Header Ads

WAVUNJA AMANI NI MAAJENTI WA SHETANI: NABII KINUNDA



Na Happiness Katabazi

KIONGOZI wa Kanisa la Elshaddai Temple International (ETI), Kanali Mstaafu wa(JWTZ),Nabii Bruno Kinunda  amesema mtu yoyote anayetenda matendo ya Uvunjifu wa sheria,Amani na kudharau mamlaka ni Ajenti wa shetani na baba yake ni shetani.

Nabii Kinunda aliyasema hayo Jana wakati akiongoza Ibada katika kanisa hilo lilipo Basihaya,Boko , Dar es Salaam,ambapo somo Kuu la Jana lilikuwa likizungumzia Amani hasa Kipindi hiki  taifa linafanya uchaguzi Mkuu wake Oktoba 25 Mwaka huu ambapo somo hili  lilikuwa na kichwa cha Habari kisemacho ' TAFUTA AMANI UPATE AMANI' ambalo linapatikana Katika kitabu cha Petro 3:10-12.

Alisema  Amani ni kioo cha Mkristo yoyote Yule na Hilo limeandikwa   Katika kitabu cha Waefesso  2: 13-19  na kwamba Amani inahusisha binadamu wote .

"Unaposema unataka Amani na unailinda uhakikishe unaepuka Kutenda matendo ya Uvunjifu wa Sheria,kukera wenzako, Kuchunga matamshi unayoyatoa kwa watu wanaokuzunguka na kuwaongoza,usiwe mnafki" alisema Nabii Kinunda na kuongeza Kuwa 'Uifuate Amani na uitende'.

Aidha amesema  binadamu yoyote anatakiwa kutii mamlaka kwasababu mamlaka na viongozi wote wamewekwa na Mungu na kwamba kitabu cha Rumi   13:1-12  na Wakorosai  1:16-17 vinathibitisha hayo.

"Hivyo nawaasa wakristo wote na Watanzania kwa ujumla wenye sifa za kupiga kura siku ya kwenda kupiga kura waende kupiga kura kwa Amani na wafu ate maelekezo na kutii maelekezo hayo yatakayotolewa Kwao na mamlaka husika ;

"Kwa sababu  mamlaka /serikali kwa mujibu wa vitabu vya dini vinatueleza mamlaka zote za duniani zimewekwa na Mungu na Mungu tangu zamani alishapanga mtu Fulani  Atakuwa kiongozi wa ngazi Fulani  hivyo Twendeni tukapige kura kwa Amani na utulivu "alisema Nabii Kinunda.

Hata hivyo alisema shetani ndiyo anapenda watu wasiishi kwa Amani na Furaha na kusukuma watu watende matendo ya kuvunja Amani na kudharau mamlaka na Kusema Kuwa binadamu yoyote anayeshiriki kuvuruga Amani kwa kutaka watu wafanye vurugu ,kudharau mamlaka na kwamba mtu yoyote hapa nchini ambaye anatenda matendo hayo baba yake ni shetani na yeye ni Ajenti wa shetani na serikali imchukulie hatua za kisheria.


Aidha alisema mtu anayeitunza amani ananeemeshwa na Mungu na hilo linadhibitishwa Katika Kitabu cha Warumi 26:  5,7,9 na 12.

No comments:

Powered by Blogger.