Header Ads

DC- MTAMBALIKE AFARIKI DUNIA


Na Happiness Katabazi
MKUU wa Wilaya  wa zamani na Kada  wa Chama Cha Mpinduzi(CCM), Deusdedit Mtambalike , amefariki Dunia nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Chanzo Cha kuaminika  kutoka ndani ya familia ya Marehemu Mtambalike, kilisema Marehemu  alifariki Januari 15 Mwaka huu, Katika Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini.

Katika uhai wake marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa wilaya katika sehemu mbali mbali nchini zikiwamo Ngara, Igunga, Tunduru, Ludewa na Muleba. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya jumapili 19/01/2014 Nyumbani kwa marehemu  Kimara Bonyokwa jijini Dar es salaam  majira ya saa sita mchana Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Januari 18 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.