MAKONGORO NYERERE AUNGANISHWA KESI YA PAPA MSOFE
Na Happiness Katabazi
MFANYABISHARA mwingine na Mkazi
wa Pugu jijini Dar es Salaam, Makongoro Joseph Nyerere jana aliunganishwa kati
kesi ya mauji inayomkabili mfanyabishara maarufu jijini hapa Abubakar Marijan [50] maarufu kwa jijini
‘Papaa Msofe chuma cha Reli akishiki Kutu mutu ya Pakee’.
Nyerere alifikishwa katika viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na askari kanzu na kabla ya wakili wa serikali Charles
Anindo kuanza kumsomea mashtaka , wakili huyo aliomba ruhusa ya mahakama ili
aweze kubadilisha hati ya mashtaka, ya awali iliyokuwa ikimhusu mshtakiwa mmoja
tu Papa Msofe, ili mshtakiwa huyo Nyerere awe kuunganishwa katika kesi hiyo ya
mauji.
Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo
Agnes Mchome alikubaliana na ombi hilo la upande wa jamhuri , lakini akamtaka
mshtakiwa huyo kuwa haruhusiwi kujibu chochote baada ya kusomewa shitaka
linalomkabili kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na
kwamba ni mahakama kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Wakili Anindo akimsoma shtaka alidai kuwa
baada ya mahakama hiyo kukubali ombi lake la kuifanyia marekebisho hati hiyo ya
mashitaka ambayo awali ilikuwa ikisomeka ni ya mshitakiwa mmoja tu(Papa Msofe),
hivyo kuanzia jana kesi hiyo itasomeka kuwa inawakabiliwa washitakiwa wawili ambapo
mshitakiwa wa kwanza ni Papa Msofe na
Nyerere ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Pugu jijini Dar es Salaam.
Wakili Anindo alidai kuwa washtakiwa
wote kwa pamoja wanadaiwa kumua kwa makusudi
Onesphory Kituli, kinyume cha
kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyorekebishwa mwaka
2002 na kwamba kosa hilo walilitenda Oktoba 11 mwaka 2011, nyumbani kwa
marehemu huko Magomeni Mapipa jijini Dar
es Salaam na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka
hilo, Hakimu Mchome aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 20 mwaka
huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru Nyerere apelekwe gerezani kwasababu kosa analokabiliwa nalo yeye na
mwenzi Papa Msofe ambaye tayari yupo gerezani tangu Agosti 10 mwaka jana, halina
dhamana kwa mujibu wa sheria.
Agosti 10 mwaka jana , Papa Msofe
alipandishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza chini ya ulinzi mkali wa askari
polisi na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka mbele
ya Hakimu Mchome alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo la mauji
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 14 mwaka 2013.
1 comment:
Also viѕіt my wеblog payday loan,
My web site ; payday loans
Post a Comment