WAKO WAPI WALIOKUWA WAKIPINGA GESI ISIJE DSM?
Na Happiness Katabazi
MEI 26 mwaka huu, niliandika makala
iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Heko JWTZ,Polisi kudhitibi vurugu
Mtwara’.
Makala hiyo niliitundika kwenye ukurasa
wangu wa facebook; happy katabazi .Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Baadhi ya watu waliyosoma makala
hiyo na kuitafsiri wao wanavyojua wao badala ya kujadili kile nilichokuwa
nimekiandika mimi, walidiriki kunitolea maneno ya kashfa na wakaitimisha
kuwaita baadhi ya wakazi wa Mtwara ambao
walikuwa wakifanya vurugu kwa kisingizio cha kukataa bomba la gesi lisije Dar
es Salaam, kuwa ni mashujaa na kwamba wananchi wa mikoa mingine wanastahili
kuwaunga mkono.
Kwa takribani miezi mitatu sasa
hatujasikia tena wale baadhi ya Wananchi
wa Mtwara na Lindi wakifanya vurugu tena kwa kisingizio cha kuzuia gesi isije
Dar es Salaam, wakati wakijua hawana mamlaka ya kuzuia.
Sote tunafahamu madhara yaliyotokana
na vurugu zile za kihistoria zilizofanywa na baadhi ya wakazi wa Mtwara ambao
ni dhahiri sasa wamelamba matapishi yao na wameudhiirishia umma kuwa hawawezi
kupambana na dola, hawana msimamo, ni waoga , wanaogopa vipigo na kufunguliwa kesi za jinai na kushi
gerezani.
Kwani kipindi kile wanaanzisha
maandamano na kusambanza vipeperushi walikuwa wakijitapa kuwa hawaogopi nguvu
ya dola, vipigo na wapo tayari kufa kwaajili ya kuakikisha bomba la gesi
haliletwi Dar es Salaam.
Tuwaulize wananchi wale leo hii mbona
hatuwasikii tena adharani wakisimamia maneno yao ya kwamba hawaliogopi dola,
kufunguliwa kesi, vipigimo ,kuwekwa gerezani?
Mbona yale maandamano yao yaliyokuwa
yakichagizwa kwa matumizi ya silaha za
jadi, kupambana na polisi na kusambaza vipeperushi, mbona hatuyaoni
tena?Kulikoni?.Mlijiita nyie ni mashushajaa sasa iweje leo hii mmetembezewa
vipigo na watu ambao mimi binafsi si wezi kudiriki kuwa ni askari wa JWTZ kwani
sina ushahidi na hilo na uongozi wa JWTZ umekanusha taarifa hizo, msalimu amri?
Hivi shujaa gani anasalimu amri kwa
kuogopa kipigo?Shujaa haogopi kipigo.risasi wa virungu.Shujaa anapambana hadi
tone la mwisho.Sasa mimi leo nasema wale wahuni waliokuwa wanafanya vurugu
Mtwara kwa kisingizio cha gesi siyo mashujaa kama walivyojiita ,minawafananisha
na ‘barafu’ kwani barafu linayeyuka.Na wananchi hao wameyeyuka haraka.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa
ambazo zimekanushwa vikali na Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ), kuwa askari
wake ndiyo wamemwagwa Mtwara na Lindi na kwamba wanajeshi hao wamekuwa
wakikamata raia wasiyo na hatia kuwapeleka kwenye Kambi ya Naliendele na
Majimaji na kuanza kuwapiga,kuwabaka na kuwalawiti baadhi ya
wananchi hao ambao wanapinga bomba la gesi lisiunganishwe kutoka Mtwara kuja Dar
es Salaam.
Binafsi navieheshimu sana vyombo
vyetu vya dola ikiwemo JWTZ kwani nafahamu mchango wake katika nchini yetu,
hivyo kwakuwa limekanusha taarifa za wanajeshi wake kuhusika na vitendoi hivyo,
name basi sina budi kuungana na jeshi hilo kupinga taarifa hizo ambazo kwanza
hakuna mwananchi yoyote aliyebakwa amejitokeza adharani au kwenda kuripoti kituo chochote cha
polisi na akalitaja jina lake na akatoa
na ushahidi kuwa amebwaka au kupigwa na JWTZ.
