MAHAKAMA YAMNG'ANG'ANIA MSHARIKA WA PONDA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa upande wa
utetezi
katika kesi ya uchochezi na
wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya
ya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Issa Ponda na wezake, lilokuwa linataka
mahakama hiyo isipokee kama kielelezo
maelezo ya ungamo yaliyotolewa na mshitakiwa
wa tano katika kesi hiyo Mkadamu Swaleh Abdallah,polisi kama kielelezo.
Uamuzi huo uliotokana na kesi
ndogo iliyofanyika jana asubuhi, ulitolewa na Hakimu Victoria Nongwa jana saa
nane mchana ambapo alisema mahakama yake jana asubuhi ilipata fursa ya
kuendesha kesi ndogo iliyoendeshwa jana asubuhi mahakamani hapo ambapo upande wa jamhuri unaowakiliwa na
wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka na Zuberi Mkakatu ili kuthibitisha
maelezo yale ungamo ya Mkadamu yalikuwa yamekidhi matakwa ya sheria walileta
mashahidi wawili ambao ni Sajenti Masikini ambaye alimkamata Mkadamu na Sajenti
Mkombozi Mhando ambaye ndiye aliyemchukua maelezo mshtakiwa huyo , ambao
walitoa ushahidi wao na upande wa utetezi ulileta shahidi mmoja ambaye ni
Mkadamu naye alitoa ushahidi wake mfupi.
Hakimu Nongwa akitoa umuzi
wake alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kulipokea ungamo hilo chini ya
kifungu cha 169 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 licha ni kweli ungamo hilo limevunja matakwa
ya kifungu cha 50(1)(a) kinachomtaka ofisa wa polisi amchukue maelezo
mshitakiwa ndani ya saa nne tangu alipokamatwa lakini Mkadamamu alichukuliwa
maelezo hayo masaaa manne yalikuwa yamepita na hivyo kufanya ongezeko la muda
la masaaa matatu.
“Licha mahakama hii
inakipokea kielelezo hiki ambacho kimeandaliwa nje ya muda wa sheria unavyotaka
lakini ieleweke kwamba kifungu cha 169 cha Sheria ya Makosa ya Jinai,
kinailazimisha mahakama kupokea kielelezo cha aina hiyo ambacho kimezidisha
muda kwani mahakama hii imeona kuongezeka kwa masaa matatu nje ya muda wa
sheria uanvyotaka hakukuweza kumshawishi mshitakiwa huyo kukiri makosa yake
ndani ya ungamo hilo ambalo amekiri kutenda makosa yanayomkabili likiwemo kosa
la kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang;’ombe Markas na kwamba anakipokea
ungamo hilo kama kielelezo’alisema hakimu Nongwa.
Kufanyika kwa kesi hiyo ndogo
kulitoka na pingamizi lilowasilishwa juzi na mawakili wa utetezi Juma
Nassor wakati shahidi wa nane wa upande
wa jamhuri Sajenti Mkombozi Mhando kuomba maelezo hayo ya onyo yapokelewe kama
kielelezo kwasababu yamekidhi matakwa ya kisheria na ndipo mawakili hao wa
utetezi walipinga kisipokelewe na ndipo mahakama juzi ikatoa amri ya jana
kuiendesha kesi ndogo ili kubaini ukweli kuhusu maelezo hayo ambapo ilikubali kuyapokea
kama kielelezo.
Baada ya uamuzi huo
kumalizika kutolewa saa 8:30 mchana, kesi kubwa ilianza kusikilizwa ambapo
shahidi wa tisa wa jamhuri Sajenti Juma alianza kutoa ushahidi wake na kudai
kuwa yeye ndiye mpelelezi wa kesi hiyo na kwamba alipewa jukumu la kwenda
kutembelea eneo la tukio la kiwanja cha Chang’ombe Marks na kushuhudia uharibu
mkubwa ulikuwa umefanywa na washtakiwa hao ambao wanadaiwa kuingia kwa jiani
katika eneo hilo na kujenga msikiti wa muda.Kesi hii inaendelea leo tena leo
kusikilizwa mfululizo.
