Header Ads

MTIKILA UMENIUMIZA SANANa Happiness Katabazi

KIFO cha Mwenyekiti wa Chama cha Democraty(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ' Kana Kwamba', Mzee wangu,Mpenzi wangu, swahiba wangu, mpiganaji wangu kimeniumiza sana ,kuniaribia siku ya Leo,kunivuruga akili na kunisababishia nimwage Machozi kwa uchungu.

Mtikila ni miongoni mwa wanasiasa niliokuwa navutiwa nao Sana,na alikuwa ni MTu wangu wa karibu na Chanzo changu Kizuri tu cha Habari bila kumung'unya maneno Mtikila Enzi za Uhai wake aliweza kutumia muda wake mwingi sana kuleta Changamoto Katika system nzima ya Tanzania na alikuwa ni tishio hasa Katika tansia ya Sheria.

Akili yangu ikitulia nitaandika makala ya nilivyomfahamu Mtikila na Mkewe Georgia kwa zaidi ya Miaka 10 nilipokuwa karibu Yao kikazi na familia Yao.Kifo cha Swahiba wangu Mtikila kimeniumiza sana sana. Pole Mama Mtikila Georgia ambaye naye ni mpiganaji kama mumewe Mtikila .

Pichani ni Happiness Katabazi nikimfunga kifungo cha koti swahiba wangu Mtikila enzi za uhai wake.Mtikila amefariki Leo asubuhi katika Kijiji cha Msolwa,Chalinze  Mkoani Pwani  kwa ajali ya Gari.

Mungu aiweke roho yake mahali panapostahili Amina.


4/10/20


No comments:

Powered by Blogger.