Header Ads

ALIYEMUIBIA RAIS MWINYI JELA MIAKA MITATU


Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Dar es Salaam, imemuhukumu  adhabu ya kifungo  cha jumla ya miaka  jela  , Abdallah Mzombe (39) baada ya kumkuta na hatia ya makosa ya wizi sh. Milioni 37.4 mali ya rais Mstaafu Alli Hassan Mwinyi Sh 37.4 milioni.

Mbali na adhabu hiyo hiyo pia Hakimu Mkazi Genivistus Dudu amemwamuru Mzombe kwa kutumia kifungu cha  348  cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,kumrejeshea Mwinyi kiasi hicho cha fedha ambazo alituhumiwa kumuibia.
Hukumu hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa na kwa  amu na wafuatiliaji wa kesi zinazofunguliwa katika mahakama nchini, ilitolewa jana hakimu Dudu ambaye alisema ili kuthibitisha kesi yao upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwalishwa na wakili wa serikali Charles  Anindo uliweza kuleta jumla ya mashahidi saba,akiwemo rais Mwinyi mwenye,Katibu Muhtasi wake na wapangaji wa nyumba tatu za Mwinyi, lakini itakumbukwa kuwa siku Mwinyi alipokuja kutoa ushahidi mahakamani hapo,wanausalama waliwazua waandishi wa habari kuingia ndani ya mahakama kumshuhudia Mwinyi akitoa ushahidi wake.

Akiuchambua ushahidi uliotolewa na rais Mwinyi, hakimu Dudu alisema Mwinyi alisema alikuwa rafiki wa familia ya ya Babu wa mshtakiwa (Abdalah), marehemu Seleman Mzombe.

Rais Mwinyi katika ushahidi wake alidai kuwa alimfahamu Abdallah  akiwa dalali  hivyo alimuamini na kumpa kazi zake mbalimbali ikiwemo kazi ya kumtafutia  nyumba  namba 481 iliyopo  Mikocheni  na nyumba namba 55 ya Msasani Village na  kumkabidhi fedha za  kufanyia manunuzi ya nyumba hizo.
Alidai kuwa baada ya kununuliwa kwa nyumba hizo, rais Mwinyi na Mzombe walikubaliana kuzipangisha na kwamba fedha zitakazopatikana zitumike  kufanyia matengenezo  ya na ukarabati wa nyumba hizo na kwamba kiasi kitakachosalia apelekewe   Mwinyi.

Mwinyi alieleza kuwa  nyumba ya Mikocheni ilikuwa na wapangaji wanne na nyumba ya Msasani Village ilikuwa na mpangaji mmoja na aliionyesha mahakama mikataba iliyokuwa imesainiwa baina ya wapangaji hao na Mzombe.

Hata hivyo katika ushahidi huo, rais Mwinyi alidai kuwa tangu Mzombe anunue nyumba hizo na kuzipangisha yeye hakuwahi kupelekewa hata Shilingi moja ila anaamini ama mshtakiwa huyo amezihifadhi ama ameziiba na kujinufaisha nazo.

Rais Mwinyi aliimbia mahakama kuwa wakati nyumba hizo zikifanyiwa matengenezo , mbali na fedha za kodi zilizokuwa zikikusanywa na Mzombe yeye pia aliwahi kutoa Sh 500, 000 kwa ajili ya matengenezo.

“Mzombe alikunyasanya jumla jumla ya Sh 37.4 milioni hata kama alitumia kufanya matengenezo kwenye nyumba hizo ,  kwenye matengenezo hayo haziwezi  kufikia Sh .milioni 17 , na binafsi ninaimani  ameziiba hivyo naomba sheria ichukue mkono w.”alidai rais Mwinyi.

Hakimu Dudu alisema chini ya Kifungu cha 231 cha kanuni ya adhabu, mahakama ikamuona mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu na kumtaka ajitetee, na alitaka kujitetea kwa njia ya kiapo na kwamba angeita mashahidi watatu ambao baadaye aliahirisha kuwaita.

