UDHAIFU HUU MAHAKAMA YA KISUTU HADI LINI?
Na Happiness
Katabazi
HII siyo
mara yangu ya kwanza kuandika makala zaidi ya nne sasa zinazoushauru mhimili wa
mahakama uanchane na ukirimba na mambo ya kizamani na badala yake ikubali
mabadiliko katika mambo kadhaa kutoka na wakati tuliopo.
Leo hii tena
nimelazimika kuandika makala hii ya kuinyoshea kidole mhimili wa mahakama ya
Tanzania ya kuiomba mhimili huo uamke katika usingi wa pono uliolala na uone
kuwa hivi sasa mhimili wa serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP),DK.Eliezer Feleshi kuanzia Oktoba 18 mwaka jana ,hadi
Februali 18 mwaka
huu, tayari umeishafungua zaidi ya tano za jina.
Ambapo kesi
hizo zinawakabili baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu ikiwemo kesi ya
uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.
Kesi hizo
zote chanzo chake ni tuhuma za kuchoma makanisa huko Mbagala mwaka jana, kufanya
maandamano haramu katika Wilaya ya Ilala.Na kesi zote hizo zimeanza kusikilizwa
tena kwa kasi ya ajabu na nitakuwa ni mnyimi wa fadhila kama sitapongeza jeshi
la polisi kwa kuarakisha upelelezi na mahakama kwa kuanza kusikiliza tena kesi
ya Ponda na kesi nyingine inayowakabili wafuasi wake 54 walioandamana Ijumaa
iliyopita zimeanza kusikilizwa mfululizo na kwa kasi ya ajabu.
Kwa sisi
waandishi wa habari za mahakamani ni mashahidi wa hilo, ila kikubwa
kinachotukera na hatua ya mhimili wa mahakama kushindwa kusoma harama za
nyakati kwa ama kutoa fedha za dharula katika bajeti yake kwenda kununua hata
feni nne tu kufunga katika kumbi mbili za mahakama hiyo zinazotumika kuendeshea
kesi ya Ponda ina jumla ya washtakiwa 49, kesi ya wafuasi wa Ponda inajumla ya
washtakiwa 54.
Si hilo
,mhimili huo umeshindwa kubaini kuwa mashahidi wanaotoa ushahidi hawasikiki
vizuri kwa watu wanaofuatilia kesi hiyo na saa nyingine hata mahakimu
wanaosikiliza kesi hiyo wamekuwa wakilazimika kuwataka mashahidi hao watoe
sauti ya juu ili waweze kuwasikia, lakini mahakama imeshindwa kuleta vipaza
sauti katika uendeshwaji wa kesi hizo ambazo zinafuatiliwa kwa karibu na umma.
Tunashangazwa
na kukerwa na hali Novemba 2008 kesi nane za wizi katika Akaunti ya EPA,
zilipofunguliwa na kaunza kusikilizwa, ni mahakama hii ililalazimika kwenda
Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara na kuwachukua wale wataalamu waliokuwa
wanakuja wakati kesi hizo zikisikilizwa wakiwa na Kompyuta na Vipaza sauti
ambavyo vilikuwa vikirekedi mwenendo mzima wa kesi hizo kwa njia ya
Elektonicki.
Kesi moja ya
EPA ilikuwa ikiwakabili washtakiwa wawili, watatu hadi wa tano, sasa ajabu ni
kwamba kesi hizi ambazo chanzo chake kinaelezwa ni chokochoko za udini hapa
nchini, mhimili huu wa mahakama unashindwa kuleta vipaza sauti hivyo?
Hivi uongozi
wa Mahakama ya Kisutu chini ya Hakimu Mkazi Elvin Mugeta, mlikuwa na uharaka
gani wa kung’oa zile feni ambazo zilifungwa baada ya vyombo vya habari kupiga makelele
wakati kesi za EPA zilipofunguliwa ndipo tukaona mahakama imenunua feni zile na
kuzifunga,wakati kumbe bado hamjapata feni mpya za kuzifunga na na ukarabati
bado haujamalizika ambapo hivi sasa ukarabati wa mahakama ya Kisutu unaonekana
ni wakusuasua.
Nawala hizi
si za uongozi wa Mahakama ya Kisutu, lawama hizi ziuendee uongozo wa mhimili wa
mahakama nchini, ambao unafahama fika kesi hizo ambazo zinapewa uzito wa
kipekee na mahakama yenyewe na serikali lakini inashindwa hata kuandaa
mazingira mazuri ya waandishi wa habari, wanausalama wanaofika mahakamani hapo
kwaajili ya kuudhulia kesi hiyo?
Tunafahamu
kuwa mhimili huu umekuwa bingwa wa kulalamika kuwa haina fedha za kutosha,
lakini mbona siku ya Law Day sherehe hizo
zinafana kwa kula na kunywa vitafuno, na fedha za ukarabati na kuweka samani
katika baadhi ya ofisi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zinatakowapi?
Hivi
kulikuwa na ulazima gani wa ukaratabi wa mahakama ya Kisutu kuanzia nje kwa
kujenga fensi, choo,kupaka rangi baadhi ya ofisi za mahakimu wakati mahakama za
wazi zote tatu zikiwa hadi hivi sasa hazijaanza kukarabatiwa wakati mahakama
hizo hasa ndiyo zinazotumiwa kuendeshea kesi?
Mbona
mahakama za wazi za mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Disheni
ya Kazi, Kitengo cha Biashara na Mahakama ya Rufaa mbona zina feni na AC? Kwani
hii Mahakama za wazi za Mahakama ya Kisutu zimekosa nini?Au ni kwasasabu
wanaondesha kesi zile ni Mahakimu na siyo Majaji?
Jaji Mkuu
Mohamed Chande Othman ni mwanasheria ambaye amepata fursa ya kufanyakazi ya
Kisheria katika nyanja za kimataifa, atatunamuomba yale mazuri aliyokuwa
akiyaona ule nje ya nchi ayalete kwenye mahakama zetu na kuhusu hali hii ya
mahakama za wazi za Kisutu kuwa ni kama maghofu tunaomba aingilie kati mara moja na
kama fedha za ukarabati zimeisha basi aende serikalini akaombe fedha ukarabati
uendelee ili wananchi wanaofika mahakamani hapo waweze kuketi sehemu nzuri na
paendane na mahali panapoheshimiwa na wananchi kuwa ni mahali pakutolea haki.
Kwani hivi
sasa baadhi ya kordo za mahakama hiyo na vyumba viwili vya wazi vya mahakama
hiyo vilivyopo chini vimegeuka kuwa stoo ya kutunzia mambao yaliyoalibika
ambayo yamejaza mavumbi makali,kuna uhaba wa mabenchi wa watu kukalia. Naimba
mhimili wa mahakama uzinduke usingizini na uchukue hatua za dharula za
kuboresha mahakama hizo za wazi.
Mungu ibariki
Tanzania, Mungu ibariki Afrika
0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 21 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment