KINGUNGE WEWE NDIO UMEISHIWA PUMZI SIO CCM
Na Happiness Katabazi
OKTOBA 4 Mwaka huu, Mwanasaisa mkongwe nchini Kingunge Ngombare Mwiru alitangaza kuhama CCM na kwamba hajajiunga na Chama chochote cha siasa.
Kingunge alisema mengi Katika mkutano huo na waandishi wa Habari uliofanyika nyumbani wake Jijini Dar Es Salaam na Kusema Kuwa CCM Ina machafu mengi hawezi kuvumilia Kuwa Mwanachama wa Chama hicho na kwamba CCM imeishiwa pumzi.
Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa Haki kwa Mwananchi yoyote kujiunga na Chama chochote hivyo Kingunge ametumia haki yake hiyo ambayo siwezi kumpora Haki yake.
Makala yangu ya Leo itamjadili baadhi ya maneno aliyoyatoa wakati akitangaza kuhama CCM Jana ikiwemo Kauli Kuwa CCM imeishiwa pumzi na Ina uchafu mwingi.
Kwanza Kimsingi nakubaliana na Kingunge Kuwa ni Kweli kuna baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakituhumiwa kwa tuhuma za utovu wa Maadili na yeye Kingunge ni wa kwanza kutuhumiwa na wananchi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo za mkataba wa maegesho wa magari ,na yule ' Mwali wake ' Edward Lowassa .
Ambaye kwasasa Lowassa ni mgombea urais (CHADEMA) ambaye Enzi zile walipokuwa wote CCM alikuwa akienda majukwaani ,Kwenye vyombo Vya Habari kumnadi Kuwa anafaa kupitishwa na CCM Kuwa mgombea urais lakini kwakuwa CCM inavikao vyake kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho ilipuuza ushauri wa Kingunge na vitisho Vya mashabiki wa Lowassa ila kata Ina lake na hadi sasa CCM shwari inaendelea na kumnadi mgombea wake wa urais, Dk,John Magufuli ambaye aandamwi na tuhuma za ufisadi isipokuwa anasifika kwa uchapakazi na uadilifu na rekodi zake safi zipo wazi .
Kingunge ,yaani baada ya 'Mwali' wako yaani 'mgombea wako wa urais unayemtaka wewe kwa Sababu zako' CCM imekataa kumpitisha asiwe mgombea urais , ndipo uliopoanza kuona machafu ya CCM na kuiona imeishiwa pumzi?
Au kwa vile ulivuliwa kwa fedhea Cheo cha Ukamanda wa UVCCM ndipo ulipoanza kuona CCM imeishiwa pumzi na Ina machafu mengi?
Kipindi kile Umepewa madaraka ya Ukuu wa Mkoa,Mjumbe wa Bunge la Katiba,uwaziri wala hakuona CCM imeishiwa pumzi na Ina machafu mengi?
CCM ni taasisi inayoongozwa na wanachama wa chama hicho .Na wewe kabla ya jana kujiondoa ulikuwa mwanachama mkongwe wa chama hicho.Unaposema CCM imeishiwa pumzi ina maana wewe ndio umeishiwa pumzi ndio maana umeondoka CCM.
Kwa sisi wananichezo tunasema Katika kukimbia Riadha au Kupanda Mlima anayeshindwa kumalizia mbio au kufika Kupanda Mlima uwa anakuwa amekumbwa na matatizo likiwemo tatizo la Kuishiwa pumzi.
Wewe Mzee Kingunge Ndio umeshiwa pumzi siyo CCM kwasababu mission yako ya kutaka 'Mwali wako' Lowassa apitishwe na CCM Kuwa rais iligonga Mwamba mchana kweupe na hapo ndipo heshima yako ilipoanza kutiliwa Mashaka Kuwa hata Mzee Kingunge naye ameamua Kujitoa fahamu mchana kweupe na ameshindwa kudhibiti hisia zake za mapenzi kwa mgombea mmoja wa CCM wakati yeye ni miongoni mwa wazee wa CCM ambao kiuungwana hakupaswa kujitokeza hadharani Kuonyesha yeye yupo upande wa mgombea Fulani ndani ya CCM .