Tunachokiona na baadhi ya vyombo vya
habari kuandika taarifa hizo, ambazo kisheria haziwezi kutumika kuwafungulia
kesi za ubakaji au shambulio la kudhuru mwili hao wanaodaiwa kuwa ni askari wa
JWTZ kwa majina yao binafsi na siyo
jeshi kama taasisi kubaka watu.
Katika makala yangu ile ya Mei 26
mwaka huu, nilisema wazi kuwa kuna msemo usemao ‘Vita haina macho’. Nilitumia
msemo huo kwasababu nilijua mwisho wa siku kuna baadhi ya watu au vyombo vya
dola ipo siku vitachoshwa na uhuni ule unaofanywa na wananchi wale na wataanza
kuwachukulia hatua na wakati wakichukua hatua, yeyote atakayekuwa karibu na
wale wanaoshukiwa kufanya vurugu zile.
Na kweli tumesikia kupitia vyombo
vya habari vikiripiti kuwa watu wanaodaiwa ni wanausalama ambao wanaendesha
opareshini maalum ya kuwashikisha adabu
wale wananchi wakarofi wanaopinga gesi isije Dar es Salaam, wakiwapiga na
kuwajeruhi watu wasiyokuwa na hatia.
Kama taarifa hiyo ni ya kweli, basi
hapo maana msemo wa ‘Vita haina macho’ unapotimia, kwani hao wanaodai leo
wamepigwa na hao wanaodai kuwa ni wanausalama bila kosa, tuwaulize wao kama
Watanzania na wakazi wa mikoa hiyo, kabla na baada ya vurugu zile waliisaidie
nchi kwa kuakikisha wanatoa maoni yao ya kupinga vurugu zinazofanywa na wenzao
kwa kisingizo cha bomba la gesi?
Au ndiyo vyombo vya habari vilikuwa
vinaminya maoni ya wale wote waliokuwa wanapinga vitendo vya kihuni vilivyokuwa
vikifanywa na wananchi wenzao walikuwa wakitumia njia za kihuni kupinga bomba
za gesi lisije Dar es Salaam?
Au ndiyo tuseme sasa kwa kitendo
hicho ndiyo kinawafanya wanahabari wa Mtwara hivi sasa kuishi kwa mashaka kwa
kuhofia kupigwa na hao wanaodaiwa kuwa ni wanausalama na hao kundi la wananchi
ambalo linapingana na agizo la serikali la kutaka gesi isiletwe Dar es Salaam?
Niitimishe kwa kusema kuwa Tanzania
ni yetu sote, nishati yoyote inayopatikana ndani ya ardhi hii itatumika
kwaajili ya watanzania wote na kwamba nyie wananchi mliokuwa mnapinga gesi
isije Dar es Salaam, mlikuwa hamna mamlaka hayo, bali mlikuwa mnafanya uhuni tu
ambao mwisho wa siku mmejikuta mkiangukia kwenye mikono ya dola, kwa kupigwa,
kufunguliwa kesi na kuishia kusota gerezani na makazi yenu kuaribiwa na kuishi
kwa wasiwasi kama ‘mnaoga Barazani’ kwa kuhofia vigipo kutoka kwa watu mnaodai
ni wanausalama wa JWTZ wakati uongozi wa JWTZ umekanusha taarifa hizo na kusema
kuwa jeshi hilo halijatoa maelekezo kwa wanajeshi wake kupiga raia.
Wanasiasa uchwara na makundi mengine yaliyokuwa yanawajaza
ujinga ujinga huo wa kutumia njia za
kihuni na vurugu kupinga bomba la gesi lisiletwe Dar es Salaam, leo hii wamewasaliti, hawapo
nanyi tena, mahakamani mnakwenda peke yenu, wao wamelala majumbani kwao na wake
zao na watoto zao raha mustarehe.
Ndiyo kwanza serikali ipo katika
hatua za mwisho za kuakisha bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam,
linajengwa na nyie mkiendelea kushuhudia huku mkiwa mmefyata mkia.
Kama kweli nyie mlikuwa ni mashujaa
na wapingaji wa hilo mlilokuwa mnalipinga kwa moyo safi, si hadi leo
mngeendelea kusimamia kile mlichokuwa mkikiamini, na mngeakikisha bomba hilo
halijengwi msingetishika na vitisho, vipigo lakini kwakuwa nyie mlikuwa ni
bendera fuata upepo na mnatumika vibaya, mmesalimu amri?.
