Header Ads

TANGULIA MZEE EMMANUEL MAKAIDI



Na Happiness Katabazi


MGOMBEA Ubunge jimbo la Masasi (NRD) na Mwenyekiti  Mwenza UKAWA , Emmanuel Makaidi afariki leo katika hospitali ya Nyangao Mkoani, mkewe Modesta Makaidi athibitisha.

Makaidi anakuwa ni Mgombea Ubunge wa tano kufariki Dunia Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu.
Waliofariki hadi sasa ni aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Ambaye pia alikuwa Wazij wa Viwanda na Biashara Dk.Abdallah Kigoda ambaye atazikwa Kesho,   Jimbo la Arusha Mjini (ACT), Estimih Mallah,Celina Kombani Jimbo la Ulanga Mashariki  (CCM), ambaye pia alikuwa Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.  Mtoi Jimbo la Lushoto( Chadema) .

Itakumbukwa Makaidi alikuwa akikabiliwa na mkosi wa kuzomewa zomewa jukwaani Katika kampeni zake za kusaka Ubunge jimbo la Masasi kitengo ambacho alisema wanaomzomea zomea na kumpinga 'wanaugua ugonjwa wa kuwashwawashwa'".Nilicheka sana baada ya kusikia akisema Hilo neno .

Pia salamu yake aliyokuwa akipenda kuwasalimia wananchi jukwaani Isemayo "Motomoto ".Na baadhi ya vibweka vyake vingine Vya kisiasa.

Aidha Makaidi a atakumbukwa kwa michango yake mbalimbali aliyoitoa Katika taifa hili. Poleni wafiwa.Mungu aiweke roho yako mahali panapostahili.15/10/2015.

No comments:

Powered by Blogger.