Ni hawa hawa baadhi ya wananchi wakiwemo makada wa Chadema Mwaka 2006 , Kingunge alipoteuliwa Kuwa waziri Katika awamu ya kwanza ya serikali ya Kikwete, Ndio walikuwa mstari wa Mbele Kuponda Baraza la mawaziri la kwanza la Kikwete Kuwa ni kubwa sana na kuhoji kwanini Kikwete Kumteua Kingunge Kuwa waziri wakati Kingunge ni Mzee sana,mchawi wa CCM ,fisadi, wa Kura wa CCM na CCM ilimtuma Kingunge kwenda kuiba kura katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya ambao ulileta machana hawezi kuleta Maisha bora KWA Watanzania.
Baada ya kelele za kutaka Rais Kikwete avunje Baraza lake mawaziri kwasababu ni kubwa mno linatafuna kodi za wananchi na Kingunge ni Mzee sana hawezi kwenda na Kasi Mpya,Hali Mpya Nguvu mpya .
Rais Kikwete aliibuka kwa kujitetea na kunukuliwa akisema : "' huwezi kuweka vijana Wengi Katika Baraza la Mawaziri bila kuweka wazee Katika Baraza Hilo kwasababu madhara ya kuweka vijana wote Katika Baraza la mawaziri Moto Utawaka ...nimeamua kumuweka Mzee Kingunge Kwenye Baraza langu la mawaziri kwasababu Wazee ni grisi ya kulainisha mambo"
Sasa Jana nilipoona Kingunge anahama CCM nikajiulize ile Grisi (Kingunge) tuliyoaminishwa na Kikwete Ndio umegeuka Maji ya Betri yaliyokuwa yakitoboa nguo 'CCM' ?
Lakini cha kushangaza Jana baada ya Kingunge kutangaza amehama CCM baadhi ya wafuasi wa vyama Vya upinzani wamejitokeza Kumuunga mkono Kingunge na kumuona Kingunge ni Mwema sana,ataleta Mabadiliko na siyo fisadi tena Kama walivyokuwa wakimuita hapo awali alipokuwa CCM.
Kingunge Mwenyewe amesema ameamua kuacha siasa licha hajatangaza kujiunga na Chama chochote licha Jana wakati Akizungumza na waandishi wa Habari Kingunge pamoja na mambo mengine alisema 'amebaini vijana Wengi wanaitaji Mabadiliko'.
Na Hakuna ubishi Kuwa Kauli mbiu hiyo ya watu kutaka Mabadiliko inatumiwa sana na wana Chadema na UKAWA kwa ujumla.Na sio kosa wala dhambi.
Waswahili wanamsemo wao usemao ' Aliyejamba atakunya tu '. Hipo siku tutajua Kingunge anaenda Chama gani au atakuwa akikiunga mkono Chama gani cha upinzani.
Tuwaulize wale wanaomuona Leo Kingunge sio mtuhumiwa tena wa mkataba wa Maegesho ya Magari ,mwizi wa kura,amechoka kikaakili ,kiutendaji Kama walivyokuwa wa kumpachika Majina hayo alipokuwa CCM, Leo Kingunge amekuwa mtu safi na umri wake umerudi Kuwa kijana na ameachaka Kazi ya uganga wa kienyeji?
Acheni unafki, Mwana CCM akiwa ndani ya CCM mnampachika tuhuma Mbaya,chafu ila Mwana CCM Huyo Huyo akihama CCM basi Kama mnawazimu kichwani mnajiokeza hadharani na kuanza kumpongeza Kuwa ni Mtu safi.
