Header Ads

KWELI 'KANA KWAMBA' MTIKILA UMEFARIKI
Picha ya kwanza kushoto Rais Jakaya Kikwete akiweka saini Kwenye kitabu maombolezo cha kifo cha Swahiba wangu Marehemu Mwenyekiti wa Chama cha Democraty(DP) , Christopher Mtikila  Leo  katika  mkusanyiko wa kuuaga mwili wa marehemu Mtikila uliofanyika Katika Viwanja Vya Karimjee Dar Es Salaam na mwili unasafirishwa kwenda Ludewa ,Njombe kwaajili ya Mazishi.

Siyo Siri kifo cha Swahiba wangu Mtikila kimeniliza sana ila tangu Jana usiku nimejikuta nikitazama video zake Kwenye mitandao, Habari zake mbalimbali zilizokuwa zikichapishwa Kwenye magazeti,vibweka yake ,Vituko vyake alivyokuwa akivifanya Enzi za Uhai wake naishia kucheka peke yangu na kuona bado Mtikila ni Kama bado MTu anayeishi Katika fikra zangu.Namuita Mtikila 'Kana Kwamba ' kwasababu enzi za uhai wake alikuwa akipenda kutaja neno hilo.By Happiness Katabazi. 7/10/2015.
No comments:

Powered by Blogger.