Header Ads

HAKIMU KESI YA KIBANDA ACHARUKA




Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkaz Kisutu Dar es Salaam, jana iliucharukia upande wa kesi kuandika makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake kwasababu jana walishindwa kutoa mustakabali wa kesi hiyo kama walivyoaidi.

Hakimu Mkazi Waliarwande Lema baada ya kumaliza kumsikiliza wakili wa serikali Beata Kitalu ambaye alieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa, hakimu Lema alianza kusema kuwa ;

“Mara ya mwisho wakati tulipoairisha kesi hii upande wa jamhuri ulisema leo mtakuja kutoa mustakabali wa kesi hii wa ama mtaendelea kuleta mashahidi au la ….sasa leo unasema kesi hii imekuja kwaajili ya kutajwa. Kutajwaa tu,kutajwa tuu…’ alisema Hakimu Lema na kuairisha kesi hiyo hadi Agosti  14 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Mbali na Kibanda washitakiwa wengine ni mwandishi wa waraka huo uliochaposhwa na Gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30, 2011 , Samson Mwigamba na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Theophil Makunga. Ambapo wanauliochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30, 2011.

Hadi sasa upande wa ni jumla ya mashahidi wa tatu  wa upande wa jamhuri waliokwisha toa ushahidi tangu kesi hiyo ilipofunguliwa Desemba mwaka 2011.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima  la Jumanne,Julai 30 mwaka 2013 

No comments:

Powered by Blogger.