Mlifanya hivyo kwa Edward Lowassa , Fredrick Sumaye walipokuwa CCM Mawaziri Wakuu wapinzani Wengi mlikuwa mkiwaita ni mafisadi lakini walipoamia Chadema basi mnaowaona wasafi ,malaika kana kwamba siyo Nyie mliokuwa mkiwapachika tuhuma chafu hizo.
Leo hii Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa alipofangaza kuhama Chadema mlimgeuka na kumuita msaliti,fisadi ila Enzi zile anakuja ya Chama chenu wala hamkuthubutu kumuita Slaa ni msaliti.
Msimamo wangu huko wazi Kuwa waache waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa awe rais kupitia CCM,waendelee kuhama CCM tena Ndio vizuri sana waende wakaungane na Mfalme wao Lowassa huko waliko waendeleze Michezo Yao CCM iondokane na Makundi na visasi Vya wao kwa wao.
Na kweli tangu Lowassa alipohama CCM,CCM imepumua kwa kiasi kikubwa sana tena hasa Kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ukilinganisha ni Kipindi cha nyuma hususani Enzi zile za kampeni za uchaguzi Mwaka 2010 na uchaguzi za ndani za CCM vurugu za wana CCM zilishamiri sana kutokana na kuwepo kwa makambi ya kusaka urais ambapo kundi la Lowassa lilikuwa likituhumiwa Kuwa na Nguvu kubwa na kucheza rafu za wazi.
Na Matokeo yake CCM Mwaka 2010 ilijikuta ikipoteza baadhi ya majimbo kwenda kwa wapinzani kwasababu ya Makundi hayo,Chuki .
Siyo Siri ,Kingunge huyu ambaye mnadai eti anayajua mengi ya CCM/Serikali alikuwa akimuunga mkono Lowassa wakati akigombea urais kupitia CCM na ushahidi upo,siyo kosa na CCM ilikataa Kumteua Lowassa na wenzake Kuwa wagombea urais kwa Sababu na vigezo walivyojiwekea .
Sasa ni Ngumu sana kwa MTu Kama Kingunge ambaye Ni mtu mzima kiumri ambaye ushauri wake ulikuwa ukiitajika hasa kipindi hiki nchi inaelekea kwenye Mzee aliamua kuficha hisia zake na kuamua kumpigia debe Lowassa ambaye CCM ilimtupa nje Katika kinyang'anyiro cha Urais.
Angeendelea kubaki CCM maana Kama kujidhalilisha alishajidhalilisha muda kwa kukosa kwakwe busara Kama wazee Wenzie Kama rais Benjamin Mkapa,Rais Aman Karume, Jaji Joseph Warioba, Dk.Salim Ahemd Salim na wengine kusimama majukwaani kushawishi CCM impitishe Lowassa Kuwa mgombea urais na hata CCM iliyokataza jina lake alijitokeza hadharani Kulalamika mchakato wa CCM uliokata jina la Lowassa.
Bila kumung'unya maneno Nasema Mzee Kingunge uamuzi wako huu,umefuata historia na heshima yako uliyojijengea kwa muda mrefu ndani na nje ya CCM.
Kwa tunaofuatilia kwa ukaribu siasa za nchi hii tulishabaini muda mapema kabisa Katika awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne, Kingunge ni Kama alishaondolewa Katika nyadhifa nyingi ndani ya CCM,serikali
Alikuwa yupo yupo tu.
Kama Mzee mwenye umri mkubwa kistaarabu ulipoona CCM imepoteza dira ulikuwa Una jukumu la kumuita kijana wako ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete na Kumpa taarifa za machafu hayo ili yafanyiwe Kazi . Je Hilo lilikushinda kujifanya?
Umejinasibu kuwa CCM,TANU ulivishuhudia vikianzishwa unajua uchungu wake
Kwanini Leo hii umeruhusu Nguvu zako ulizoziweka Katika Chama hicho zipotee bure kwasababu ya Hao wakaribifu ambao wamekuja wamekuta Tayari vyama hivyo ulivyoshiriki kuvijenga vimekuwa imara?