Wakati huo huo , Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Kipolisi Mkoa wa Dar es
Salaam(ZDCO), Hemed Msangi ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya kula
njama na kufanya maandamano haramu inayowakabili Salum Bakar Makame na wenzake
53 jana alieleleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kati ya Februali 11-17
mwaka huu, yeye alikuwa ndiye Kamanda wa Kanda ya Maalum ya Dar es Salaam, na
kwamba Februali 11 alipokea barua toka
Shura ya Maimamu iliyokuwa ikimuomba kibari cha kufanya maandamano ya kwenda
ofisi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kumhoji ni kwanini hampatii dhamana Ponda na kwamba maandamano hayo walikuwa
wakitaka yafanyike Februali 15 baada ya swala ya Ijumaa na wataandamana kutokea
misikiti mbalimbali.
Kamishna Msaidizi huyo wa
Polisi, Msangi alidai yeye na maofisa
wenzake walitafakari hiyo barua ambayo
ilikuwa na saini ya Sheikh Juma Idd ambaye ni Amir wa Shura ya Maimamu Temeke na walijiuliza uzito wa maandamano
hayo na kwamba jeshi hilo walibaini kuwa hawakuwa na askari wa kutosha
wakuwapeleka kila msikiti kwaajili ya kuyalinda waandamanaji hao na hivyo uhaba
huo wa askari ungeweza kuleta usalama mdomo na pia walifikia uamuzi wa kuyakaza
maandamano yake kwasababu waliona ofisi ya DPP ipo katikati ya jiji na ina
sehemu finyu hivyo maandamano hayo yangeruhusiwa yangweza kuathiri haki za watu
wengine wanaotumia jengo hilo la ofisi ya DPP ambalo linatumiwa na maofisi
mengi na watembea kwa mguu.
“Pia jeshi la polisi
lilitazama kuwa kesi ya Ponda ipo mahakamani hivyo ingewaruhusu waandamanaji
hao kwenda mahakamani ni kama kuingia huru wa mahakama na kwamba jeshi lilipata taarifa toka kwa DPP
kuwa DDP alikuwa amepokea barua toka kwa Baraza la Wanazuoni iliyokuwa
ikimuomba wakazungumze naye na kwamba tayari DPP alishalikubalia baraza hilo kuwa
angekutana nao Februali 28 mwaka huu, ....kwasababu hiyo mimi niliwandikia
barua ya kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu hizo zilizozitaja hapo juu
kwani pia jeshi lilikuwa limepata taarifa za watu walikuwa wamepanga kufanya
vurugu katika maandamano hayo”alidai ZDCO-Msangi.
Aliendelea kueleza kuwa licha
ya kuwapelekea zuio hilo la maandamano kwa maandishi waombaji hao wa
maandamano, pia yeye aliutangazia umma kupitia vyombo vya habari kuwa jeshi la
polisi limezuia maandamano hayo lakini ilipofika Februali 15 washitakiwa hao
walikaidi amri hiyo ya jeshi polisi waliandamana wakiwa na mabango, mawe,na
silaha za jadi na mwishowe waliishiwa kukamatwa,kuhojiwa na kufikishwa
mahakamani.
Hata hivyo washtakiwa hao
ambao walifikishwa kwa mara ya kwanza juzi ,jana wakati Msangi akitoa ushahidi
wake walilazimika kumhoji maswali kwamba anauthibitisho gani kwamba wao ni
wafuasi wa Ponda na kwamba una ushahidi gani kama hao washitakiwa walikuwa
wameandamana siku hiyo lakini hata hivyo shahidi huyo na hakimu Sundi Fimbo
waliwataka washitakiwa hao wasubiri mashahidi waliowakamata siku wakija kutoa
ushahidi mahakamani ndiyo wawaulize maswali hayo kwani shahidi huyo Msangi siye
aliyewakamata na kesi hiyo imearishwa hadi leo ambapo shahidi wa pili anakuja
kuanza kutoa ushahidi na washitakiwa wote wamerudishwa gerezani kwasababu
dhamana zao zimefungwa na DPP na mahakamana.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la
Jumatano, Februali 20 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment