SERIKALI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA PONDA
Na Happiness
Katabazi
HATIMAYE
upande wa jamhuri katika kesi ya uchochezi na kuiba malighafi zenye thamani ya
Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh
Pnda Issa Ponda na wenzake 48 , umetangaza rasmi kuifunga kesi yake.
Hayo
yalisemwa jana na Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka mbele ya Hakimu
Mkazi Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, muda
mfupi baada ya shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuru D/C F8586 Ismail wa kituo cha
Polisi Chang’ombe kumaliza kutoa ushahidi wake ambapo jana jumla ya mashahidi
watatu kwa mpigo walitoa ushahidi wao.
Wakili Kweka
alieleza kuwa hadi kufikia jana upande wa jamhuri ulikuwa umeleta mashahidi 17
na vielelezo 13 ambavyo vilipokelewa mahakamani kama vielelezo vimetosheleza
upande wa jamhuri kufikia uamuzi huo wa kuifunga kesi yao.
Baada ya wakili
Kweka kutoa maelezo hayo wakili wa Ponda, Juma Nassor aliomba mahakama iwapatie
muda hadi Machi 4 ili waweze kwenda kujiandaa na kufanya utafiti
utakaowawezesha kuwasilisha maombi ya kuwaona wateja wao wote 49 hawana kesi ya
kujibu.
Hata hivyo
Hakimu Nongwa alisema jukumu la kupanga tarehe ya kuja kufanya majumuisho ya
mawakili wa pande hizo mbili katika kesi hiyo ya kuwaona washitakiwa wanakesi
ya kujibu au la ni vyema ikaachiwa mahakama na hakimu huyo akatoa amri kuwa
majumuisho hayo yatafanyika kesho (Februali 27 mwaka huu),saa mbili asubuhi na kwamba na akautaka upande wa utetezi ndiyo
utakuwa wa kwanza kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo.
Kabla ya
Hakimu Nongwa jana saa nane mchana ya kukubali ombi la upande wa jamhuri la
kuifunga kesi yake, alisikiliza ushahidi wa mashahidi watatu wa waliokuwa
wameletwa na upande wa jamhuri ambao ni shahidi wa 15 ambaye ni F3929 D/C ,Constebo
Eliaeli (35) ,shahidi wa 16 ambaye ni Stationi Sajenti Amos wa kituo cha Polisi Kati na Shahidi wa
17 ambaye askari mpelelezi Na. F8586 D/C Ismail.
Kwa upande
wake shahidi wa 17, D/C Ismail aeleza mahakama kuwa Oktoba 17 mwaka jana,
alipewa kazi na Mkuu wake wa kazi na saa
2-9 alasiri alikuwa katika kituo cha Polisi Kijinyoma alipewa jukumu la
kuwahoji washitakiwa ambao walikamatwa katika kiwanja cha Chang’ombe Marskas wakikabiliwa na makosa ya kuingia kwa jinai
katika kiwanja hicho .
Ismail
alidai kuwa yeye alimhoji mshitakiwa aitwaye
Fiswaa ambaye alimweleza kuwa kati ya tarehe ,mwezi na saa isiyofahamika
akiwa nyumbani kwake Mlandazi Mkoani Pwani, akiwa anasikiliza Redio Iman,
alisikia tangazo lilokuwa likiwataka waumini wa dini ya Kiislamu kwenda
kuongeza nguvu ya kujenga msikiti katika kiwanja cha Chang’ombe Markas ambacho
ni mali ya waislamu na si Bakwata lakini kilikuwa kimevamiwa.
Shahidi huyo
alidai kuwa , mshitakiwa huyo alimweleza kuwa aliitikia wito huo na kufunga safari toka
nyumbani kwake Mlandizi na kwenda kuja hadi kwenye kiwanja hicho kilichopo Dar
es Salaam, na kuungana na wenzake ambapo kiongozi wao aliyekuwa akiwaongoza
walipokuwa kwenye kiwanja hicho ni mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Ponda.
“Sululu,mapanga
vilitumika kama vifaa vya kujengea msikiti wa muda katika kiwanja hicho na ndipo usiku wa kuamkia Oktoba 17 mwaka
jana, tukiwa tumekaa kwenye kiwanja hicho nikasikia sauti ikisema kuwa panda
kwenye gari ,panga kwenye gari na sikuwa na kumbukumbuku yoyote’alidai Ismail
kuelezwa na Fiswaa na maelezo ya mshitakiwa huyo yalipokelewa kama kilelezo cha
13 na hakikupingwa na mawakili wa utetezi.
Kwa upande
wake shahidi wake Shahidi wa 16, Station Sajenti Amos, alidai kuwa Oktoba 17
mwaka jana alipewa jukumu la kumhoji mshtakiwa Hussein Ally ambaye mshitakiwa huyo alimweleza kuwa
alipokea maelekezo kutoka kwa msheikh wake wa msikiti wa Kinyerezi yakimtaka
afike katika kiwanja cha Markas na alienda akakutana na wenzake ambapo walianza
kufanya usafi ili waweze kujenga msikiti
na walikuwa wakiongozwa na Ponda kufanya ujenzi na usafi katika kiwanja hicho
ambacho tayari mashahidi wengine toka Bakwata walishasema kiwanja hicho ni mali
ya kampuni ya Agritanza Ltd siyo Bakwata tena na maelezo ya mshitakiwa hayo
yalipokelewa kama kielelezo cha 12.
Aidha kwa
upande wake shahidi wa 15 , D/C Constebo Elieli
alidai kuwa Oktoba 17 mwaka jana , alipewa jukumu na mkubwa wake wa kazi
la kuandika maelezo ya mshitakiwa Mohamed Ramadhan ambaye alimweleza kuwa siku
hiyo yeye alikwenda kusali katika eneo la kiwanja hicho akitoa Oysterbay Dar es
Salaam.
Elieli
alieleza kuwa mshitakiwa huyo alimweleza kuwa alifikia uamuzi wa kwenda kusali
swala ya alfajiri hapo Chang’ombe markas kwasababu alikuwa anauguliwa na ndugu
yake anayeishi Keko ambapo yeye mshitakiwa hakutaka kwenda kusali misikito ya
Keko kwasababu hali ya usalama ili ni mbaya na hivyo akaamua kwenda kusali
katika eneo hilo la Markas.
“Mshitakiwa
huyo akanieleza eti baada ya kusali hapo alfajiri ya Oktoba 17 mwaka jana,
ndiyo ghafla alishitukia anakamatwa na mapolisi na kwamba yeye hakuwa.Na kwamba
nilipomhoji kama analifahamu vuguvugu la waislamu kudai haki zao, mshitakiwa
huyo alikubali kulifahamu vuguvugu hilo na kwamba yeye pale kwenye lile eneo
alipokamatiwa alikuwa katika kutetea na
kudai haki yao ya kurejeshewa kiwanja kile ambacho ni mali ya waislamu na si
Bakwata”alidai Elieli lakini hata hivyo mahakama ilikataa kuyapokea maelezo
hayo kama kielelezo kwasababu yana dosari nyingi za kisheria.
Awali Oktoba
18 mwaka jana, ilidaiwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na wakili Kweka
mbele ya Hakimu Nongwa kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano likiwemo
kosa la kula njama,wizi wa malighafi zenye thamani y ash.milioni 59 na
uchochezi ambalo linamkabili Ponda na mshitakiwa wa tano Mkadamu Swalehe ambao
wanaendelea kusota gerezani kwasababu Mkurugenzi wa Mashitaka,Dk.Eliezer
Feleshi bado hawajaondolea hati ya kuwafungia dhamana.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Februali 26 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment