UPELELEZI KESI YA LWAKATARE BADO
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imearisha kesi
ya kula njama na kutaka kuumua kwa sumu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Mwananchi, Denis Msacky inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.
Hakimu MKazi Alocye alisema kwakuwa kesi hiyo jana ilikuja
kwaajili ya kutajwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Ponsia Lukosi amedai upelelezi
wa shauri hilo bado haujakamilika, mahakama yake inaiarisha kesi hiyo hadi
Julai 22 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Wakili wa Lwakatare, Nyaronyo Kichere ambaye alifika
mahakamani hapo na Lwakatare ambaye yupo
nje kwa dhamana, Ludovick yeye bado yupo gerezani kwasababu ameshindwa kutimiza
masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama hiyo Juni 11 mwaka huu, ambapo
Hakimu Katema alisema ili washitakiwa wapate dhamana ni lazima kila mshitakiwa
awe na wadhamini wawili
wanaotoka taasisi zinazotambulika kisheria ambapo kila mdhamini atatakiwa asaini bondi y a sh.milioni
10 pamoja na washitakiwa wenyewe,washtakiwa hao kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani na
kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha
mahakama. Lakini hadi jana Ludovick ameshindwa kutimiza masharti hayo nab ado anaendelea
kusota gerezani.
Machi 18
mwaka huu, ilidaiwa na wakili wa serikali Mkuu Lukosi kuwa washitakiwa
walitenda kosa hilo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Julai 9 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment