Header Ads

ALIYEZIRAI KORTINI AFUNGIWA DHAMANA NA MAHAKAMA


Aliyezirai KORTINI afungiwa dhamana
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,  imekataa kumpatia dhamana mfanyabiashara Hussein Amin Suleiman (39), mwenye asili ya Kiasia, anayekabiliwa na makosa miwili ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi ambaye Ijumaa iliyopita, mshtakiwa huyo alianguka na kupoteza fahamu kizimbani baada ya kumsikia Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, akiieleza mahakama hiyo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha hati ya kufunga dhamana kwa mshtakiwa.

Kesi hiyo ambayo Jana ilikuwa kwaajili ya kutajwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Issaya Arufani, Alisema Ijumaa iliyopita alisikili ombi la Wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka AMBAlo lilidai  Kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya KUMFUNGIA dhamana mashitakiwa Huyo chini ya kifungo Cha 148(4) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002.

Hakimu pia alilisikiliza ombi la Wakili wa mashitakiwa Pascal Kamala liliomba Mahakama hiyo iipuuze hati ya DPP na badala yake impatie dhamana mashitakiwa KWA KWA makosa yanayomkabili yana dhamana na kwamba hiyo hati ya DPP haijafafanua ni Sababu zipi za Kumnyima dhamana.

Hakimu Arufani Alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili anikate a ombi la Wakili wa utetezi na kwamba anakubaliana na ombi la upande wa jamhuri ya Kumnyima dhamana mashitakiwa KWA Sababu ya maslahi ya taifa na usalama.

"Kisheria pale DPP anapowasilisha mahakamani hati hiyo ya KUMFUNGIA dhamana mshitakiwa Katika Kesi yoyote ile....Mahakama inakubaliana imefungwa mkono hakiwezi kutoa dhamana KWA mshitakiwa na kwasababu hiyo mahakama hii Katika Kesi hii iliyopo Mbele yangu Mahakama hii inakubaliana ombi la DPP la KUMFUNGIA dhamana mshitakiwa na ninaamuru arejeshwe Gerezani hadi Februali 10 Mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa" Alisema Hakimu Arufani.

Januari 24 mwaka huu. Wakili Kweka alidai kuwa kosa la kwanza linahusu kudharau amri ya mahakama kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la Sea View Upanga, Dar es Salaam,  alifanya marekebisho katika kiwanja  Kitalu Na. 1032 /60 LO No. 51464 huko eneo la Ocean Road  na akafanya marekebisho kitendo ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi  katika kesi Na. 41 ya mwaka 2012 ya Novemba 18, 2013.

Amri hiyo ilikuwa  ikiikataza Kampuni ya Twiga  Paper  Production  Limited  au wakala wake kuvunja au kufanya mabadiliko yoyote  katika nyumba iliyopo kitalu Na. 1032/60LO No. 51464 Ocean Road.

Wakili Kweka alilitaja kosa la pili kuwa ni la kudharau pia amri ya mahakama hiyo  kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la See view Upanga   alivunja  nyumba aliyokuwa akiishi ofisa mwenye cheo cha juu wa serikali mwenye cheo cha  Kamishna wa Fursa Sawa ya Kibiashara na nyumba hiyo ni mali ya serikali ilioyopo kwenye kitalu Na. 1032/60LO.No.51464 iliyopo eneo la Ocean Road  kinyume na amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi katika kesi  namba 240 ya mwaka 2004 iliyotolewa mwaka 2007  kwa Kampuni ya Twiga  Paper Products  Limited  au wakala wa kampuni hiyo  ambapo mahakama hiyo ilitoa amri ya kuzitaka pande zote katika kesi hiyo kuacha nyumba hiyo Na. 3 iliyopo kitalu Na. 1032/60  ibaki kama ilivyo hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika, lakini mshtakiwa huyo alikaidi amri hiyo ya mahakama na kuivunja.

Kweka alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa na kwamba licha kesi inayomkabili mshtakiwa huyo ina dhamana, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka, Dk. Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana mshtakiwa huyo chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Kwa upande wake wakili wa mshtakiwa, Pascal Kamala, aliipinga hati hiyo ya DPP kwa sababu inakwenda kinyume na Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inasema kila mtu ana haki ya kupata dhamana.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alikuwa akimtazama mshtakiwa aliyekuwa amesimama wakati akisomewa mashtaka yake na ilipofika wakili Kweka kuieleza mahakama kuwa DPP amefunga dhamana, mshtakiwa huyo aliyekuwa amesimama alikuwa akianza kufumba macho na kuhema kwa taabu na baada ya muda kidogo mshitakiwa huyo alianguka chini na kuanza kupepewa na ndugu zake.

Hali iliyosababisha hakimu atoke kwenye kiti chake cha enzi na kwenda kumshuhudia mshtakiwa alivyoanguka kizimbani huku mahakama yote ikibaki na taaruki.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Januari 29 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.