POLISI KORTINI KWA PEMBE ZA NDOVU
Na Happiness
Katabazi
ALIYEKUWA
askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba
EX G5226 PC Ramadhani Selemani (27) wa Ukonga Polisi na wenzake jana
alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa
na kosa la kukutwa na pembe za ndovu zenye thamani ya Sh.21 mali ya serikali.
Wakili wa
Serikali Mwanaisha Kombo mbele ya Hakimu Mkazi
Nyigulila Mwaseba alimtaja mshitakiwa mwingine kuwa ni Hamis
Mwanga(22) mkazi wa Mbadala Zakhiem.
Wakili Kombo
alidai kuwa Julai 19 mwaka huu, washitakiwa hao walikamatwa wakiwa Pembe nne za Ndovu, na vipande 12 za pembe za
ndovu huko eneo la Tazara Dar es Salaam,
nyara zote hizo zikiwa na thamani ya Sh.Milioni 21 mali ya serikali na kwa
upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Hata hivyo
Hakimu Mwaseba aliwataka washitakiwa wasijibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza
kesi hiyo na hivyo akaiarisha kesi hiyo Agosti 7 mwaka huu kesi hiyo
itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru washitakiwa warejeshwe rumande.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Julai 25 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment