SILAHA ZA JADI ZAPOKELEWA KAMA KIELEZO KESI YA SHEIKH PONDA
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,jana ilipokea mapanga, Jambia, mabango,vipaza
sauti,masufulia ,majenereta kama
kielelezo cha nane cha upande wa jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa
malighafi zenye thamani y a sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu ,Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.
Uamuzi wa
kuvipokea vielelezo hivyo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Victoria Nongwa baada kukubali
ombi la wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka na Zuberi Mkakatu lilokuwa
linaomba mahakama hiyo ipokee hati inayoonyesha idadi ya vitu hivyo iliyotolewa
na shahidi wa kumi wa upande wa jamhuri Inspekta Thobias Walelo (34) ,ipokelewe
kama kielelezo ambacho kinaonyesha vifaa hivyo vilivyokuwa vikitumiwa na
washitakiwa hao wakati walipokamatwa wakiwa wamevamia na kuishi isivyo halali
katika kiwanja cha Chang’ombe Markas ambacho ni mali ya kampuni ya Agritanza
Ltd na siyo mali ya waislamu kama wanavyodai washitakiwa na kutupilia mbali
pingamizi la wakili wa utetezi Juma Nassor lilokuwa linaomba hati hiyo
isipokelewe.
Akitoa
ushahidi wake Inspekta Walelo ambaye ni Mpelelezi mkuu wa kesi hiyo, alieleza
kuwa alipokea jalada la kesi hiyo ilianze kulifanyiakazi ya upelelezi ambapo
lilikuwa likihusiana na kosa la kuingia kwa jinai katika kiwanja hicho Oktoba
13 mwaka jana aliindikia barua ofisi ya
ardhi katika Manispaa ya Temeke ilikutaka kufahamu nani hasa ni mmiliki halali
wa kiwanja cha Chang’mbe Markas na nilizipeleke mwenyewe.
Inspekta
Walelo alidai kuwa Oktoba 14 mwaka jana ,kwa kuwa yeye ndiye mpelelezi mkuu wa
kesi hiyo alienda hadi kwenye kiwanja hicho kupata uhakika na nilikuta umati wa
watu ambao ni washitakiwa na niliueleza umati ule kuwa sikuwa na nia mbaya
kwani nataka kupata ukweli wa nani hasa ni mmiliki wa kiwanja kile na ndipo
umati ule ukamteua mwenzao mmoja ambaye ni Sheikh Hussein Ismail ili aweze
kunipa majibu sahihi ambapo umati ule ulinijibu upo pale kwaajili ya kulikomboa
eneo lao wanaolimiliki kihalali na kwamba nyaraka za kuthibitisha hilo wanazo
na akamweleza Sheikh Hussein kuwa kuna mtu alifika kituo cha Polisi Chang’ombe
kulalamika kuwa hicho ni kiwanja chake na kwamba wao wamevamia na kwamba
akamtaka sheikh Hussein kesho yake afike kituoni waje kumpatia ukweli wa
mmiliki halali wa eneo hilo ni nani.
“Ilipofika
Oktoba 15 mwaka jana kweli Sheikh Ismail
na wenzake ambao Hamza Kambi, Sheikh Said Nyoni, Mkadamu Adhallah ambaye ni mshitakiwa wa tano na Mbaraka Daluweshi
na kweli walifika asubuhi na nilipowataka nianze kuwachukua maelezo yao
,masheikh hao wakasema hawapo tayari kuchukuliwa maelezo bila ya kuwepo wakili
wao na wakaniomba niwaruhusu waende kumleta wakili wao kisha watarudi naye
mchana ili ndiyo nianze kuwachukua maelezo:
“Niliizingatia
kauli mbinu ya Jeshi la Polisi inayosema Utii wa sheria bila
shuruti,niliwaruhusu waende kumleta wakili wao lakini cha kushangaza ilipofika
huo mchana hawakurudi tena nikaamua kuwapigia simu zao na kuwakumbusha kuwa
wanatakiwa warudi polisi wachukuliwe maelezo lakini walinijibu hawatarudi ng’o
na wakanitaka eti mimi nirekodi yale niliyoongea nao asubuhi”alidai Inspekta
Walelo na kusababisha watu kuangua vicheko.
Aidha
Inspekta Walelo alieleza kuwa Oktoba 15 mwaka jana, alipota majibu ya barua
yake yaliyokuwa yanayaka kufahamu nani ni mmiliki na manispaa ikamdhibitishia mmiliki
wa kiwanja kile ni kampuni ya Agritanza na ndipo akaamua kutoa taarifa kwa
viongozi wake wa juu ambao waliunda kikosi kazi ambapo usiku wa kuamkia Oktoba
17 mwaka jana, kikosi hicho ambapo yeye alikuwa miongoni mwao walifika eneo
hilo ambalo washitakiwa hao walikuwa wameingia kwa jinai na kuwakamata
washitakiwa wale ambao jumla yao walikuwa ni 50.
Aidha
alieleza kuwa baada ya kuwakamata washitakiwa hao wakiwa na majambia, visu,
vipaza sauti, viloba viwili vya unga wa sembe, mikeka,mabango, visu,sufulia
,ndoo za plastiki waliamua kuwabeba washtakiwa hao kwenye magari ya polisi kwa
awamu mbili na kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi Kijitonya ambapo
waliwafikisha saa 12 asubuhi na kuanza kuwahoji ambapo waliwahoji hadi Oktoba
18 mwaka jana , washitakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo
wakikabiliwa na kesi hiyo.
Kesi hiyo
iliyoanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Jumatatu wiki hii, inaendelea tena leo.
Chanzo:Gazeti la
Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 21 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment