HAWA NG'HUMBI AUKWAA TENA UDC
Na Happiness Katabazi
Hongera sana rafiki Ng'umbi kwa kuteuliwa tena na Rais Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Ng'umbi ambaye ni mwanamke mpambanaji ,asiyekata tamaa na mvumilivu hata akikosa madaraka.
Mwaka huu Mwana mama huyo msomi ambaye amekuwa akipata sapoti kubwa sana toka kwa mume wake Katika harakati zake kusaka madaraka tangu Mwaka 2000 alipokuwa Diwani viti Maalum kutoka Kata ya Sinza.Mwaka 2010 aligombea Ubunge jimbo la Ubunge lakini kura hazikutisha akashindwa na John Mnyika (Chadema) akashinda nafasi hiyo ya Ubunge.Mwaka 2015 Ng'umbi aligombea tena Ubunge jimbo la Ubungo (CCM) Katika ngazi za kura za ndani ya CCM pia kura hazikutosha na hatimaye Dk.Didas Masaburi (CCM) akaibuka mshindi na CCM ndiyo imempitisha Dk.Masaburi Kuwa mgombea Ubunge jimbo la Ubungo .Na CCM ikamteua Ng'umbi Kuwa Mwenyekiti wa Kampeni za Dk.Masaburi Kazi ambayo amelifanya bila kinyongo watu waliokuwa wakimuunga mkono mama Huyo Walisema huyu ni mwanamke wa aina yake ambaye licha Masaburi ameshinda lakini anampigia kampeni.
Ng'umbi pia ni Mjumbe wa Mkutaño Mkuu wa CCM Taifa,Katika awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne,Rais Jakaya Kikwete aliwahi Kumteua Kuwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Njombe na Mvomero lakini baadae Rais Kikwete alimtupa nje.
Namfahamu mama Huyo ni tofauti kabisa na wanasiasa Wengi wa kike hapa nchini kwanza ni msomi,ananiheshimu na mume wake Ndio amekuwa msaada mkubwa kwake Katika harakati zake tena wazi wazi.
Hongera sana Hawa Mgonja Ng'umbi kuteuliwa tena Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
4/10/2015.
No comments:
Post a Comment