Kulingana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili hakuna ubishi  kuwa rais Mwinyi  alikuwa na mahusiano  kama mtu na dalali wake na hakuna ubishi kuwa baada ya kupata nyumba walikubaliana kupangisha na Mzombe ndiyo aliyekuwa akikusanya kodi  za pango la nyumba hizo.

Aidha hakimu Dudu alisema hakuna ubishi kuwa   rais Mwinyi  alikuwa alimkabidhi Mzombe jukumu la  kufanya shughuli zote kwa kuaminiana na hakukuwepo na maandishi ya aina yoyote, lakini kitu ambacho  kinaubishi na kinahitaji kutatuliwa ni je ni kweli fedha hizo zilizokusanywa na mshtakiwa aliziiba?.

Alisema  kutokana na yote hayo, hapakuwepo na uhasama wowote kati yao walikuwa na mahusiano mazuri hivyo mahakama inaamini kuwa yaliyosemwa na rais Mwinyi ni ya kweli kuwa hakuwahi kupokea hata senti moja kutoka kwa mshtakiwa.

Katika utetezi wa mshtakiwa alidai kuwa kesi hii imetengenezwa ili kumfanya rais Mwinyi asiweze kutimiza ahadi yake, kwake ya kumjengea nyumba , ushahidi huu unatia mashaka  na una acha maswali mengi kwa sababu mshtakiwa hata siku moja hakuwahi kuileeleza  polisi wakati akichukuliwa maelezo, kumhoji rais Mwinyi wakati akitoa ushahidi wake wala kuiharifu mahakama awali.

“Yote haya  yanazidi kuuufanya utetezi wa mshtakiwa kuwa na matundu mengi na kwasababu hiyo mahakama inaona kuwa fedha  alizozikusanya mshtakiwa kama kodi  ya pango la nyumba hazijawahi kupelekwa kwa rais Mwinyi, aliiba mshtakiwa….hivyo mahakama hii inasema upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yake bila kuacha mashaka na hivyo mahakama hii inamuona mshtakiwa alitenda makosa yote mawili hivyo mahakama hii inamtia hatiani”alisema hakimu Dudu.

Wakili wa Serikali, Charles Anindo alidai kuwa upande wa mashtaka hauna kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya mshtakiwa huyo, ni kosaji wa mara ya kwanza  na kuiomba mahakama kuzingatia kifungu cha 348 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002  ambacho kinaipa mamlaka mahakama kuamuru mtu aliyeiba kurejesha kile alichokiiba kwa mlalamikaji.

Anindo alidai kuwa rais Mwinyi alikwenda mahakamani hapo kudai kile alichoibiwa  na kuiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.
Aidha kwa  upande wa mshtakiwa aliiomba mahakama isimpe adhabu kali  kwa sababu anafamilia  inayomtegemea wakiwamo wazee na watoto wadogo.

Hakimu Dudu alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela katika kosa la kwanza, na kifungo kingine cha miaka mitatu jela katika kosa la pili lakini vyote vitakwenda sambamba na kwa maana hiyo mshtakiwa huyo atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu gerezani kuanzia jana.
Mzombe alifikishwa katika Mahakam a hiyo kwa mara ya kwanza Agosti 21 mwaka jana,akidaiwa kuwa katika. siku tofauti kati ya Januari mosi na Julai 10, akiwa wakala wa kukusanya kodi kwenye nyumba za Mzee Mwinyi, aliiba Sh milioni 17.6.

Inadaiwa aliiba fedha hizo za kodi ya mwaka 2011/12 na 2012/13 alizokuwa amekusanya kutoka kwa mpangaji wa nyumba namba 481 ya Mikocheni.

Katika mashitaka mengine, Mzombe anadaiwa kuiba Sh milioni 19.8 za malipo ya kodi ya mwaka 2011/12 na 2012/13 ya mpangaji wa nyumba namba 55 ya Msasani Village.

 Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Februali 13 mwaka 2013 .


No comments:

Powered by Blogger.