Kingunge wewe Ndio umeishiwa pumzi ndio maana umehama CCM baada ya 'Mwali wako' Lowassa kukatwa jina lake na CCM .
CCM ipo imara na Nina kuakikishia itashinda kwa ushindi wa kufulu Oktoba 25 Mwaka huu licha umeirushia tuhuma hizo hivi sasa baada ya CCM kukubana mbavu kila kona.Aibu yako.
Mzee wangu Kingunge nenda salama huko uendako kawasalimie sana ,wewe Ndio umeishiwa pumzi ndiyo maana umeingia mitini ,wenye pumzi zao za kukimbia mbio wapo CCM .Kingunge wewe ndiyo umeishiwa pumzi siyo CCM.
Kingunge wewe ni mchezaji wa zamani Veterani, tunakuheshimu kuwa wewe ni mwanasiasa mkongwe ,sasa tunakushangaa ulivyoamua kulilia kuchezea timu ya mpira wa vijana under 17 ( Serengeti Boys ).
Huko kwa vijana hukuwezi , Kama Kwenye ya Maveterani wenzako(CCM) kumekushinda hata kutoa ushauri kwenye benchi la ufundi pia nako umeshindwa . Huko unakokwenda Kwenye hiyo Timu ya under 17 chenga na kanzu utakazopigwa utaziweza?
Hukutangaza unaamia Chama gani ila wenye akili timamu tumeng'amua unamfuata mwali wako ambaye ni mchovu mwenzako.
Swali la kumuuliza Kingunge Katika dakika Chache zilisosalia nchi ifanye uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu,unaenda kucheza namba ngapi katika hiyo timu ya vijana 'under 17' ambayo umetamba kuwa vijana Wengi wanataka Mabadiliko?
Kama unaenda kumshikia kipaza sauti mwali wako ili baada ya mechi (uchaguzi), upewe hata Kombe la nizamu ,sawa huku ukishuhudia Kombe la ushindi likichukuliwa Timu ya Tingatinga yaani CCM ,sawa.
Tunajua mazoezi ya viungo huwezi,Push Ups,huwezi,mwali wako hawezi pia push up,kukimbia Hamuwezi wote .
Sasa nimechi gani na Sheria zipi zitatumika kuchezesha mechi ya Timu moja ya wachezaji wanatembea Uwanjani dhidi ya wanaokimbia uwanjani?
Watanzania Tumuulize huyu Kingunge Unaijua vizuri historia ya Tanzania na Amani tuliyonayo Tanzania imetokana na nini na imejengwa kwa Misingi gani.
Lakini Kumbe wewe kuwepo Kwenye TANU,CCM lilitokana na ajira siyo utashi wa kutumikia Chama bali ulikuwa ukisaka ajira.
Ndiyo maana baada ya kukosa madaraka Katika Chama Ndio mAana umeamua kusaka ajira lakini Mzee umechelewa umekumbuka Shuka alfajiri sio kinga ya Maralia hata kidogo kwasababu Hakuna Mbu alfajiri mwenye Njaa,wanakuwa wameshiba na wameishaambukiza watu Maralia,wewe ni mmoja walioathirika na Maralia hiyo.
Nakushauri Kingunge amka kitandani uanue chandarua Chako ukiweke dawa Usubiri usiku mwingine utakaokuja(uchaguzi).
Hata hivyo sishangai yote uliyoyasema Jana Mbele ya waanishi wa Habari wakati natangaza kuhama CCM .
Kwasababu ulichokifanya Kingunge Jana ni sawa na wakati wa Mchana Kuku anakula Mchele lakini yeye Kuku tunamkuta analiwa na wali usiku.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
5/10/2015
No comments:
Post a Comment