DEREVA WA VICENT NYERERE KORTINI KWA KUKUTWA MLIPUKO
Na Happiness Katabazi
DEREVA wa Mgombea Ubunge Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere( CHADEMA), Godluck Msuya ,HIvi Punde ameshitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Mkoani Mara kwa kosa la kukutwa na milipuko kinyume na Sheria na Mahakama imemfungia dhamana kwasababu ya unyeji wa kosa a alishitakiwa nalo.
Mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Msaloche , Wakili wa Serikali alidai Kuwa mshitakiwa Huyo anadaiwa Kutenda kosa Hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha 25(1),(3) cha Sheria ya Milipuko na upelelezi wa Kesi hiyo bado aujakamilika.
Hata hivyo mshitakiwa Huyo alikana na Hakimu Janeth alisema Mahakama imeamua Kumfungia dhamana kwasababu ya unyeti wa kosa a alishitakiwa nalo na akaairisha Kesi hiyo hadi Novemba 3 kwaajili ya kutajwa na kuamuru mshitakiwa apelekwe gerezani.
Itakumbukwa Kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ilielezwa na Vicent Nyerere kwa umma Dereva huyo wa Nyerere alikuwa kitu Chenye mlipuko Kwenye Gari lake ambacho kilikuwa kimetegwa na mtu asiye fahamu. 20/10/2015
No comments:
Post a Comment