Wahenga walisema ‘akili ni nyeweli
kila mtu anazake’.Hivyo wananchi tusikubali kutumiwa vibaya na wanasiasa
uchwara wanaotafuta umaarufu au kukamata dola kwa njia za kuamasisha
maandamano, migomo haramu na vurugu,lugha za kukashifiana na kuzuliana uongo.
Kwani mwisho wa siku ni sisi ambo tumekubali
kutekeleza upuuzi huo wa wanasiasa ndiyo tunakuja kupata madhara ya moja kwa
moja ya kuangukiwa na mkono wa dola.Na wakati tunashughulikiwa na mkono wa dola
wanasiasa uchwara wale waliotushawishi kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria,
wanatuacha solemba.
Tutambue sheria za nchi zipo na
zinawashughulikia wale wote wanaozivunja, na kuna watu ambao wamepewa madaraka
ya kuruhusu au kutoruhusu jambo fulani lifanyike au lisifanyike kwa niaba yetu.
Nawapongeza askari wanaodaiwa na
baadhi ya wakazi wa Mtwara kuwa ni wa JWTZ kuwa wamekuwa wakiwapiga na kuwatesa
wananchi wale kwa lengo la kuakikisha wananchi hao wanaachana na habari ya
kupinga gesi isiletwe Dar es Salaam.
Kwani askari hao ambao mimi
sijawaona na ninarudia kuwa sina uhakika kuwa ni wa JWTZ , wameweza kusaidia
kutokomeza vitendo vya uvunjifu wa sheria vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya
wananchi wa Mtwara.
Kwani uenda bila kundi hilo la
askari wanaodaiwa kuwa ni wa JWTZ wasingeingia mitaani na kuwaadhibu wananchi
hao, uenda wananchi wale wangeendelea na kelele na na vitendo vyao vya uvunjifu
wa sheria kwa kisingizio cha gesi hali ambayo ingesababisha hali ya uchumi,
usalama huko Mtwara kudorora.
Mwisho napongeza vyombo vyote vya
ulinzi na usalama kwa kuweza kudhibiti vurugu za wahuni wale waliokuwa na
kisingizio cha kukaidi gesi isiletwe Dar es Salaam, kwani zilikuwa zinalitia
doa taifa letu kwenye sura ya dunia.
Kwani ni wazi sasa nilichojifunza
mimi hapa nchini hasa katika utawala wa serikali ya awamu ya nne inayoongozwa
na Rais Jakaya Kikwete, wananchi wengi wanapenda sana kuongea, kuhukumu, bila
kwanza kuwa na ushahidi na maelezo ya kutosha kuhusu jambo wanalolijadili na
matokeo yake sehemu kubwa ya jamii yetu imekuwa ikiamini habari na taarifa hizo
hata kama habari hizo zilitangazwa na vyombo vya habari kwa nia ovu ya ama
kumchafua mtu, kundi au chama fulani kwa makusudi na kwa uongo na pindi dola
linapoamua kutumia mamlaka yake wananchi wanafyata mkia.
Sasa tunapenda sana kuvunja sheria
za nchi lakini pindi tunaposhughulikiwa na dola ndipo akili zinatukaa sawa, na
tunakuwa na adabu. Sasa wale wakazi wa Mtwara waliokuwa wanafanya vurugu
walikuwa hawajatiwa adabu, sasa wametiwa adabu kwa kufikishwa mahakamani.
Na hilo kundi linalodaiwa ni la
askari wa JWTZ kutembezea kipigo ndiyo limesaidia sana kuwatia dabu wahuni wale
na ndiyo maana hadi leo huko Mtwara
tunaelezwa hakuna watu kukaa vikundi vikundi, wala kuzungumzia masuala ya gesi
inatoka au haitoki,watu wanafanyakazi za kujenga uchumi wanchi.
Na mkumbuke kuwa kifungu cha 21(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002, kinawapatia mamlaka polisi kutumia
nguvu kuwakamata wale wote wanavunja kwa makusudi sheria za nchi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki
Afrika.
Chanzo:Facebook;
happy katabazi ;
0716 -774494
Julai 19
mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment