FILIKUNJOMBE UMAUTI UMEMKUTA
Na Happiness Katabazi
AIYEKUWA mgombea Ubunge jimbo la Ludewa(CCM), Deo Filikunjombe , baba Mzazi wa mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga (CCM), Jerry Slaa, Rubani William Slaa na wamefariki Katika ajali ya Helkopta iliyotokea Jana Katika Mbuga ya Selou baada ya Helkopta hiyo kupata itilafu.Filikunjombe anakuwa ni mbunge wa Sita kufariki Dunia.
Filikunjombe ndiye aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC, iliyofanyakazi mbalimbali ikiwemo kuchunguza ufisadi kuhusu Fedha za Akaunti ya Escrow ambayo ripoti Yao ilisababisha nchi kutikisika na Filikunjombe na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo Kudai kutishiwa Maisha.
Ripoti ya Escrow ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospeter Muhongo kujihudhuru na aliyekuwa Katibu Mkuu Eliachim Maswi kusimamishwa Kazi kupishwa uchunguzi wa tuhuma hizo lakini hata hivyo baadae Katibu Mkuu Kiongozi , Ombeni Sefue alitoa ripoti ya uchunguzi na kumsafisha Maswi na Professa Muhongo Kuwa hawana hatia.
Aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Masasi (NLD) na Mwenyekiti Mwenza UKAWA , Emmanuel Makaidi afariki Jana Oktoba 15 Mwaka huu katika hospitali ya Nyangao Mkoani, mkewe Modesta Makaidi.
Makaidi anakuwa ni Mgombea Ubunge wa tano kufariki Dunia Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu.
Waliofariki hadi sasa ni aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Ambaye pia alikuwa Wazij wa Viwanda na Biashara Dk.Abdallah Kigoda ambaye atazikwa Kesho, Jimbo la Arusha Mjini (ACT), Estimih Mallah,Celina Kombani Jimbo la Ulanga Mashariki (CCM), ambaye pia alikuwa Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mtoi Jimbo la Lushoto( Chadema) .
Poleni wafiwa.Mungu aiweke roho yako mahali panapostahili. .16/10/2015.
No comments:
Post a Comment