Header Ads

JAMHURI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA SUMA JKT


Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema kuwa Februali 5 mwaka huu, itatoa uamuzi wake wa kuwaona Kanali wa Jeshi la Kujenga Taifa, Ayoub Mwakangata na wenzake wanaokabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka wana kesi ya kujibu au la.

Hayo yalisemwa Jana na Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya upande wa jamhuri Kusema Kuwa shahidi wa Kumi AMBAE ni machunguzi toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Vang Mkarimoto kumaliza kutoa ushahidi wake  AMBAPO shahidi Huyo akitoa ushahidi wake alidai Kuwa washitakiwa Hao ambao walikuwa wa kumbe wa Bodi ya SUMA JKT walitumia madaraka Yao vibaya kutoa tenda KWA kampun ya ujenzi ya Tacopa bila ya kufuata matakwa ya Sheria ya Manunuzi.

Wakati Huo Huo Mkazi wa Mbagala , Salama Omary Nzala (30) ,Jana alisilisha Mbele ya Hakimu Mkazi Mbando akikabiliwa na kosa la kusafirisha dawa zenye uzito wa gram u 875.46 zenye Thamani ya sh 39.3 aina ya cocaine.

Mkaguzi wa POLISI, Hamis  Said  alidai Kuwa mashitakiwa Huyo aliteka kosa Hilo jAnuari 6 Mwaka huu Katika uwanja wa Kimataifa wa  Julias Nyerere na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Mbando aliarisha Kesi hiyo hadi Januari 29 Mwaka huu, utakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Katika Hatua nyingine Mahakama hiyo Jana iliarisha kutoa hukumu Katika Kesi ya kukutwaa na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba hadi Leo asubuhi.Pia Mahakama hiyo iliarisha kutoa hukumu ya Kesi la jengo linalochungulia Ikulu inayowakabklk  VIGOGO wa Wakala wa Majengo(TBA),Yusunto Tongola na mwenzake  linalochungulia ikulu  hadi Februali  10 Mwaka huu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Januari 16 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.