyo
kufanya sasa kuwa na jumla ya washitakiwa tisa.
Washitakiwa wengine ni Che
Mundugwao, Raia
wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa Ugavi wa Idara ya
Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi cha Zimamoto
na Uokoaji na mfanyabiashara Ally Jabir.
Hata
hivyo washitakiwa hao walikanusha mashitaka hayo na kudai kuwa upelelezi bado
haujakamilika na hivyo hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo hadi Agosti 5 mwaka
huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru washitakiwa hao warejeshwe
rumande kwasababu bado Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi
hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana mahakamani.
Akiwasomea
mashitaka wakili Komanya alidai kuwa tarehe isiyofahamika washitakiwa walikula
njama ya kutenda kosa. Aidha tarehe tofauti Dar es Salaam, Momba aliiba hati ya
kusafiria yenye namba AB 651926 mali ya serikali.
Alidai washitakiwa hao wa nne na wanadaiwa tarehe isiyofahamika Dar es Salaam, walighushi hati ya kusafiria yenye namba hiyo, kuonesha ni halali na imetolewa na Idara ya Uhamiaji ya Tanzania jambo ambalo si kweli.
Juni 3 mwaka huu, Chemundugwao na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26, ambapo hata hivyo DPP aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo hadi sasa wapo gerezani.
No comments:
Post a Comment