Header Ads

WASHITAKIWA KESI YA MAUJI YA DK.MVUNGI WALALAMA MAHAKAMANI


Na Happiness Katabazi
Mshtakiwa mmoja  kati ya washtakiwa 10 wanaokabiliwa na kesi ya KUMUUA KWA makusudi  ALIYEKUWA  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amedai kuwa hawana imani na Mkuu wa Gereza la Segerea  kutokana na kuwahoji vitu ambavyo hawavielewi vinavyohusiana na kesi yao wakati wakiwa gerezani.

Mshtakiwa  John Mayunga (56) alitoa Madai hayo  hayo jana mara baada ya Wakili wa Serikali, Charles Anindo kuwasomea hati mpya ya shtaka la kuua  kwa kukusudia kwa lengo la kumuunganisha mshtakiwa mpya ambaye ni George Geofrey Mulugu (28) mkazi wa Vingunguti na kufanya idadi ya washtakiwa hao kufikia 11.

Akiwasomea upya hati ya Mashitaka  Wakili , Anindo alidai kuwa  washtakiwa hao kwa pamoja  Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa  la mauaji ya kukusudia  kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Anindo  ,  siku hiyo ya  tukio katika  eneo la Msakuzi Kiswegere  lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua kwa kukusudia Dk Sengondo Mvungi ambaye mjumbe  wa Katiba Mpya.

Wakili  Anindo alieleza Kuwa  upelelezi bado haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe ya kutajwa ili kuangalia kama utakuwa umekamilika ama la ambapo hakimu Mkazi, Geni Dudu alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha hadi Februari 13, 2014.

Baada ya Wakili Anindo kumaliza Kusema hayo ,  Mayunga alinyoosha  kidole na kisha kumueleza Hakimu Dudu kuwa wao wanashangazwa na hatu ya Mkuu wa Magereza kuwahoji vitu ambavyo hawavielewi kuhusiana na kesi yake.

“Hatuna imani naye  anatuhoji vitu ambavyo hatuvielewi kuhusu kesi hii, tunahojiwa mara ngapi, polisi tulikwisha hojiwa  na yeye anatuhoji  tena vitu ambavyo hatuvijui.”Alidai mashitakiwa Huyo .

Baada ya kuyatoa malalamiko hayo, Hakimu Dudu alimwambia mshtakiwa huyo kuwa anacheo fahamu upelelezi bado haujakamilika.

Kwa upande  mshtakiwa Chibago Magozi (32) alimwomba  Hakimu Dudu kumfahamisha juu ya haki za mahabusu, hawaruhusiwi kunywa maji wakiwa mahabusu na kubainisha kuwa yeye ni mgonjwa wa kifua  Kikuu anahitaji maji kwa jaili ya afya yake lakini, akiwa mahabusu kwenye mahakama ya Kisutu akinywa maji askari Magereza alimpokonya maji yake.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Dudu alimwambia kuw yeye bado ni mahabusu kosa lake bado halijathibitika hivyo ana haki zote na kumueleza askari magereza aliyekuwemo mahakamani humo ampatie maji yake.

Askari magereza huyo, naye alimwambia hakimu Dudu kuwa  wanapokuwa wanajiandaa kutoka  magereza kuwapeleka mahabusu mahakamani huwa wana andaa na maji ya kunywa  ambayo yanakuwa wamekwisha yakagua kwa ajili ya mahabusu hao kunywa.

Alieleza ,  kwa bahati mbaya mahabusu hao huyachukua  na kuyaoga na kwamba yanapoisha hawawezi kuruhusu watumie maji yoyote ambayo wao hawajayakagua.

Washtakiwa wengine  wanaokabilia na kesi hiyo ni  Chibago Magozi (32)  mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti Machinjioni, John Mayunga (56) mfanyabiashara na mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29)  mkazi wa Vingunguti.

Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu  Losingo (29) na Masunga Makenza (40) dereva na  mkazi wa Kitunda,  Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Zacharia  Msese (33)  mkazi wa Buguruni, Msungwa Matonya (30)  mkazi wa  Vingunguti  na Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala wilayani Kinondoni


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Januari 31 mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.